Maswali megine juu ya afya ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869

09 January 2024​

Washington DC​

Maswali Mengi Juu Ya Afya ya Waziri Wa Ulinzi wa Marekani​



View: https://m.youtube.com/watch?v=xHZWbI5w3NY Waziri wa Ulinzi jenerali Lloyd Austin aligunduliwa kuwa na saratani ya tezi dume mnamo Desemba 2023 na alipata matatizo baada ya upasuaji mdogo aliofanyiwa ili kutibu ugonjwa huo , taarifa rasmi kutoka kwa maafisa wa Kituo cha Kijeshi cha Walter Reed iliisema.

Taarifa iliongeza kuwa, baada ya upasuaji mdogo ili kutibu tezi dume ya saratani waziri aliruhusiwa kurudi nyumbani. Lakini baadaye waziri alijisikia vibaya hivyo kukimbizwa kurudi hospitalini kutokana na maumivu makali alitosikia katika mmoja wa mguu wake pamoja na sehemu ya nyonga.

Ikalazimu jenerali Austin kulazwa katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed mnamo Januari 1, na hatimaye, kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi.

Jenerali Austin alibaki hospitalini hadi Jumanne. Taharuki ilizuka kutokana na usiri wa wapi alikuwapo waziri huyo kwa siku kadhaa kutokana inasemekana hata amiri jeshi mkuu ambaye ni rais wa nchi hakupewa taarifa hizo mapema. Hii taharuki inatokana na hali ya kidunia ilivyo sasa ambapo kuna vita ya Ukraine na Russia pia kule Mashariki ya Kati Israel vita vyake katika Gaza na mpaka wake wa Lebanon.

Waziri wa ulinzi hutakiwa aweze kupatikana muda wote kukitokea suala la ulinzi .
Source : NBC News
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…