Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014
Naomba ufafanuzi kuhusu kuhamisha ofisi za TFF na kujenga kitega uchumi pale Karume.
Ufafanuzi na uwazi ni muhimu ili wadau wa soka wajue kinachoendelea.
Tumeona jinsi ufisadi ulivyoingia kwenye maeneo kama hayo. Chukua mfano wa UVCCN na UWT. Hivi kweli jumuiya hizo zimenufaika?
TFF wasije kuwa wapangaji kwenye eneo lao wenyewe. Nani alitoa uamuzi huo? Kamati ya utendaji au mkutano mkuu.
Nahisi suala hili linahittaji baraka za mkutano mkuu kama ajenda muhimu
Nani mwekezaji? Yapi makubaliano na TFF? Gharama yake na vitu kama hivyo
Last edited by a moderator: