Maswali na ushauri kwa Malinzi


Naomba ufafanuzi kuhusu kuhamisha ofisi za TFF na kujenga kitega uchumi pale Karume.
Ufafanuzi na uwazi ni muhimu ili wadau wa soka wajue kinachoendelea.
Tumeona jinsi ufisadi ulivyoingia kwenye maeneo kama hayo. Chukua mfano wa UVCCN na UWT. Hivi kweli jumuiya hizo zimenufaika?
TFF wasije kuwa wapangaji kwenye eneo lao wenyewe. Nani alitoa uamuzi huo? Kamati ya utendaji au mkutano mkuu.
Nahisi suala hili linahittaji baraka za mkutano mkuu kama ajenda muhimu
Nani mwekezaji? Yapi makubaliano na TFF? Gharama yake na vitu kama hivyo
 
Last edited by a moderator:
uko sahihi kabisa na hoja zako ni za msingi.Wakati wa contract reviews yote haya tutayazingatia.

kuna gazeti hivi karibuni liliandika kwamba ulikwenda kuonana na waziri mkuu aliyejiuzulu Lowassa kumueleza mikakati ya uongozi wako, je ni kweli? kama ni kweli ni kwasababu gani iliyofanya uende kwake?
 
Jamal Malinzi
Naomba kujua kuhusu mashindano ya Kombe la Taifa, Je mtayarudisha lini?

Kiukweli nilikuwa mshabiki wa kombe hili sana maana lilikuwa likiibua vipaji vingi na ningependa mtakapo lifufua mruhusu liwe ni la Vilabu na sio Mikoa na mruhusu timu yeyote hata kama ni ya Mchangani ishiriki kama ilivyo kwa kombe la Carling/Capita one Cup huko uingereza ambapo mashindano ni ya mtoano na yana shirikisha timu zote nchi nzima no mata ni kubwa kiasi gani.

Naamini wazamini wapo wengi wali tayari kudhamini na Kuonyesha haya mashindano naamini hata Makampuni ya soda/Maji/ simu/ na mengineo yalio kosa nafasi kwenye Ligi kuu, itakuwa ni nafasi yao kushindania na huku waweze kujitangaza.

Na ni hivyohivyo kwa makampuni ya Tv. Kama Zuku, Dstv, Startimes, Ting, Continetal/Digitec wanaweza kupata fursa pia ya kugombania tender ya kuonyesha hii michuano pia.

Na kama utakubaliana na mimi nina ushahuri zaidi wa jinsi ya kupata mapato na kuendesha hii ligi ya Mtoano na iwe ya Ufanisi.Maana kwenye Kombe kama hili tunaweza tukashuhudia timu yangu ya mtaani ikicheza fainali au hata robo fainali na Yanga/simba au ata Timu yeyote ya Ligi kuu.
 
Last edited by a moderator:
Hon. Jamal Malinzi leo 04/02/14 nimesikia BBC wakitangaza kuwa unafanya mazungumzo na mataifa yaliyoendelea kisoka ili yatupatie vifaa vya michezo kama vile VIATU VILIVYOTUMIKA ili tuvigawe mashuleni; kuna ukweli katika hili? Kama 'NDIYO', kwa nini viatu vilivyotumika?
 
Last edited by a moderator:
Eng Jamal Malinzi,

Naomba maelezo kwa maswali yafuatayo
1) Nimesoma kuwa TFF imeteua walimu 40 kwenda kusaka vipaji ili kuboresha timu ya Taifa. Binafsi nasema haya ni matumizi mabaya au ubadhilifu wa pesa. Timu haiwezi kuundwa na walimu 40, mwalimu huchagua wachezaji kutegemea muundo wa uchezaji anaoutaka au atakao utumia.

Hivi kweli mko serious au sasa mnataka kufurahishana? Hii haijawahi tokea duniani, timu inachaguliwa na walimu 40?

wewe umepata kuwa katibu mkuu wa Yanga, na unajua moja ya matatizo yamekuwa yakizikumba timu zetu ni wachezaji kusajiliwa na uongozi, unakuta huyo mchezaji haendi na mfumo wa mwalimu, matokeo yake watu wanalalamika kuwa timu imeua uchezaji wa mtu fulani.

ninachokiona, ni kweli mna nia tufanikiwe lakini yaelekea hamjui ni kwa nini tumekwama.

2) Mapatao ya milangoni
Wewe umepata kuwa kiongoziwa juu kabisa katika klabu ya Yanga, sasa ukirejea kwenye kwenye mgawo wa mapato ya mlangoni na gharama ambazo timu inaingia kuiweka au kuiandaa timu, je unaona kweli kuna uhalali na makato yanayotolewa?

Hivi tunategemea kweli soka letu likuwe kwa dhuluma kama hii? VAT, hiyo nakubali, kwani bila hiyo hata huu uwanja wa Taifa tusingekuwa nao, lakini hayo makato mengine , asilimia inayokatwa ni kubwa mno na ni wizi mweupe.

3) Mkataba wa Azam TV.
Hili najua ni swala zito na wewe unaweza kuonekana kama unaisaidia Yanga, lakini tuwe wa wakweli, timu zetu na hasa Yanga na Simba, ambazo ndo zinategemea mapato yake makubwa kupitia kiingilio, hivi ni sahihi walipwe mil 3, kwa mechi? wakati wanaingiza hela nyingi.

Ukweli inapoonyeshwa live, kwa kiasi kikubwa inapunguza watu kwenda uwanjani, je hili TFF mlilitazama? na kwa nini klabu zisishhirikiswe kujadili haki yao?

naomba niishie hapa kwa leo
 
kuna mpango gani wa kuboresha matangazo ya moja kwa moja toka national stadium maana ni tofauti kabisa na tunapoangalia mechi za wenzetu kuanzia muonekano wa picha, matukio, slow motion hapo kwetu bado sana. nini tatizo hasa mkuu? vifaa? wataalamu wa kuendesha mitambo? ama?
 
awali ya yote nikupongeze kwa ujasiri wako,kuamua kukubali challenges,then nijaribu kutoa mawazo yangu................
wadau wengi wasisitiza kuwa bila ya academy za soka ili kuandaa vijana, tanzania haitapiga hatua ktk soka la kimataifa.hofu yangu kuwa utafiti unaonyesha uingereza,ufaransa,ujerumani na wengine wana academy nyingi sana lakini ukiitazama uingereza hawafanikiwa vya kutosha,ufaransa wanabebwa na mamluki(foreigner) nawaza endapo tutaendeleza academy halafu tukashindwa itakuwaje?the way forward...........

pamoja na uwepo wa academy ishu kubwa ni exposure TFF ikae meza moja na serikali kama kuna vijana wanapelekwa ulaya na amerika kusoma fani nje ya kwanini tusiteue vijana bila upendeleo wenye vipaji halisi wakapelekwa kama vile spain,france,portugal kwa idadi maalumu hasa washambuliaji na mabeki wengi ila viungo wachache wakawe trained kiasawasawa naamini baada ya miaka 5 tutakuwa na mabadiliko japo kidogo then 10 yrs to come its amazing.......

lingine TFF iunde national supporters group ambalo kazi yao itakuwa ni kushangilia tu mwanzo mwisho kama ilivyokuwa kidedea kwa Simba SC au mdumange,Hawa supporter wewe trained na taasisi ya sanaa bagamoyo au JKT wafundishwe nyimbo za uzalendo ili wao ndio watakuwa waanzilishi ktk kushangilia pale Taifa Star inapopeperusha bendera ndani au nje au timu yoyote itakayo kuwa inawakilisha taifa,iwe simba,yanga,azam ,mtibwa au mbeya city.

mwisho nakushauri unapouunda kamati tafadhali achana na mazoea jaribu kukisumbua kichwa tafuta watu makini ambao wataweza kukusaidia kufikisha mpira wa TZ pale unaamini utatupeleka,TZ hivi sasa wasanii ni wengi kuliko unavyofikiria achana na wale wanotaka kushine majina ili wakagombee ktk siasa hawana malengo ya kukuza mpira,wao ni tantarila tu.pia jitahidi kuto elimu kwamashabiki wa soka hasa vilabu vikubwa watambue kuwa wachezaji wanastahili kupata malipo halisi kutokana na jasho laowajanja wachache wasiendekezwe kuendelea kudhulumu haki zao...tulisimamie hilo la wachezaji ili endapo watapata haki yao sahihi watasaidia kupambana ktk kuendeleza mpira.....
naomba kuwasilisha.
 

ahsante kwa ushauri. Mikataba ambayo nimeikuta wajibu wangu ni kuiheshimu hadi kipindi chake kimalizike na ndipo tuiboreshe,ingawa mingine kwa kweli inabidi ifanyiwe kazi haraka kwa usalama wa watazamaji.
 
Mokoyo kwa vyovyote vile tutaongeza timu za premier league na kuanzisha mashindano mapya ili vijana wetu wapate angalao mechi 40 za kucheza kwa mwaka.Mabadiliko haya yatakuja msimu ujao.
 
Last edited by a moderator:

Umuhimu wa TFF kuwa na vyanzo mbadala vya mapato uko wazi na unaeleweka,TFF haiwezi kuendelea kutegemea mapato ya milangoni katika kugharimia shughuli zake.
Maamuzi ya kuwekeza uwanja wa karume sio ya leo ni ya siku nyingi,nimeyakuta.Kikubwa ni kuwa TFF haiko tayari kuweka rehani ardhi yake kwa ajili ya mradi huu.Taratibu zitafanyika ili financing ya mradi huu iendane namatakwa ya TFF.Ili kukidhi azma hii tutahakikisha financier anakuwa ni taasisi inayomilikiwa asilimia 100% na serikali
 
Mokoyo kwa vyovyote vile tutaongeza timu za premier league na kuanzisha mashindano mapya ili vijana wetu wapate angalao mechi 40 za kucheza kwa mwaka.Mabadiliko haya yatakuja msimu ujao.
Jamal...

Kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya Mkataba wa Azam TV ambao ni dhahiri haukuuingia wewe na safu yako.....Kwa maono yako unaonaje juu ya malalamiko haya ya vilabu hususan Klabu ya Yanga?....Je kuzipa Kalbu Tshs. 100,000,000/= kwa msimu kunazisaidia Timu?....

Ni kwa nini Timu zisipewe fursa ya kushiriki katika majadiliano ya Mikataba baina ya TFF na Wadhamini (hasa ule wa VodaCom)....

Pia mna mpango gani na Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen ambaye tayari ameonekana hana msaada wowote kwa Timu hiyo?

Na mwisho, mbona makato ya mapato kwa mechi za Ligi Kuu yamekuwa ni mengi na hayavisaidii vilabu?
 

uko sahihi kabisa na ninaomba nikuhakikishie muda si mrefu tutaanzisha mashindano kama FA cup ya Uingereza.
 
ahsante kwa ushauri. Mikataba ambayo nimeikuta wajibu wangu ni kuiheshimu hadi kipindi chake kimalizike na ndipo tuiboreshe,ingawa mingine kwa kweli inabidi ifanyiwe kazi haraka kwa usalama wa watazamaji.

Ndugu rais nachojua mimi ata kabra mkataba haujafikia mwisho pande mbili za mkataba zinaweza kukaa na kufanya review ya mkataba ili kuuboresha kulingana na mahitaji na mnaandaa mabadiliko hayo ya mkataba (Adendum) je uone kuna haja ya kufanya hivyo sasa hasa mkataba wa vodacom na azam tv.
 
uko sahihi kabisa na ninaomba nikuhakikishie muda si mrefu tutaanzisha mashindano kama FA cup ya Uingereza.

Ligi yetu KUU ina teams nyingi sana za MAJESHI(JK Ruvu na Mgambo zikicheza team iliyo ktk hatari ya kushuka daraja likely ikanufaika na mazungumzo ya kiafande;Polisi Moro vs Polisi Dodoma)

Kwa nn isije sheria kwenye top league idara moja iruhusiwe kuwa na team moja tu?
 

Malafyale kanuni za FIFA za club licencing ziko wazi mmiliki mmoja haruhusiwi kuwa na timu zaidi ya moja kwenye ligi moja.Hata kwenye mkutano mkuu wa TFF President Tenga wakati huo alilizungumzia,inabidi tupate muafaka juu ya jambo hili kwa kuwa kitaifa lina unyeti wake tena mkubwa tu.
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli ulilolisema,majadiliano yanatakiwa yaanze mid way kwenye mkutaba.Tunajipanga kupitia vitengo na kamati zetu husika.
 
Bwana Malinzi hebu pitia tena mgawanyo wa mapato ya viwanjani. Haiwezekani gharama za uwanja zitofautiane. Kuna baadhi ya mechi gharama ya uwanja mfano taifa inakuwa 20m zingine 50m wakati maji hakuna vyoo vichafu viti vichafu. Kwani gharama halisi ya kukodisha uwanja wa taifa ni kiasi gani???
 

wazazi samahani nimechelewa kukujibu.
1.uwekezaji kwa vijana duniani kote huwa ni gamble/kubahatisha. mfano mzuri ni Samuel Etoo aliyekwenda Mallorca akiwa kinda wakamuuza Barcelona akacheza kidogo wakaona hafai Mallorca wakamchukua tena na kwa bahati at 17 akachezea timu ya Taifa na kung'ara......the rest is history Barcelona walikuja kumnunua tena kwa bei mbaya sana.Mfano mwingine ni Nii Lamptey wa Ghana aling'ara WC U17 lakini baada ya hapo akapotea kwenye ulimwengu wa soka.Tusiogope kubahatisha ,tuwekeze kwa vijana tukimpata Etoo mmoja katika vijana elfu moja ni kheri.Thomas Ulimwengu ni nyota mmoja aliyetokea katika kundi la maelfu wa vijana wa copa coca cola.
2.waganda ni mfano mzuri wa nchi zinazopeleka watoto wao wakajifunze mpira nje ya nchi,leo wanao zaidi ya 60.Risk yake ni kwamba Tanzania hatuna uraia wa nchi mbili,wakienda spain,dubai,qatar,ujerumani,belgium wakang'ara huko na kupewa passport ndo tutakuwa tumemwaga maji na mwana ,tutaishia kuwaona supersport wakiwa wamevalia jezi za ughaibuni.Hata leo vijana wa namna hiyo ughaibuni tunao wengi tu.
3.Nigeria wametutangulia kwa kuunda kikosi rasmi cha ushangiliaji na kupitia mdhamini wa kundi hilo (Glo) wanawezeshwa kusafiri duniani nzima kushangilia timu,hata brazil watakuwepo na ngoma zao.Tff kwa kushirikiana na wadau na sisi tutaunda kikosi chetu na pia tutatunga wimbo maalum wa kuhamasisha timu yetu kama ilivyo Anfield na "you will never walk alone"
4. Kamati tumeziunda tumemaliza,tulizingatia mambo mengi katika kuziunda,haikuwa kazi ndogo na ndio maana tulichelewa.
 
Last edited by a moderator:

Umegonga msumari mahali pake,kusema kweli zipo gharama za mchezo ambazo zinapaswa kuwa fixed na sio kutegemea mapato ya siku hiyo.
 
Ni kweli ulilolisema,majadiliano yanatakiwa yaanze mid way kwenye mkutaba.Tunajipanga kupitia vitengo na kamati zetu husika.

Ndugu Rais kuna hili suala la wachezaji wa kigeni kupungua kutoka watano hadi watatu, mimi binafsi siungi mkono hoja hii ukizingatia idadi hiyo ya watano si wengi kiukweli halafu pia timu zenye hao wachezaji ni Tatu tu AZAM SIMBA na YANGA na COASTER mmoja na ligi ina timu 14 zinazosajiri wachezaji 30 kila timu hivyo katika jumla ya wachezaji 420 wa kigeni ni 16 nadhani hapa kuna ukurupakaji waliofanya maamuzi hawakufanya utafiti na tathmini ya kisoka ata kisayansi please liangaliwe kwa makini nani hajui MBUYI TWITE anavyowapa changamoto washambuliaji wetu nani hajui HAMIS TAMBWE anavyowapa changamoto mabeki wetu na KIPRE hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…