Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Mh Jamal Malinzi ninaswari, ikiwa team akabainika Kuwa imesajiri mchezaji wa nje kama local player (bila ITC) na ikawa imemchezesha mechi kama kumi adhabu yake ni nini?

Hilo litakuwa ni kosa la wote,Federation kwa kumuidhinisha acheze bila ITC,klabu husika kuleta jina la mchezaji asiye na ITC na mchezaji mwenyewe kutofuatilia usajili wake kama uko sawa.Ndio maana wiki iliyopita FA ya uingereza haikuwanyang'anya pointi Sunderland bada ya kumchezesha mechi nne mchezaji wa Korea bila ITC.Basicaly suala la ITC liko more adminstrative kuliko technical.Ukiwa na kadi nyekundu ukacheza mechi ifuatayo na ikajulikana timu yako itanyang'anywa ushindi,thats technical.
 
Last edited by a moderator:
Lakini Rais tusubiri mpaka lini tena baadhi ya watu waliokuwa wanatuhumiwa kuhonga wachezaji ni viongozi wa kamati ya utendaji ya TFF hapa namzungumzia GEOFREY KABULU na kashfa ya kumpa hela ya hongo ulimboka Mwakingwe akampe Shabani Kado kipindi akiwa MTIBWA ili alegeze Simba ishinde lakini hakuna muendelezo wa uchunguzi na mtuhumiwa kama hivyo mpo nae humo TFF.

Mimi naamini hivi vilabu vikubwa hasa YANGA SIMBA na AZAM (ambaye inasemekana kwa sasa ndio kinara) vinatoa sana hongo/rushwa kupata ushindi.

Na mimi nayasema haya Rais naujua vizuri mpira wa Tanzania nimekulia familia ya mpira Baba angu alikuwa katibu Mkuu wa Shinyanga Shooting Star kipindi ikiwa ligi kuu nilikuwa nipo secondary kuna mambo mengi nilikuwa nayaona hadi ikafikia nikawa naenda uwanjani najua leo mchezaji gani atafungisha eeh kwa nini nisijue wakati usiku niliona anavyopewa mlungula sitting room ya nyumbani.

Hii hali ilikuwa inanifadhahisha sana na si kwa wachezaji tu ata marefa.

MKALIKENYA mbona sasa unataja majina ya watu?
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi kwa nn hata baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi ya juu zaidi kwenye uongozi wa soka TZ bado unang'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa soka mkoa wa Kagera?
1.Je ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza soka Kagera?
2.Kwa nn unapenda kujilimbikia madaraka?
3.Umeiga wapi aina hii ya uongozi kwenye soka ambapo kiongozi wa Kitaifa hataki kuachia uongozi wa mkoa aliokuwa nao kabla hajashinda nafasi ya juu?
 
Kiukwel hata km katiba ya TFF haijakataza kuhodhi madaraka ya namna hii ( rais wa TFF na mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa) lakn sifikiri kama ni busara kujilimbikizia madaraka ambayo yanahusiana moja kwa moja,
ushaur wng mh. Rais tafadhali waachie wengine wapate kuongoza mkoa wako.
 
MKALIKENYA mbona sasa unataja majina ya watu?

Ndugu Rais sijui kama ulifanikiwa kupewa tamaduni na desturi zetu humu JF? humu hatufichi kitu tunaruhusiwa kutuhumu lakini si kuhukumu tena kwa kutaja majina mchana kweupeee na kwa kuzingatia hilo wewe unaweza husijibu nilichokuuliza lakini unaweza kufanyia kazi mawazo yangu kama kweli una nia ya dhati ya kukomesha hivyo vitendo.

Weka urafiki pembeni kaa ukijua vinara wa kununua wachezaji wengine ni viongozi wa TFF nakuonea huruma una kazi nzito mbele yako kama hutaamua kujitenganisha nao eti pengine walihusika na mchakato wa wewe kuingia madarakani.

Bado tuna imani na wewe fanya kazi kwa kuzingatia misingi ya uadilifu na kutukuogopa ata kimvuli chako.
 
FIFA/CAF wamekuja na kanuni mpya ya club licencing.Ili klabu ipewe leseni ya kushiriki mashindano italazimika,pamoja na mambo mengine,kuwa na youth football system.

Youth Football System, sawa. Inamaanisha uwepo wa vilabu HAI vya watoto sio? Mtashikia bango hili kwa utimilifu?
 
Jamal Malinzi kwa nn hata baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi ya juu zaidi kwenye uongozi wa soka TZ bado unang'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa soka mkoa wa Kagera?
1.Je ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza soka Kagera?
2.Kwa nn unapenda kujilimbikia madaraka?
3.Umeiga wapi aina hii ya uongozi kwenye soka ambapo kiongozi wa Kitaifa hataki kuachia uongozi wa mkoa aliokuwa nao kabla hajashinda nafasi ya juu?

Swali zuri.. Ndo yale yale ya enzi za chama kimoja, CCM enzi zile Waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais
 
Ndugu Rais kuna thread imeanzishwa ikizungumzia juu ya wewe kuendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA mimi mawazo yangu yalikuwa ni haya chini naomba majibu yako ndugu rais ukizingatia uzito wa hoja niliyotoa.

Mimi nadhani sio sahihi kwa MALINZI kuendelea kuwa MWENYEKITI wa KRFA ata kama sheria zipo kimya busara itumike hapo aachie hiyo nafasi mtu mwingine.

Kwa mfano uwanja wa Kaitaba unawekewa nyasi za bandia na FIFA kwa maombi maalumu ya TFF hapo kwa nini tusipate shaka kuwa ametumia nafasi yake kama rais na mwenyekiti kuhakikisha hilo ukizingatia viwanja vyenye mahitaji si Kaitaba peke ake, kwa nini wasingeombewa Sokoine ambao uwanja wao ulisimamishwa kwa pitch kuwa mbovu na pia wana timu mbili ligi kuu tena mbeya city imeonesha mwamko mkubwa na uwanja huo umekuwa wa pili kuingiza mapato baada ya uwanja wa taifa.

Mimi nadhani ifike mahali rais wetu Malinzi alione hili na ajiuzuru mara moja sababu inaleta mgongano wa kimaslahi kama nilivyoeleza hapo juu.
 
Mkuu malinzi naheshimu sana uwezo wako toka kwa rashidi matumla hadi sasa, ninachosema kwa leo kuwa nilikuwa na big expectations kwa mr tenga lakini alichoki deliver sicho nilichotegemea, naomba kwako isiwe hivyo tunacho au ninachokitegemea ndo tukipate
 
pachanya kuna kanuni imepitishwa na FIFA inaitwa "club licencing". Huko mbele tuendako reforms lazima zifanyiken ili vilabu vyetu viweze kupata leseni za kushiriki mechi za kimataifa.Mfano ni hilo la viwanja masharti ya club licencing ni kuwa kila klabu lazima iwe na access na uwanja wa mazoezi na wa mechi.Masharti mengine ni klabu kuwa na waajiriwa hasa watendaji muhimu,kuwa na youth programme n.k.
Mimi nadhani suala la kuboresha viwanja visiishie kwenye viwanja vikuu vya mikoa na tusiishie tu kwenye sera za fifa,twende extra mile.kwani wachezaji wote tunaowajua wametokea kwenye viwanja vya mtaan,wanacheza katika viwanja
Vibovu havielezeki,mf unakuta kiwanja kipo mlimani goli moja lipo bonden lingine lipo mliman,vingine vimejaa mchanga,vingine vigumu sana ,vina mashimo kwa staili hii tutapata timu na wachezaji wazuri kweli wanaopanda daraja na wengine wanaokua na kujifunza mpira?nadhan mngetafuta wadhamini na mshirikiane na wizara ya elimu na ile ya michezo ili kuboresha hivi viwanja ambavyo vingi vinamilikiwa na shule na vingine ni viwanja vya wazi.start from grassroot,kama kweli tunataka tuendeleze mpira wetu twende mtaan,tusiwatafute tu wachezaji bali tuwaboreshe viwanja vyao pia,haipendezi kuona raisi wa TFF anafuatilia vipaji kwenye viwanja vya aina hii
 
Jamal Malinzi kwa nn hata baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi ya juu zaidi kwenye uongozi wa soka TZ bado unang'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa soka mkoa wa Kagera?
1.Je ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza soka Kagera?
2.Kwa nn unapenda kujilimbikia madaraka?
3.Umeiga wapi aina hii ya uongozi kwenye soka ambapo kiongozi wa Kitaifa hataki kuachia uongozi wa mkoa aliokuwa nao kabla hajashinda nafasi ya juu?

Malafyale haya uliyayaongea hapa yote niliyaeleza kwenye mkutanoo mkuu wa KRFA,mwisho niliulizwa "hivi Malinzi kumbe ulituomba uenyekiti wa KRFA ili utupandie mgongoni kuwa Rais wa TFF?".
Malafyale nisaidie jibu la swali hili niwapelekee wana Kagera.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Rais kuna thread imeanzishwa ikizungumzia juu ya wewe kuendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA mimi mawazo yangu yalikuwa ni haya chini naomba majibu yako ndugu rais ukizingatia uzito wa hoja niliyotoa.

Mimi nadhani sio sahihi kwa MALINZI kuendelea kuwa MWENYEKITI wa KRFA ata kama sheria zipo kimya busara itumike hapo aachie hiyo nafasi mtu mwingine.

Kwa mfano uwanja wa Kaitaba unawekewa nyasi za bandia na FIFA kwa maombi maalumu ya TFF hapo kwa nini tusipate shaka kuwa ametumia nafasi yake kama rais na mwenyekiti kuhakikisha hilo ukizingatia viwanja vyenye mahitaji si Kaitaba peke ake, kwa nini wasingeombewa Sokoine ambao uwanja wao ulisimamishwa kwa pitch kuwa mbovu na pia wana timu mbili ligi kuu tena mbeya city imeonesha mwamko mkubwa na uwanja huo umekuwa wa pili kuingiza mapato baada ya uwanja wa taifa.

Mimi nadhani ifike mahali rais wetu Malinzi alione hili na ajiuzuru mara moja sababu inaleta mgongano wa kimaslahi kama nilivyoeleza hapo juu.

Malafyale nchini Tanzania kuna umiliki wa viwanja wa aina nne,vyama vya siasa,halmashauri makampuni binafai na TFF.Karume ni mali ya TFF,Kaitaba,nyamagana na st george Moshi ni hlamshauri,manungu na Azam kampuni binafsi na uhuru serikali.Hizi miliki zina utendaji tofauti na ukitaka kujenga nyasi bandia kuna viwanja huwezi kuamka ukamwambia mmiliki nimekuja kukuwekea artificial turf fungua mageti......you know what i mean???
 
Last edited by a moderator:
Mkuu malinzi naheshimu sana uwezo wako toka kwa rashidi matumla hadi sasa, ninachosema kwa leo kuwa nilikuwa na big expectations kwa mr tenga lakini alichoki deliver sicho nilichotegemea, naomba kwako isiwe hivyo tunacho au ninachokitegemea ndo tukipate

tuombeane heri
 
Malafyale haya uliyayaongea hapa yote niliyaeleza kwenye mkutanoo mkuu wa KRFA,mwisho niliulizwa "hivi Malinzi kumbe ulituomba uenyekiti wa KRFA ili utupandie mgongoni kuwa Rais wa TFF?".
Malafyale nisaidie jibu la swali hili niwapelekee wana Kagera.
Jamal Malinzi
Kwa mara ingine unaleta mzaha kwenye maswali muhimu sana!Onyesha japo seriousness kidogo!Waambie hivi KRFA HAUNA KITU UTACHOSHINDWA kuwafanyia KRFA kwa nafasi yako ya U-Rais wa TFF!

Tuache majibu ya kisiasa kwenye issue muhimu kama hizi!JIUZURU haraka maana unaonyesha wazi wazi u dikteta wako!!
 
Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nategemea upo njema sana na unaendelea na jukumu la kujenga taasis kubwa sana ya mpira hapa tanzania mm nina maswali mawili mpaka matatu.
I)Ni nini mustakabali wa mwalimu wa Taifa stars?
II)Kipi kinachokuzuia ww jamal malinzi usiachie cheo cha mwenyekiti wa chama cha mpira cha kagera ili hali ww tayari n rais wa tff? huoni kukumbatia vyeo viwili n kujitengenezea mashaka kwa wapenda soka kuwa maamuzi yako hayatakuwa na uhalisia??
III)Vpl imemalizika je nyie kama tff mmekumbana na changamoto zipi na mmejipangaje kukabiliana nazo ukizingatia mfumo na ufadhili kwa timu ambazo hazina majina??

Naomba majibu ya maswali yangu ili niweze kuuliza mengine zaidi
 
Malafyale ukitaka niwe najibu hoja zako tumia lugha ya uungwana,who is joking here?
Jamal Malinzi ACHIA MADARAKA kwa wengine!Umeonyesha picha mbaya sana kwa kweli!Kuna watu wengi sana KRFA wana weza kuongoza na kauli yako kama walikuambia kuwa"kumbe uligombea KRFA kama njia ya kukupeleka TFF"na eti kauli hii ndiyo ilikufanya USIACHIE MADARAKA ya KRFA ni kauli ya KUPUUZWA kwa kila mpenda maendeleo ya soka!

ACHIA MADARAKA ya KRFA uonyeshe ukomavu wako wa dhana nzima ya utawala bora!
 
Last edited by a moderator:
Pesa za waekezaji zinafanya watu kutoka Kabla lengo kutimiza inakuwa ngumu kwao ila kila unavyongangania mambo yanazidi kuharibika. Pesa mwanaharamu ukiiwekea kwajili ya moyo wako tu.
 
Malafyale nchini Tanzania kuna umiliki wa viwanja wa aina nne,vyama vya siasa,halmashauri makampuni binafai na TFF.Karume ni mali ya TFF,Kaitaba,nyamagana na st george Moshi ni hlamshauri,manungu na Azam kampuni binafsi na uhuru serikali.Hizi miliki zina utendaji tofauti na ukitaka kujenga nyasi bandia kuna viwanja huwezi kuamka ukamwambia mmiliki nimekuja kukuwekea artificial turf fungua mageti......you know what i mean???

Ndugu Rais kwanza hoja yangu ya msingi ilikuwa ni wewe kuachia nafasi ya uenyekiti KRFA na nikajenga dhana ya mgongano wa kimaslahi nadhani hujajibu hoja ya msingi ya wewe kuachia nafasi ya uenyekiti wa soka mkoa wa Kagera.

Lakini pili majibu yako hayajaniridhisha Ndugu Rais umezungumzia umiliki kama ni kikwazo cha kufanya mabadiliko kwenye viwanja vyetu sasa hapa nataka kujua je mlijaribu kufanya hivyo sokoine mkakwama au hii dhana unaitoa wapi pia uniambie ni kwa nini imekuwa rahisi Kaitaba kuliko Jamhuri Morogoro na kwa nini ilikuwa rahisi kwa Gombani pemba na uwanja wa uhuru.
 
kama Bwana Malinzi havunji sheria yeyote basi sioni kama kuna haja ya yeye kuachia uongozi wa KRFA labda tuu iwe kwasababu ya ufanisi na kuachia wengine
 
Back
Top Bottom