Maswali magumu ya Luhaga Mpina mkataba wa DP-World

Hoja ni nzuri sana, ila ieleweke mapema kuwa hakuna nchi inayoitwa Dubai. Kuna nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates - UAE), ambayo hufupishwa Himarati kwa Kiswahili.

Dubai ni sehemu ya Himarati (simply Emirates), kama ilivyo Abu Dhabi ambako ni makao makuu ya Himarati kama ambavyo sisi ni Dodoma. Aidha, Dubai ni jiji kubwa la biashara na anasa UAE kama sisi ilivyo Dar es Salaam.
 
Naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia...hakuna kilichofanyika kwa bahati mbaya kwenye hili saga..
 
Waweja sana goku...
Wadanganyika bado tunauliza maswali....
💪🙌🙏🤙
 
Ndugu Luhaga Mpina anamalizia kwa kushauri TPA iingie mkataba wa HGA na DP World. Mimi nasema hakuna haja!

Tujengeane uwezo na udhibiti katika kuendesha bandari zetu wenyewe, tusitafute kujengewa na kuendeshewa na wengine toka nje.

Tunakosea tunapoacha kutafuta maarifa ya jinsi ya kuvua samaki na kuanza kuomba tupewe kitoweo cha samaki na wanaojua kuvua. Tutabaki ombaomba daima milele!

Tutafute maarifa na teknolojia ya kujenga, kuendesha na kuzidhibiti bandari zetu wenyewe.
 
Ukisikia uzalendo ndio huu, na Wazalendo ndio hawa!.
P
 
Mchakato umekimbizwa mchaka mchaka tu,wabunge hawajapata muda wa kutosha,wananchi pia hvo hvo. Bahati mbaya pia maslahi ya mwenyekiti wa CCM hayawezi kupingwa na mbunge au mwanachama yoyote . Atakuja kiongozi mwingine ambae juzi alikuwepo bungeni kuiunga mkono hoja atataka kuvunja huu mkataba. Tutakuja kumsikia kwamba mafisadi waliuza nchi huku naye akiwemo katika watu waliobariki hii dhambi.
 
Upuuzi na unafiki kama huo ndio unaoligharimu sana taifa. Wanaunga tu mkono hoja ambazo wanajua kabisa ni za ovyo!
 
Mpina kaandika mengi lakini ni chuki zile zile. Alichosahau kusema ni kuwa huo mkataba mama unakwenda kuzaa mikataba midogo midogo inayokwenda kutofautiana na huo mkubwa kwa kuzingatia vigezo vya nchi hii.

Kawatisha watu kwa vipengele viiingi na baadhi ya maneno ya kingereza lakini ni uoga ule ule wa kutoka kivingine.
 


Mkuu ngoja nitulie niisome tena😍😍kama kuna hoja nzito hapa

Huyu mpina ngoja nimtafutie frame kubwa nitengenze picha yake niweke kwangu
 
Kwanini huu mkubwa haufuati vigezo na sheria za nchi?
 
Kautoa kabla ya azimio la Bunge au baadae ya azimio la Tulia
 
Yale makongamano na utopolo wote walitakiwa waongelee haya si vinginevyo, ndio maana nilisema wazi kua mijadala yote iliyofanyika ilikua ni brain washing na kutupoteza direction sisi wananchi wa kawaida.

Ili mwisho tuwe tunabishana wenyewe kama kujenga mnara wa babeli! Aibu kubwa ya karne hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…