Maswali na ushauri kwa Malinzi


Naomba nijibu 'hoja' zako kwa mtiririko wako huohuo :
1. Kuna kanuni yoyote inayoipa nguvu TFF kuhakikisha kwamba vilabu vya madaraja yote vinatekeleza jukumu la kutengeneza vipaji vya vijana? Kwa mujibu wa kanuni hiyo, vilabu visipotekeleza vinachukuliwa hatua gani? Mbona nasikia Azam wana mipango mizuri kwenye hilo? Mbona basi hakuna tofauti baina ya vilabu vinavyochangia sana na vinavyochangia kidogo? Hii tarakimu ya 5% chanzo chake ni nini? Lakini kama wajibu ni wa vilabu vya madaraja yote, na kama uendelezaji vijana maana yake ni mikato ya 5% tu, vilabu vya madaraja mengine mtavitoza nini? Nani mwengine anachangia, kwa asilimia ngapi, ya mapato yepi? Kama jawabu ya swala la awali kabisa hapo juu ni ndio, kuna onyo au hatua yoyote imechukuliwa dhidi ya wahalifu wa kanuni hiyo? Kama jawabu ni sio, yaani hakuna kanuni inayolazimisha hivyo, kwa nini TFF ivihukumu vilabu kwa kanuni isiyokuwapo? Kama jawabu ni ‘ndiyo’ au ‘siyo’, ni dhahiri kwamba hakuna uhalali wa kuhamishia/kuhaulishia fedha za udhamini kwenda kwenye uendelezaji soka la vijana.
2. TFF ina takwimu zozote zinazoonesha ni asilimia ngapi ya wanaoitwa wadau wa mpira wanaodai kuwa maporomoko ya kiwango cha mpira wetu ni kwa kutowekeza kwenye vijana? Dhidi ya asilimia ngapi ambao hawafikirii hivyo? Lakini hata kama asilimia kubwa ya wadau ndio inafikiria hivyo, maana yake ndio fedha hiyo itoke kwenye mdau mmoja tu, ambaye ni vilabu? Hao wadau wenyewe wanaodai hivyo nao wamechangia asilimia ngapi, au hayo maoni yao tu yanatosha? Marefa asilimia ngapi? Makocha? Madaktari? Wizara? TFF yenyewe? Hakuna anayebisha haja ya kulea vipaji ndani ya vijana wetu. Lakini hakuna aliyesema kwamba njia pekee ya kugharimia ulezi huo ni kutoka kwenye mapato ya vilabu.
3. Kuna kanuni yoyote duniani inayoagiza kwamba hiyo seed capital ni lazima ianzie na vilabu? Kwa nini hao wadau wengine wasianze wao, vilabu vikafuata? Jawabu ya rahisi ni kwamba TFF inataka kukusanya, sio kutafuta, mapato. Labda tungejua hii 5% inayozozaniwa ni asilimia ngapi ya mfuko wote, wenye bajeti ya kiasi gani, itayopatikanaje? Vinginevyo inakuwa ni kama kumtaka bi arusi achangie sehemu ya mahari yake kwa ajili ya sherehe ya arusi yake, bila ya kujua sherehe hiyo inagharimu kiasi gani na hizo zilizobaki zitapatikana wapi!
4. Utanogeshaje mahaba kwa wali wa matangani? N’gombe wa maksai atalimaje kwa kusukuma badala ya kukokota jembe lenyewe? Ndiyo mnavyofanya kwa msingi wa hoja yako #4 hapo juu. Licha ya kuwa hatuwezi kusubiri zaidi, lakini huwezi kuanza na kukusanya vijana halafu ndio utafute fedha ya kuwagharamia. Ndiyo mantiki ya kibajeti ilivyo hivyo? TFF inapaswa kujipanga, kutafuta fedha kwa vyanzo tofauti na ndipo ianze kukusanya vijana. Kwani tuna ulazima gani wa kuandaa U19 kama uwezo hatuna? Au ndio tunahisi kwa kugombania kwenye makundi hatutafaulu? Ni bora kutolewa kwenye makundi ambako gharama zake ni ndogo, kuliko kugharamika mno kuwa wenyeji na hatimaye kutolewa nyumbani kwenye raundi ya kwanza.
Yote kwa yote, bado nahisi hoja zako zinazidi kuwa ni porojo, linalozidi kuanika udhaifu wa mwenendo mzima wa swala hili. Kwenye hili, ni TFF ndiyo inayoendelea na wakati wa maneno kwa sababu vitendo vingeanza na mipango kamili ya mradi mzima. Hichi kinachofanywa na TFF ni kukurupuka. Lakini ni bora ukurupuke kwa maneno, angalau ukikosea utaomba radhi papo hapo. Ukikurupuka kwa matendo na kuishia kuboronga, hakuna radhi itayoombeka. Unaweza kudhani kwamba TFF haitarudi nyuma, lakini kumbuka nadharia ya uwiano (theory of relativity) ya mwanasayanyi Albert Einstein. Kwa ufupi kasi (speed) na mwelekeo (direction) hutegemea sio tu mwendo wa chombo ambacho umepanda, lakini pia kasi na mwelekeo wako wewe abiria ndani ya chombo hicho. Nina wasiwasi TFF inarudi nyuma kiuwiano (relatively), ingawa chombo walichoabiri (FIFA) kinasonga mbele. Mkiendelea hivyo na Mungu akitupa uhai, iko siku nitakufafanulia kulingana na matokeo ya huko kutorudi nyuma kwenu.
 

hyo namba 3 kwanini isiwe kinyume vilabu vianze hlf wadau wafate
 
cc Jamal Malinzi
Ndg Rais
jana nilimsikiliza wakili / mwanasheria wa vilabu bwn Damas Ndumbaro kuwa wateja wake ambao ni vilabu wanakusudia kuanzisha mchakato wa kuitisha MKUTANO MKUU wa DHARULA...wa TFF..Kupinga MAKATO YA 5% ya mlangoni
Moja ya Hoja zao ni kupiga KURA ya KUTOKUA na IMANI na WEWE rais..
Nini Mtazamo wako juu ya Hatua hii ...
 
Last edited by a moderator:
hyo namba 3 kwanini isiwe kinyume vilabu vianze hlf wadau wafate
Hasa kwenye kandanda, huu si ulimwengu wa kuvumbua upya gurudumu. Tunapaswa kujifunza kwa waliotangulia. Ni wepi kati yao ambao huanza kuchangisha vilabu na baadaye ndio wakafuata wadau wengine? Hiyo ndiyo ilikuwa mantiki ya swala langu #3 .
 
[h=1]ANKO TENGA, TAFADHARI RUDI, KAKA MALINZI AMEFELI[/h]


Na Saleh Ally
USISHANGAZWE nami kuamua kujaribu kumshawishi aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga arejee tena ili kusaidia kuyatoa kwenye matope magurudumu ya shirikisho hilo.

TFF imekwama, rais wake Jamal Emily Malinzi, amefeli na hali inaonyesha wazi kuwa tuendako kuna hatari zaidi ya kutumbukia kabisa shimoni.
Kuna mengi ya kuonyesha kwamba Malinzi amefeli na kwa kuwa watu wanaona haya kuelezana ukweli, wanachukia kukosolewa, huenda kilichofanywa na TFF ya Tenga kwa mihula miwili, kitaporomoka na kupotea kabisa ndani ya nusu mhula wa Malinzi, nitafafanua.


Yamepita mengi kama ambayo tumeona, ile Taifa Stars maboresho iliyopotelea kusikojulikana na hakuna faida ya kusema ilikuwa imewekwa kwa malengo zaidi ya kuwasikia viongozi wakisema kuna wachezaji wa timu hiyo wamesajiliwa timu fulani tena asilimia 5 tu ya wachezaji hao, wengine hawajulikani walipo.


Matumizi mabaya na kuhama ofisi zao kwenye kupanga kwa mamilioni lukuki ni jambo jingine. Lakini kufeli kwa Taifa Stars ambayo iliwekewa ahadi kibao na sasa zinaanzishwa kamati tu eti za kutafuta walioihujumu ikionyesha wazi ni janja ya kutaka kuwaziba
Watanzania macho na masikio.


TFF ya Malinzi ni ile inayokwenda na mtindo wa ‘unfinished business'. Hakuna ilichokianza, ikikimaliza na kila ilichofanya kimefeli, huenda kipo, basi watanikumbusha.
Sijui kama kuna yule anayeweza kukataa kuwa TFF ya sasa imejaa ubabe, inayoangalia itapata vipi fedha bila ya kujali wengine wataathirika vipi.


Mfano mzuri ni sakata la TFF sasa kuagiza klabu zianze kukatwa udhamini wao wa Vodacom na Azam TV ili ziende kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Soka (FDF) eti ina mpango wa kusaidia vijana.
Ni maajabu saba kusikia eti kuna watu wanaona TFF iko sawasawa, inajenga hisia katika masuala yanayotakiwa kufanyiwa kazi kuusaidia mpira wetu, wako wanaofanya ushabiki kwa kuwa tu wanaweza kusaidiwa kurahisisha maisha yao!


Mpira huu ni kwa faida ya sisi tuliopo, wadogo na watoto wetu, pia vizazi vijavyo. TFF inafeli kwa kuwa inataka kuyapeleka mambo kiswahiba, kwa kubahatisha na viongozi kuangalia watapata nini, si mpira utapata kipi kwa ajili ya leo na baadaye.
Kichekesho cha kwanza ni kwamba TFF ndiyo inachukua fedha nyingi zaidi kwenye udhamini wa Azam TV na Vodacom kuliko hata klabu moja, hii ni kwa kila msimu. Lakini sasa inataka zaidi.
Kichekesho zaidi, klabu zinakatwa tayari fedha asilimia 6 katika mapato na zinakwenda kwenye mfuko huo.
Kukata mapato ni jasho lao, sawa hilo limekubalika, kukata hizo wanazopewa na wadhamini ndiyo juhudi na morali, ni sawa na kuwaua kisoka. Hofu yangu, TFF isije ikaagiza hata asilimia 5 za mishahara ya wachezaji na makocha nayo ianze kukatwa ili kusaidia soka.


Vodacom:
Udhamini wa Vodacom uko hivi, nitaufafanua kidogo; mkataba huo wa Vodacom uliosainiwa Septemba 11, 2012 ni wa miaka mitatu na kila msimu unatofautiana.
Msimu wa 2012-13, klabu zote 14 zilipewa Sh milioni 882 kwa ajili ya usafiri na zikigawanywa kila moja inapata Sh milioni 63. Msimu wa 2013-14, zinatolewa Sh milioni 952 (kila klabu Sh milioni 68) na msimu wa mwisho wa 2014-15 Vodacom wanatoa Sh bilioni 1.1 (kila timu Sh milioni 72).
Mgawo wa TFF kwa fedha kutoka Vodacom katika misimu hiyo mitatu uko hivi; 2012-13 (Sh milioni 160), 2013-14 (Sh milioni 172) na 2014-15 (Sh milioni 183).
Ukichukua fedha za TFF kwa kila msimu, toa za klabu moja, utagundua TFF inapata zaidi ya kila klabu kama ifuatavyo. Msimu wa 2012-13 (TFF inapata zaidi Sh milioni 97), 2013-14 (zaidi Sh milioni 104) na 2014-15 ambao ndiyo msimu huu (TFF inachota zaidi ya Sh milioni 111).
Kila msimu fedha ya Vodacom imepanda kwa kila klabu, lakini pengo la kuchukua nyingi zaidi kwa TFF nalo linazidi kuwa kubwa!


Azam TV:
Mkataba wa Azam TV, una pande tatu, kampuni hiyo ya runinga, TFF na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPL). Kampuni hiyo inatoa fedha sawa kwa pande hizo mbili.
Ni wa misimu mitatu ukianza 2013-14, TFF na TPL kila moja inapewa Sh milioni 140, 2014-15 (kila mmoja Sh milioni 154) na 2015-16 (kila moja Sh milioni 169). Kwa misimu yote mitatu, wote wawili, kila mmoja anapata Sh milioni 463.4.
Mgawo wa Azam TV kwa kila klabu kwa misimu mitatu uko hivi, msimu wa 2013-14 (Sh milioni 100), 2014-15 (Sh milioni 110) na 2015-16 (Sh milioni 121). Jumla kwa misimu yote mitatu, kila klabu italamba Sh milioni 331.
Msimu wa kwanza TFF inazizidi klabu kwa Sh milioni 40, wa pili Sh milioni 44 na wa tatu Sh milioni 48, maana yake pengo la wingi kati ya TFF pia linazidi kuongezeka kila wadhamini wanavyoongezeka kama ilivyo kwenye ule mkataba wa Vodacom!
Kama umeona yote hayo, basi nitakuachia maswali zaidi utafakari na kujiuliza, vipi TFF hairidhiki? Vipi inataka kufanya dhuluma mchana na vipi haitaki kujibu hoja na inafanya lazima?
Jiulize TFF na klabu, ipi inalipa mshahara watu wengi, ipi inasafiri zaidi na ipi ina gharama nyingi za uendeshaji, lakini usisahau shirikisho hilo kila mwaka linapewa dola 250,000 (zaidi ya Sh milioni 400) kwa ajili ya maendeleo ya soka kutoka kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Usisahau TFF inapata fedha za mfumo wa maendeleo ya soka kutoka kwenye makato ya viingilio vya klabu na haijawahi kusema hata mara moja kwa mwaka inaingiza kiasi gani na kinatumika vipi. Hakika inatakiwa kueleza hilo kwa kuwa fedha hizo ni za taasisi ya umma na si ya Malinzi au washauri wake!
Kutaka klabu ziwatangaze wadhamini, halafu fedha zitumike kuisaidia Taifa Stars, si sahihi. Hii inaonyesha mawili.
Moja, fedha inazopata TFF kutoka kwa wadhamini hazitumiki vizuri na wakati wa kuanika mahesabu hadharani umefika sasa.
Pili, unaweza kusema ukosefu wa ubunifu kwa kuwa TFF ina kitengo cha masoko ambacho kingefanya kazi ya kusaka wadhamini ambao watakubali kuzidhamini timu za vijana na watoto kama ambavyo uongozi wa Malinzi ulivyoingia madarakani na kuikuta Taifa Stars tayari inadhaminiwa na Kilimanjaro, uongozi wa Tenga ulifanya ubunifu ndiyo maana haukuingia kwenye mzozo na klabu kwa kutaka fedha zao za udhamini ambazo zilikuwepo tokea wakati ule, ndiyo maana nasema uongozi wa sasa wa Malinzi, umefeli. Nitarudi
 
Hasa kwenye kandanda, huu si ulimwengu wa kuvumbua upya gurudumu. Tunapaswa kujifunza kwa waliotangulia. Ni wepi kati yao ambao huanza kuchangisha vilabu na baadaye ndio wakafuata wadau wengine? Hiyo ndiyo ilikuwa mantiki ya swala langu #3 .

sidhani km Kuna ubaya wowote kwa vilabu kuchangia ikiwa lengo letu Ni moja km taifa kuundeleza mpira sasa hebu jiulize kwanini suala la kuendeleza mpira linaonekana la tff peke yake? Hili jukum la kuibua vipaji lilipaswa kufanywa na vilabu lkn jiulize vilabu vyetu vimefanya mini kwny suala kuibua vipaji ukiachana na azam? Wanalalamikahawana hela lkn hela za Kuweka kambi south Africa kwa ajili ya mechi ya mtani wanazo
 
Umeongea vizuri kwa kutumia neno 'kuchangia'. Kwa tafsiri sahihi ya neno hilo, kuchangia na ridhaa. Hili inalotaka TFF sio kuchangia, ni 'kulipia'. Sasa vilabu vilipie huduma gani iliyokwishatolewa na TFF kwenye kulea vijana? Kama ni hivyo, vilabu vya kuchangia ni hivyo vinavyosemekana kuwa vimesajili wachezaji 11 wa Taifa Stars ya maboresho. Lakini kwani timu yenyewe ilikuwa na hao 11 tu? Wengine wako wapi, hawachezi tena mpira? Haiwezi kuwa. Basi timu zilizo nao nazo hazichangii? Haiwezekani, kwa sababu zenyewe ndizo zenye wachezaji hao tangu awali, ndipo TFF zikawaona. Kama ni hivyo, ni nani aliyewalea baina ya TFF na timu hizo? Kama 'malipo' ni nani anayestahiki kulipwa na vilabu vyenye hao 11, TFF au timu zao za asili za mitaani ambako ndiko TFF iliwachukua? Kwa utaratibu huu, TFF itasemaje kuwa hakuna uleaji vipaji?
Kwa tafsiri ya TFF Na wanaowaunga mkono, dunia nzima hakuna timu inayolea vipaji. Watoto wa La Masia hawakuzaliwa na akina Pique ua Johan Cruyf. Barca iliwaona kutoka vilabu vya chini, wengine kutoka nje ya Hispania (mf. Messi). Etoo alichukuliwa na Academia ya Real Madrid, si mtoto wa De Stefano. Hivyo ndivyo vilabu vyetu, hasa Yanga na Simba vimekuwa vikifanya. Vimekuwa vikichukua baadhi ya wachezaji wadogo na kuwakuza, mpaka wengine hawakumbukwi timu za utotoni kwao. Kibadeni, Pondamali, kihwelu wengi na kadhalika. Mambo yamebadilika baada ya FAT/TFF kuibadilisha Ligi Kuu kinyemela kutoka kuwa ya ridhaa kuwa si ya ridhaa wala ya kulipwa. Utamlazimishaje mfadhili wa timu anayoipenda achangie (sio alipie) unavyotaka wewe? Hatuwezi kuwa na timu, wachezaji, waalimu, viongozi, akademia, waandishi, watazamaji na wadau wengine wa kandanda wa kiwango sawa na wa FA na Ligi zilizoendelea. Kwa sababu huko, Ligi, FA na vilabu, vyote vinaendeshwa kibiashara. Hapa kwetu hata hiyo Azam mnayoisifia haiendeshwi kibiashara (sina hakika kama angalau inaendeshwa kitaalamu). TFF ombaomba haiwezi kuiga malengo ya FA zinazoendeshwa kibiashara. Mambo taratibu. Hata Waziri Nkamia asingingilia, hata vilabu vingekatwa mapato hayo, lengo lisingefikiwa. Dunia ya leo, mambo yote ni uendelevu (Sustainability). Huo hauwezi kupatikana kiharambee-harambee. Unapatikana kwa mipango yakinifu ya FA yakinifu.
 
Ndugu Malinzi nilipotea kidogo humu leo narudia kwa maneno machache tu....ANGALIA SANA WASHAURI WAKO UNAPOTEA NA KWA KIPINDI UTAKACHOKUWA MADARAKANI KAMA HAUTABADILIKA UTAPOTEZA ATA ILE NURU HAFIFU YA NDGU TENGA ILIOKWISHA ANZA KUONEKANA.
 
nashangazwa na malinzi kutaka tff imiliki matimu yake,wakt tZ hatuna mashindano ya kutsha,anzisha mashndano mapya bwan
 

mkuu kabla ya kupost uwe unasoma ulichoandika vizuri maana hueleweki unakubali na kukanusha at the same post unasema suala la kuibua vipaji cyo la vilabu(labda utuambie Ni jukum la nan) hpo hpo unasema wakina pique wameibuliwa la masia hii inanipa wakat mgumu kuelewa unazubgumza nn hasa
 
Ni kwa sababu unasoma maelezo yangu kwa muktadha unaoutaka wewe, sio kwa ujumla wake. Nimesema jukumu la kulea vipaji si la vilabu (vinavyotaka kukatwa 5%). Kama unakumbuka, nimehoji kwamba si lazima vilabu viwe na sera ya kutumia vijana, ni kosa? Sasa kama vilabu haviwajibiki (moja kwa moja) kulea vipaji na bado vimelea kwa ushahidi niliokupa, ni sahihi kuvilaumu kwamba havilei? Ni haki kuwakata 5% ya udhamini lakini vilabu vya madaraja yote yaliyobakia havikatwi?
Kuhusu la Massia, ninaikosoa TFF na wanayoiunga mkono kwamba kulea vipaji si lazima iwe kwa kupitia FA. Kuchomoa wachezaji kutoka vilabu vidogo na kuviweka Mbeya miezi mitatu ndio kuibua au kulea? Iweje TFF idai imeibua vipaji na kuvilea kwa staili hiyo, huku ikivilaumu vilabu vilivyoinua na kukuza akina Silvatus Ibrahim, Anwar Awadh, Nonda Shaaban na wengineo, ziambiwe haziibui na kulea vipaji? Kwa tafsiri hiyo ya TFF, hata akina Messi na Etoo hawakuibuliwa na La Massia na Real Madrid Academy. Inshalla umenielewa.
 

Unajua, na wewe unajichanganya au hujui unachoongea, sasa ni wapi ulisikia chama cha mpira kiaanzisha kuwa na accademy, kuitaalisha kuwa ndio timu ya Taifa after 4 years?

Aliyekwambia vilabu haviibui wachezaji ni nani? hawa wanaoibuliwa na kuchukuliwa timu ndogo, ziyo kuibua???

Hii anayotuletea ni big investiment, sasa huyu mchezaji akitaka kununuliwa kwenda nje, je hayo mapesa nani atachukua? kumbuka vilabu vimechangia kukua kwake kisoka?

Naona niishie hapa kwanza, nitaendelea kesho, kwa kifupi, huu ni mradi kulipa hela za waliomuweka hapo, usidanganywe huyu ni bogus
 

Mkuu nakubaliana na wewe kua msela anafanya mchakato wa kulipa hela za walomweka hapo, mengine ni mbwembwe tu.
 

mkuu upo negative Sana na wala hu try so hard to criticize your brain kwa fikra zako unaamini vilabu vyetu vinaibua vipaji serious??? Kumnunua mchezaji akiwa na miaka 23 na kumchezesha kwa misimu 3 na kumtema ndyo kuibua vipaji? Kwa staili unayosema wewe ya kuibua vipaji tumefanya kwa miaka mingap? Na matokeo yake Ni yapi? Labda tusaidiane ktk Hili kuibua vipaji na kuviendeleza Ni kwa njia ipi labda? Ninavyoelewa Mimi system ambayo IPO active ya kuibua vipaji Ni kumchukua mchezaji akiwa mdogo WA miaka 12 na kumpatia acces zote za kuendeleza kipaji chake ikiwemo walimu wenye taaluma ya mpira,miundombinu ya mazoezi na vifaa vya kutosha,vile vile anatakiwa apewe elimu ya kujitambua na kuandaliwa kisaikolijia kuwa mchezaji WA kulipwa,hii ndyo system inayotumiwa na mataifa yote yalioebdelea kimpira ,ujeruman wamechukua kombe la dunia hyo ndyo system waliotumia ukienda Spain is the same ,Italia is the same Brazil is the same na kote huko kazi hii ya kuibua vipaji na kuviendeleza ilifanywa na vilabu sasa jiulize vilabu vyetu vinafanya ivo???? Usitake kuniambia mchezaji amecheza soka la mtaani miaka kibao Toto Africa wakamuona wakamsajili akacheza msimu mmoja yanga wakamuona wakamsajili unasema huko ndyo kuibua vipaji! Tff wanalazimika kufanya kazi ya kuibua vipaji kwa sababu wanaopaswa kufanya kazi ya kuibua vipaji Wako busy na siasa za mpira na sio kuuendeleza
 

mkuu naanza kupata wasiwasi na wewe km Una fikra pambanuzi na hii comment kiasi inanipa mwanga Ni mtu WA aina gani na dili nae,kwanza umeanza kwa kusema jukum la kulea vipaji si la vilabu! Labda nikuulize km vilabu cyo jukum Lao kulea vipaji Ni jukum la Nan??? Dunia nzima inajua kuwa jukum la kulea vipaji Ni la vilabu PIA ujue hatuzungumzii kulea peke yake tunazungumzia na kuibua!!unasema vilabu haviwajibiki na kulea vipaji!! Mkuu are u serious???? Labda nikuulize km wao hawawajabiki nani awajibike?? Tff au? Nashindwa kuelewa kabsa Ina maana sporting Lisbon walikuwa wehu kumchukua Ronaldo kwao maddeira na kumlea mpk alipifikisha miaka 20 na kununuliwa na man u ,...man u iliwalea akina scholes ,bechkam ,giggs, toka wakiwa na miaka 10 Ina maana walikuwa wanawajibika kwa jambo ambalo hawana wajibu nalo!! Unachoshindwa kuelewa vilabu ndyo mlezi mkuu WA vipaji kwny mchezo husika Hilo lipo wazi ,unawazungumzia etoo na messi km mfano hujui kwamba wamelelewa na vilabu vyao toka wakiwa na miaka 13 na 14
 
Wanasaikolojia wanaamini kwamba huwa tunawafikiria watu kwa jinsi tulivyo sisi. Angalie usije nawe ukawa ni takwimu ya nadharia hiyo. Jiulize kwa nini hoja yangu ianyokupa mashaka mpaka ukanifikiria hivyo imeshapata Likes mbili, huku hoja zako dhidi ya hoja hiyo zikiwa zimeshapingwa mara mbili. Ushauri kwa hili: tuondoe boriti machoni mwetu ndipo tuangalie vibanzi machoni kwa wenzetu. Ukimnyoshea mwenzako kidole kimoja, vitatu vilivyosalia unajielekezea mwenyewe.
Anyway, kwa mara ya mwisho nisaidie ufafanuzi. 1. Hoja yangu ya msingi ni kwamba si lazima (ingawa ni busara) kwa vilabu kulea vipaji. Inawezekana sana klabu kuamua kununua wachezaji waliokomaa tayari. Kwa hivyo kama FA ya nchi hiyo haina kanuni inayolazimisha vilabu kulea vipaji, si sahihi kuvilazimisha kama inavyofanya TFF hivi sasa. Na kama FA ina kanuni hiyo, basi hatua za kuchukua kwa asiyelea vipaji iwe kwa mujibu wa kanuni hiyo, siyo kuvikata vilabu vya daraja moja tu 5%. 2. Si kweli kwamba Vilabu havilei vipaji. Nimekutajia akina Kihwelu (Simba), Adolf (Yanga) na wengineo wengi kabla (kibaden-Simba) na baada ya hapo (Anwar Awadh - Yanga) wamelelewa na vilabu. Hivi sasa vilabu vinaonekana havilei vipaji kwa sababu TFF imekuja na utaratibu wa kujidanganya. Timu zote zinazoa wachezaji wa Kombe la Uhai linalolazimishwa na TFF kuwa ndio vikosi vya pili, kutoka timu za mitaani ili tu kukamilisha wajibu. TFF wanalijua hilo na wanaridhika nalo. Kama ilivyo kwenye viumbe, haja ya kuwa na academy hutokana zaidi na mazingira yanayozizunguka timu na ligi zao. Mazingira ya TFF na ligi yake hayahamasishi kuwa na academy. Yanga Kids ya Prof. victors haikuja kwa kulazimishwa na FAT ya wakati ule. Hata hao Sporting Lisbon hawakupiga ramli na kumwona Ronaldo tangu mchanga kuwa angewafaa. Walimkuta anaendelezwa tayari. Kulea vipaji is a relative phenomenon ambayo haijapata kufanywa na FA. Yenyewe inapaswa kuweka misingi tu.
nimalizie malumbano yangu nawe juu ya swala hili kwa kukuambia kwamba kila mtu ana haki ya maoni yake. Ila kwa hili la 5%, kama michango ya wengi inavyoonekana, wanaohisi TFF wamekosea ni wengi zaidi. Mwambie Malinzi kwamba vox populii, vox dei (sauti ya wengi ni sauti ya Mungu).
 

kwa akili hizi za kusubiti kila kitu kifanywe na tff tutasubiri sana
 

Hivi nani amekudanganya kuwa Italy, brazil na Spain wanachukua watoto wenye miaka 12 na kuwaweka academy ili waje wachezee timu ya Taifa? Unaweza kuleta document hapa ku support hii argument yako?

Wechezaji wanaovuma sasa hivi Spain, wengi wao ni uzao wa accademy ya Barcelona, hapo Nedherland, kwa miaka mingi academy ya Ajax, inasifika kwa kutaarisha wachezaji bora.

nirudi kwa hoja ya Malinzi, huwezi kuanzisha academy na kusema unawataarisha ndio timu ya taifa in four years, yaani Taifa liwekeze kwa watoto wa Mwanza tu? Hivi mnajua madhara yake kitaifa? hili ni swala sensitive kwa uasalama wa taifa hapo baadae, huwezi kuandaa jamii moja kwa nguvu ya watanzania wote, waje wale mkate peke yao, kaeni mfikirie. Kama ni hivyo, pitenmi, Tanzania nzima yafanyike mashindano ya watoto wa umri huo, kata kwa kata, Tarfa kwa Tarfa, baadae wilaya kwa wilaya, mpaka ngazi ya mkoa. Na baadae yafanyike mashindao ya kitaifa, na wachaguliwe watoto 40, ndo wakae kambini.

Vinginevyo, mtaliingiza taifa kwenye matatizo makubwa.

Jukumu l;a TFF, ilikuwa kusaidia kuandaa kozi za walimu wa soka, kwa mashule mbalimbali, na serikali kupitia wizara husika, kuandaa kila mwaka mashindano ya soka ya kikanda, na hata kupendekeza mfumo uliokuwepo wa kupata kombaini ya kamiseta, na kuchezaa na kombaini ya kamiseta ya Zambia.

Kingine TFF, ni kutafuta mfadhili wa kudhamini kombe la Taifa cup, au kombe ambalo litajumuisha timu zote toka zilizo chini kabisa, ili kutoa fursa kwa wachezaji wengine waweze kuonekana.

kupitia mashindano hayo, tutapata waxhezaji wazuri tu, kwani hapo zamani, hawa akina Aloo mwitu, Shabani Barsaza, Hamisi askari, walipatikana kupitia makombe hayo.

Nikija kuhusu ufanisi wa timu ya Taifa, si kweli kuwa kufanya vibaya ni kutokana na kutokuwa na wachezaji wazuri, hili kwanza ni tusi na dharau kwa wachezaji wetu. Kwa nini tusijiulize mbona Mbwana Samatta, na Ulimwengu wanapata namba kwenye moja ya timu bora kabisa katika Africa? Hawa si watanzania?

Tuliona Maximo, alifyotafuta wachezaji, na wala hakujali jina kubwa na ni vipi mpaka watu wakaipenda timu ya Taifa. Leo kocha anachojua ni kuwa wachezaji wapo Azam tu, sasa huyu ni kocha kweli?

Timu ya Taifa imekutana na Msumbiji ikiwa katika kiwango duni kabisa, wachezaji walikuwa hawana stamina. nakumbuka Ngassa, alitoka kufanya majaribio South africa akiwa ametokea timu ya Taifa, amekuja kufanya mazoezi Yanga, alishindwa kabisa, alikuwa hana pumzi kabisa. sasa kweli tulitegemea tushinde.

Nitaendelea kesho, mmfikishie salaam
 
FA unveil football academy - Telegraph
 
taarf ya habr jana,r1,walim watishia kugoma kufundisha kwa kukatwa elf 10 kila mwez,kwa ajil ya kujenga maabr ya shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…