Jamal Malinzi
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 710
- 650
- Thread starter
-
- #201
Mh Jamal Malinzi ninaswari, ikiwa team akabainika Kuwa imesajiri mchezaji wa nje kama local player (bila ITC) na ikawa imemchezesha mechi kama kumi adhabu yake ni nini?
Lakini Rais tusubiri mpaka lini tena baadhi ya watu waliokuwa wanatuhumiwa kuhonga wachezaji ni viongozi wa kamati ya utendaji ya TFF hapa namzungumzia GEOFREY KABULU na kashfa ya kumpa hela ya hongo ulimboka Mwakingwe akampe Shabani Kado kipindi akiwa MTIBWA ili alegeze Simba ishinde lakini hakuna muendelezo wa uchunguzi na mtuhumiwa kama hivyo mpo nae humo TFF.
Mimi naamini hivi vilabu vikubwa hasa YANGA SIMBA na AZAM (ambaye inasemekana kwa sasa ndio kinara) vinatoa sana hongo/rushwa kupata ushindi.
Na mimi nayasema haya Rais naujua vizuri mpira wa Tanzania nimekulia familia ya mpira Baba angu alikuwa katibu Mkuu wa Shinyanga Shooting Star kipindi ikiwa ligi kuu nilikuwa nipo secondary kuna mambo mengi nilikuwa nayaona hadi ikafikia nikawa naenda uwanjani najua leo mchezaji gani atafungisha eeh kwa nini nisijue wakati usiku niliona anavyopewa mlungula sitting room ya nyumbani.
Hii hali ilikuwa inanifadhahisha sana na si kwa wachezaji tu ata marefa.
MKALIKENYA mbona sasa unataja majina ya watu?
FIFA/CAF wamekuja na kanuni mpya ya club licencing.Ili klabu ipewe leseni ya kushiriki mashindano italazimika,pamoja na mambo mengine,kuwa na youth football system.
Jamal Malinzi kwa nn hata baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi ya juu zaidi kwenye uongozi wa soka TZ bado unang'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa soka mkoa wa Kagera?
1.Je ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza soka Kagera?
2.Kwa nn unapenda kujilimbikia madaraka?
3.Umeiga wapi aina hii ya uongozi kwenye soka ambapo kiongozi wa Kitaifa hataki kuachia uongozi wa mkoa aliokuwa nao kabla hajashinda nafasi ya juu?
Mimi nadhani suala la kuboresha viwanja visiishie kwenye viwanja vikuu vya mikoa na tusiishie tu kwenye sera za fifa,twende extra mile.kwani wachezaji wote tunaowajua wametokea kwenye viwanja vya mtaan,wanacheza katika viwanjapachanya kuna kanuni imepitishwa na FIFA inaitwa "club licencing". Huko mbele tuendako reforms lazima zifanyiken ili vilabu vyetu viweze kupata leseni za kushiriki mechi za kimataifa.Mfano ni hilo la viwanja masharti ya club licencing ni kuwa kila klabu lazima iwe na access na uwanja wa mazoezi na wa mechi.Masharti mengine ni klabu kuwa na waajiriwa hasa watendaji muhimu,kuwa na youth programme n.k.
Jamal Malinzi kwa nn hata baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi ya juu zaidi kwenye uongozi wa soka TZ bado unang'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa soka mkoa wa Kagera?
1.Je ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza soka Kagera?
2.Kwa nn unapenda kujilimbikia madaraka?
3.Umeiga wapi aina hii ya uongozi kwenye soka ambapo kiongozi wa Kitaifa hataki kuachia uongozi wa mkoa aliokuwa nao kabla hajashinda nafasi ya juu?
Ndugu Rais kuna thread imeanzishwa ikizungumzia juu ya wewe kuendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA mimi mawazo yangu yalikuwa ni haya chini naomba majibu yako ndugu rais ukizingatia uzito wa hoja niliyotoa.
Mimi nadhani sio sahihi kwa MALINZI kuendelea kuwa MWENYEKITI wa KRFA ata kama sheria zipo kimya busara itumike hapo aachie hiyo nafasi mtu mwingine.
Kwa mfano uwanja wa Kaitaba unawekewa nyasi za bandia na FIFA kwa maombi maalumu ya TFF hapo kwa nini tusipate shaka kuwa ametumia nafasi yake kama rais na mwenyekiti kuhakikisha hilo ukizingatia viwanja vyenye mahitaji si Kaitaba peke ake, kwa nini wasingeombewa Sokoine ambao uwanja wao ulisimamishwa kwa pitch kuwa mbovu na pia wana timu mbili ligi kuu tena mbeya city imeonesha mwamko mkubwa na uwanja huo umekuwa wa pili kuingiza mapato baada ya uwanja wa taifa.
Mimi nadhani ifike mahali rais wetu Malinzi alione hili na ajiuzuru mara moja sababu inaleta mgongano wa kimaslahi kama nilivyoeleza hapo juu.
Mkuu malinzi naheshimu sana uwezo wako toka kwa rashidi matumla hadi sasa, ninachosema kwa leo kuwa nilikuwa na big expectations kwa mr tenga lakini alichoki deliver sicho nilichotegemea, naomba kwako isiwe hivyo tunacho au ninachokitegemea ndo tukipate
Jamal Malinzi
Jamal Malinzi
Kwa mara ingine unaleta mzaha kwenye maswali muhimu sana!Onyesha japo seriousness kidogo!Waambie hivi KRFA HAUNA KITU UTACHOSHINDWA kuwafanyia KRFA kwa nafasi yako ya U-Rais wa TFF!
Tuache majibu ya kisiasa kwenye issue muhimu kama hizi!JIUZURU haraka maana unaonyesha wazi wazi u dikteta wako!!
Jamal Malinzi ACHIA MADARAKA kwa wengine!Umeonyesha picha mbaya sana kwa kweli!Kuna watu wengi sana KRFA wana weza kuongoza na kauli yako kama walikuambia kuwa"kumbe uligombea KRFA kama njia ya kukupeleka TFF"na eti kauli hii ndiyo ilikufanya USIACHIE MADARAKA ya KRFA ni kauli ya KUPUUZWA kwa kila mpenda maendeleo ya soka!Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?
Malafyale nchini Tanzania kuna umiliki wa viwanja wa aina nne,vyama vya siasa,halmashauri makampuni binafai na TFF.Karume ni mali ya TFF,Kaitaba,nyamagana na st george Moshi ni hlamshauri,manungu na Azam kampuni binafsi na uhuru serikali.Hizi miliki zina utendaji tofauti na ukitaka kujenga nyasi bandia kuna viwanja huwezi kuamka ukamwambia mmiliki nimekuja kukuwekea artificial turf fungua mageti......you know what i mean???