Maswali magumu kwa atheist

Maswali magumu kwa atheist

Mimi siwezi kuufunga huo mnyororo wa galaxy.

Wewe unaweza?
Kama huwezi

Nani aliziweka au zimejiweka zenyewe?


Sir Isack Newton

(Kumkana Mungu)… ni aina ya Upumbavu

“Kumkana Mungu ni aina ya Upumbavu: Ninapoangalia utaratibu wa jua ninaona kuwa ardhi imekaa sehemu inayostahiki kutoka kwenye jua, ambayo inayoiwezesha kupata kiasi cha kutosha cha joto na mwanga, na hii bila ya shaka halijatokea ghafla.”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point ni kutafuta ukweli uko wapi na hadithi za uongo ziko wapi.
unatafuta ukweli adje sasa kwa kumuhoji mwanadamu mwenzako? Soma vitabu vya dini ndo vina majibu yako.... Likija suala la imani sio mabishano ya mechi za VPL mkuu.
 
Atheism is not a choice, it is just an obvious conclusion of accepting the reality.
kutokuamini jambo la kiroho moja kwa moja ni kuchagua kupinga uwepo wake. Maanaimani ya kiroho haijengwi na mwili bali imani ya kiroho huujenga mwili.
 
unatafuta ukweli adje sasa kwa kumuhoji mwanadamu mwenzako? Soma vitabu vya dini ndo vina majibu yako.... Likija suala la imani sio mabishano ya mechi za VPL mkuu.
Vitabu gani vya dini?

Vitabu vingi vya dini tumeshaonesha uongo wake kwa kuweka contradictions zake hapa.

Taja kitabu cha dini unachoona hakina uongo.
 
Unahakikishaje kila kilicho na umbo lazima kiwe kimetengenezwa na kuumbwa?
Mfano labda kwako wewe kipi kilicho na umbo ambacho hakijaumbwa.
Unaelewa kwamba dhana nzima ya "chanzo" kufuatiwa na "matokeo ya chanzo" ni njozi inayotokana na ujinga wako tu?
Labda nikuulize wewe ni nini chanzo cha ulimwengu na vilivyomo ulimwenguni.
 
Mimi kwa uelewa wangu najua akili zetu za binaadam ni ndogo sana kujua ukuu na sababu za Mungu kufanya haya yote tunayoyaona hivyo huko mbinguni ndio tutajua. Ni sawa na kuchukua maji ya bahari uhamishie kwenye kishimo kidogo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] km kitu hujui kaa kmyaa.
 
Mungu ni zaidi ya ufahamu kinachowaponza wengi ni kutumia akili kumjadili Mungu,unadhani ukisoma biblia Basi umeshamjua Mungu la hasha.kiufupi Mungu ni ufahamu ambayo ni very infinite, Mwanadamu ni sehemu ndogo ya ufahamu huo hutaweza kumjua Mungu simply kwa kutumia logic.By The way Binadamu tuna linear thinking Ambapo tuna starting point na end point.Na ndio Maana swali Kubwa la Binadamu, Mungu alitokea wapi Nani?, alimuumba? .Kwa mtindo huu huwezi kutoboa.Kimsingi Amini kwamba Kuna Nguvu Kubwa Katika ulimwengu wote inayotawala kila kitu isiyo na upinzani .
Bado hujathibitisha kuwa Mungu yupoo.
 
Kama hujui umbo la Mungu, Umejuaje kwanza kwamba huyo Mungu yupo??

Utasemaje hujui umbo la kitu, Halafu useme kipo???

Uko sawa kiakili kweli??
Nimejua kupitia maandiko je ww umejuaje Mungu hayupo.
 
Ulimwengu unachanzo kwasababu kilicho na umbo lazima kiwe kimetengenezwa au kuubwa



Ulimwengu ni mjumuiko wa vilivyomo ardhini na juu ya ardhi.
Haya ulinwengu uliumbwa na nani??
 
Mfano labda kwako wewe kipi kilicho na umbo ambacho hakijaumbwa.

Labda nikuulize wewe ni nini chanzo cha ulimwengu na vilivyomo ulimwenguni.
Kuumbwa ni nini?

Mto unaoshuka chini ya mlima kwa gravity na kutengeneza njia yake, unaumba hiyo njia au hauumbi?

Ulimwengu ni nini? Kwa nini unafikiri ulimwengu una chanzo? Unaelewa kwamba cause and effect is neither essential nor fundamental?
 
Mungu hana chanzo.
Kwasababu hakuna ajuaye umbo la Mungu

Mungu hajaumbwa kwasababu yeye ndiye muumba wa viumbe vyote
Sasa utasemaje kuwa Mungu yupo, na hakuna ajuaye hata umbo lake??

Watu tunataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu.
 
Vitabu gani vya dini?

Vitabu vingi vya dini tumeshaonesha uongo wake kwa kuweka contradictions zake hapa.

Taja kitabu cha dini unachoona hakina uongo.
Kwamba unanuwezo wa kujua uwongo kwenye vitabu kuliko ukweli? haya niambie uwongo uliopo kwenye bibble
 
Back
Top Bottom