Maswali na Majibu kuhusu gari aina ya Toyota Voltz

Kama yupo mdau anayetumia gari hiyo anaweza kufunguka zaidi hasa upande wa confortability maana gari zingine ukipanda kama upo kwenye kigoda maana vikiingia shimoni usasikilizia mgongoni. Hahaha
 
Ukiagiza kupitia Beforward kwenye BF Supported I.D weka 500291 utapata punguzo kwenye gharama za kununua gari
 
Sijui chochote kuhusu specifications zake, ila naipenda sana, ukute ina Rims za kueleweka halafu pale juu kuna ki luggage rack au roofrails zenye akili huwa inavutia sana.
 
Hiyo gari bora ununue BMW au Benz, haina tofauti kwa bei ya spear parts
 
Gari nzuri kwa mwonekano ila sijui mambo yake mengine, ila sijui kama inatengenezwa tena maana sijawahi ona iliyotengenezwa mwaka 2005. Labda searching yangu sio nzuri.
 

Mkuu, Toyota Volz ni gari nzuri sana na imara pia ila uimara wake haufiki kwa Rav 4 old.

Utumiaji wake wa mafuta uko poa kwani ina cc1790 ambayo kawaida inakula 1lt/8-11km kutegemea na mwendo wa dereva.

Kwa upande Confitability iko poa sana ndani ina muundo kama Harrier.

Spear zilikuwa adimu kidogo ila kwa sasa naona zimeongezeka so usijali kuhusu hilo.

NB: Kama barabara unayopita haina shida kipindi cha masika chukua yenye 2 wheel bt kama ni njia zetu zile yenye 4 wheel itapendeza bt ulaji wa mafuta unaongezeka pia.

Ukiwa na swali uliza tu maana naijua vilivyo hii gari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…