mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
Kigogo, masikrodiga Kipaji Halisi Mjasiria Akili mwangalimungu Wa Kwilondo Masuke nguvu Mawenzi makoyo matale na wengine wote mliochangia hii mada,kwa niwashukuru kwa kuonyesha your concern kuhusu hii kanuni mpya ya mashindano:Naomba sasa niwafahamishe yafuatayo:
1.Kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji ni gharama kubwa sana na zoezi hili ideally lilitakiwa lifanywe na vilabu vya madaraja yote kuanzia vya ligi kuu hadi madaraja ya chini.Unfortunately hili linafanyika kwa kiwango cha chini sana.
2.Wadau wa mpira hasa kupitia media wamekuwa wakidai mpira unaporomoka kwa kuwa hatujawekeza katika mpira wa vijana.Uwekezaji huu ni mkubwa kuanzia hatua za kuibua,kulea na kuendeleza vijana.Majuzi tumefanya program ya maboresho ya timu ya Taifa,vijana kumi na moja toka program hii leo wanacheza ligi kuu,bila shaka ni tumaini kuu la Taifa stars ya kesho
3.Mfuko wa kuendeleza soka la vijana vyanzo vyake havitakuwa fedha za TFF peke yake,sisi tunachofanya ni kuandaa mbegu (seed capital) baada ya hapo umma wa watanzania utahamasishwa kuchangia mfuko huu ambao utakuwa huru katika kujiendesha (hautaendeshwa na sekretariet ya TFF).
4.Program za vijana zinaanza mwaka huu hivyo hatuna muda wa kusubiri,mwaka huu kitaifa tutakusanya watoto umri chini ya miaka 12 na kuwahamishia kwenye Academy.lengo letu ni kuwa na timu imara umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 ambapo Tanzania ita host fainali za Afrika umri chini ya miaka 17.Tunaamini program tuliyonayo itatufanya 2023 tucheze Afcon finals na tuingie fainali za world cup 2016.Hatuwezi kuongoza TFF bila malengo maalum.
Naomba suala la maendeleo ya mpira wa vijana tulitenge kabisa na siasa za mpira,mpira unahitaji fedha,mpira unahitaji sacrifice kwa wote wanaoutakia mema.
Baada ya kuyasema haya naamini tutashikamana pamoja katika kuinua mpira wetu.Muda wa kuongea kuhusu mpira wa vijana umekwisha sasa ni vitendo,katika hili TFF hatutarudi nyuma.
ahsanteni
Naomba nijibu 'hoja' zako kwa mtiririko wako huohuo :
1. Kuna kanuni yoyote inayoipa nguvu TFF kuhakikisha kwamba vilabu vya madaraja yote vinatekeleza jukumu la kutengeneza vipaji vya vijana? Kwa mujibu wa kanuni hiyo, vilabu visipotekeleza vinachukuliwa hatua gani? Mbona nasikia Azam wana mipango mizuri kwenye hilo? Mbona basi hakuna tofauti baina ya vilabu vinavyochangia sana na vinavyochangia kidogo? Hii tarakimu ya 5% chanzo chake ni nini? Lakini kama wajibu ni wa vilabu vya madaraja yote, na kama uendelezaji vijana maana yake ni mikato ya 5% tu, vilabu vya madaraja mengine mtavitoza nini? Nani mwengine anachangia, kwa asilimia ngapi, ya mapato yepi? Kama jawabu ya swala la awali kabisa hapo juu ni ndio, kuna onyo au hatua yoyote imechukuliwa dhidi ya wahalifu wa kanuni hiyo? Kama jawabu ni sio, yaani hakuna kanuni inayolazimisha hivyo, kwa nini TFF ivihukumu vilabu kwa kanuni isiyokuwapo? Kama jawabu ni ndiyo au siyo, ni dhahiri kwamba hakuna uhalali wa kuhamishia/kuhaulishia fedha za udhamini kwenda kwenye uendelezaji soka la vijana.
2. TFF ina takwimu zozote zinazoonesha ni asilimia ngapi ya wanaoitwa wadau wa mpira wanaodai kuwa maporomoko ya kiwango cha mpira wetu ni kwa kutowekeza kwenye vijana? Dhidi ya asilimia ngapi ambao hawafikirii hivyo? Lakini hata kama asilimia kubwa ya wadau ndio inafikiria hivyo, maana yake ndio fedha hiyo itoke kwenye mdau mmoja tu, ambaye ni vilabu? Hao wadau wenyewe wanaodai hivyo nao wamechangia asilimia ngapi, au hayo maoni yao tu yanatosha? Marefa asilimia ngapi? Makocha? Madaktari? Wizara? TFF yenyewe? Hakuna anayebisha haja ya kulea vipaji ndani ya vijana wetu. Lakini hakuna aliyesema kwamba njia pekee ya kugharimia ulezi huo ni kutoka kwenye mapato ya vilabu.
3. Kuna kanuni yoyote duniani inayoagiza kwamba hiyo seed capital ni lazima ianzie na vilabu? Kwa nini hao wadau wengine wasianze wao, vilabu vikafuata? Jawabu ya rahisi ni kwamba TFF inataka kukusanya, sio kutafuta, mapato. Labda tungejua hii 5% inayozozaniwa ni asilimia ngapi ya mfuko wote, wenye bajeti ya kiasi gani, itayopatikanaje? Vinginevyo inakuwa ni kama kumtaka bi arusi achangie sehemu ya mahari yake kwa ajili ya sherehe ya arusi yake, bila ya kujua sherehe hiyo inagharimu kiasi gani na hizo zilizobaki zitapatikana wapi!
4. Utanogeshaje mahaba kwa wali wa matangani? Ngombe wa maksai atalimaje kwa kusukuma badala ya kukokota jembe lenyewe? Ndiyo mnavyofanya kwa msingi wa hoja yako #4 hapo juu. Licha ya kuwa hatuwezi kusubiri zaidi, lakini huwezi kuanza na kukusanya vijana halafu ndio utafute fedha ya kuwagharamia. Ndiyo mantiki ya kibajeti ilivyo hivyo? TFF inapaswa kujipanga, kutafuta fedha kwa vyanzo tofauti na ndipo ianze kukusanya vijana. Kwani tuna ulazima gani wa kuandaa U19 kama uwezo hatuna? Au ndio tunahisi kwa kugombania kwenye makundi hatutafaulu? Ni bora kutolewa kwenye makundi ambako gharama zake ni ndogo, kuliko kugharamika mno kuwa wenyeji na hatimaye kutolewa nyumbani kwenye raundi ya kwanza.
Yote kwa yote, bado nahisi hoja zako zinazidi kuwa ni porojo, linalozidi kuanika udhaifu wa mwenendo mzima wa swala hili. Kwenye hili, ni TFF ndiyo inayoendelea na wakati wa maneno kwa sababu vitendo vingeanza na mipango kamili ya mradi mzima. Hichi kinachofanywa na TFF ni kukurupuka. Lakini ni bora ukurupuke kwa maneno, angalau ukikosea utaomba radhi papo hapo. Ukikurupuka kwa matendo na kuishia kuboronga, hakuna radhi itayoombeka. Unaweza kudhani kwamba TFF haitarudi nyuma, lakini kumbuka nadharia ya uwiano (theory of relativity) ya mwanasayanyi Albert Einstein. Kwa ufupi kasi (speed) na mwelekeo (direction) hutegemea sio tu mwendo wa chombo ambacho umepanda, lakini pia kasi na mwelekeo wako wewe abiria ndani ya chombo hicho. Nina wasiwasi TFF inarudi nyuma kiuwiano (relatively), ingawa chombo walichoabiri (FIFA) kinasonga mbele. Mkiendelea hivyo na Mungu akitupa uhai, iko siku nitakufafanulia kulingana na matokeo ya huko kutorudi nyuma kwenu.