Maswali magumu ya Luhaga Mpina mkataba wa DP-World

Mpina umeacha alama katika historia ya nchi hii... haijalishi ulitumika vibaya kipindi cha Magufuli lakini katika hili umesamia ukweli unastahili pongezi
 
Tujufunze tunapochagua Kiongozi tuhakikishe kweli ni mzawa.
maana inaonekana rais ni kama anatumiwa na taifa fulani
 
Hii biashara kama Mungu angempa uhai hayati JPM leo hii wangekuwa wanasaini mkataba wa DPW na serikali.

Na sidhani kama angeibuka mtu na kuanza kuleta maneno ya kuhoji juu ya kinachofanyika, taasisi mbalimbali zingepanga foleni kusifia ujasiri wa awamu ya tano.

Tumpe heshima yake SSH kwa kuwa muwazi na kuruhusu demokrasia ikashamiri kwenye suala zima la huu mkataba, kuliko kuleta akili za kibaguzi kisa asili ya rais.

JPM ndio aliyepigania mpaka reli ya SGR ikajengwa kwa trilioni 17 akijua kuwa uendeshaji wa hawa waarabu utakuja kurudisha gharama zote zinazotumika kwenye ujenzi.

SSH ni mrithi wa biashara iliyokuwa ifanywe na hayati JPM tupunguze hizi roho za chuki.
 
Jitahidi uelimishwe na uelimike. UAE ni muungano wa majimbo saba yenye uhuru wa kufanya biashara na kusimama kama nchi zinazojitegemea.

Dubai, Abu Dhabi na majimbo mengine matano yana uhuru kamili japo yapo chini ya UAE.
 
WATU WANGESEMA KWANI HAWAKUSEMA? DEMOKRASIA SI HISANI, NI HAKI. HAKUNA CHA KUMPONGEA, AKITAKA AUE KAMA MAGUFULI
 
Mbona hakupewa nafasi ya kuchangia bungeni?
 
Mkuu acha kumkashifu Magu mikataba kama hii aliipiga vita hadharani unakumbuka siku alkua anazungumzia mkataba wa bandari ya bagamoyo?? Si ilikua na mambo kama haya na akayapiga chini??
Heshima sio kitu Cha kuombwa mkuu kama unastahili utaipata kitendo Cha wewe kututaka tumpe heshima mtu wako inaonyesha dhahiri Hana na hastahili heshima huwezi kuwafanyia wabongo hivyo wazidi kukuheshimu
Mwenda zake aliwafungua watu akili Sana ndio maana raia wanauelewa na tunaona huu mwitikio na alikua hamkubali uyo dalali wa ili Dili kabisa na alishawahi kumfukuza ikulu ona leo anachotufanyia?? Alistahili kukimbizwa kabisa. Ipo siku sauti za watanzania zitasikika na woga utapotea na ndio itakua mwisho wa mafisadi nchini kwetu. IPO SIKU
 

JPM alikwenda akaonana na Kagame wakajadili kwa kina kuhusu ujenzi wa dry port pale KIgali na ushahidi upo mpaka leo. Akaja akaijenga SGR ili ikikamilika mzigo uje na kuondokea bandari ya Dar. Alikuwa mzalendo na suala hili la bandari linao uzalendo wake, ni kwa maslahi ya nchi Samia ameingia huu mkataba.

Tatizo letu watanzania huwa tunalishwa matango pori halafu tunaingia chaka mazima. Waliokuja na tafsiri potofu ya huu mradi ni wafanyabiashara wanaohisi maslahi yao yanakwenda kupotezwa wakati DPW watakapoanza uwekezaji wao pale bandarini.

Alikuwa akimtuma Hamza Johari mara kwa mara huko Dubai ili kuiwezesha hii deal kukaa sawa. Siwezi kukulazimisha wewe uamini lakini huo ndio ukweli.
 
ushukuriwe mwanaCCM

umejitahidi
 
Huyu ni Mbunge wa CCM! Hivi zile mbuzi nyingine na yule mwenye sura ya tumbilii anayetumikia spika ana majibu hapa!? Huyu hakuruhusiwa kuchangia!
Nyie chawa na kunguni wa ccm msikilizeni angalau huyu mwenzenu anayejitahidi kuoga uchafu asipate chawa!

NB nasikia kuna maandalizi ya maandamano ya kumkaribisha DP world July 1 2023. Yajayo yanafurahisha ngoja tuone!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…