Maswali na ushauri kwa Malinzi

hata kama hujui kusoma na picha huoni? saleh ally anamsifia tenga na kumponda malinzi, sasa ni kipi alichofanya tenga kwenye mpira wetu leo hii tunaweza kujivunia? tenga amekaa miaka nane tff iweje leo umsifie na kumlinganisha na mtu aliyekaa mwaka mmoja? kumbuka kipindi tenga anaingia madarakani watu wote tulikuwa tumechoka na madudu ya fat ndo maana wengi mnahisi tenga kafanikiwa, la muhimu malinzi apewe muda tu.
 

Jumamosi kwenye mkutano kati yangu na vilabu vya ligi kuu kocha wa timu ya Taifa Maart Nooij alitangaza program ya kitaifa ya kuboresha Taifa stars.Kuanzia mwezi Novemba kila mwezi atakuwa anaweka kambi ya siku mbili vijana umri chini ya miaka 23,lengo ni kuandaa timu itakayoshiriki CHAN june mwakani.Wengi wa vijana hawa wametoka program ya maboresho lakini pia wanatoka timu za madaraja ya chini kama Kahama FC.Scouting inaendelea kuboresha kikosi hiki.
Kudanganya umri ni kosa kubwa sana,majuzi Gambia walifungiwa na CAF miaka miwili,mwaka 2005 tulifungiwa na CAF juu ya Nurdin Bakari kudanganya umri.Sasa hivi bila kipimo cha MRI mchezaji haruhusiwi mashindano ya vijana.Anayedanganya umri ajue anajidanganya maana katika ngazi ya kimataifa atakamatwa tu,mashine hazidanganyi.
 

nguvu do not waste your breath on the likes of Saleh Ali,i know what is going on.Tenga alitujengea taasisi nzuri,kazi kaikamilisha,tunamshukuru,kazi iliyoko mbele yetu sasa ni kujenga mifumo thabiti ya mpira wa watoto na wa vijana grassroot na youth football.Kujenga misingi hii maana yake ni ku train coaches,referees,doctors and adminstrators.Pia tunajenga mfumo imara wa soccer academies tukianza kwa kuziongezea uwezo hizi zilizopo kwa kutrain makocha wao na kuwapa vifaa.Tunataka tuhakikishe kila mkoa mpira wa vijana unachezwa kwa kuwezesha mikoa na kuanzisha michuano ya vijana ya mikoa.It is expensive inabidi tutafute vyanzo madhubuti vya fedha za kuendeshea program hizi.Tujipange tutafanikiwa.
 
Last edited by a moderator:

Natumaini unaelewa vyema mfumo wa uendeshaji wa vilabu vyetu.Ukiondoa Azam bila shaka unajua nini kinaendelea kwingine kuhusu youth football.Kama unaelewa kwa undani nini kinaendelea bila shaka utaona kwa nini TFF tumeamua kusema sasa basi something must happen.Tunaanza na program ya kitaifa umri chini ya miaka 23 kujiandaa na CHAN qualifiers,tunaanza na program ya kitaifa umri chini ya miaka 14 kujiandaa na Africa U17 qualifiers 2016,tunaanza na program ya kitaifa umri chini ya miaka 13. Kujiandaa na Fainali za Afrika U17 mwaka 2017,wale U17 waliotolewa mashindanoni mwaka huu tumewatafutia tayari ligi za madaraja ya chini wakomae,muda wa kuzungumza tuzungumze lakini na vitendo viwepo.
 
Last edited by a moderator:
Saleh hajalinganisha watu hawa katika hoja yake kataja mapungufu ya Malinzi hivyo kimantiki ulitakiwa upinge au utoe utetezi kuonyesha kuwa hoja ya\ Saleh ni dhaifu. Lakini kusematu huyo ni team Nyamlani hakumfanyi Malinzi awemsafi. Two wrongs canot make it right
 

Asnte kwa majibu yako ingawa umekwepa kueleza kwanini timu ya vijana kujaa sura za Dar es Salaam.

Mimi naomba nishauri kuwa mpira haswa kwa vijana haukui kwani umewekewa msisitizo Dar peke yake, na hata hizo sports center zinajengwa Dar tu Je kwanini msipeleke maeneo ya nyanda za juu na ambazo zina hali ya hewa nzuri na mazingira mazuri kama Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza, Manyara nk kwani naona Dar siasa ni nyinyi kuliko maendeleo halisi ya mpira tunyo yataka.
Mwisho naomba muanzishe utaratibu wa lazima kwa vilabu vikubwa na mikoa ambayo kuna timu za ligi kuu au hata daraja la kwanza kujenga vituo vya mpira ili vijana waweze kukaa katika hivyo vituo wasome na kujifunza mpira
 
UFISADI TFF wa shilingi bilioni 1.4
chanzo mwananchi la leo..uk 40
cc@Jamal Malinzi

Very soon hatutakuwa na wadhamin..... bilion 17 za udhamini wa bia ndo zinafikia mwisho..... ngoja tuone kinachoendelea kwenye hii movie ya Malinzi na tieftief yake.
 
nimekuelewa saleh,
 
Very soon hatutakuwa na wadhamin..... bilion 17 za udhamini wa bia ndo zinafikia mwisho..... ngoja tuone kinachoendelea kwenye hii movie ya Malinzi na tieftief yake.

You think so Blueband?
 
Last edited by a moderator:
Kitendo cha kumfungia Ndumbaro kimeonesha jinsi gani uongizi wako ulivuo ba mapungufu, kiutendaji na kifikra, inaonekana uongozi webu hauhitaji challenges (changamoto) na hii ipo kuanzia kuanzia ngazi ya vilabu hadi TFF kwenyewe... Tunaona watu wanafungiwa kwa sababu tu ya kukosoa au kupingana na baadhi ya masuala na uongozi, which is not fair... Everywhere kuna challenges utafungia wangapi? Fanyia kazi changamoto jibu hoja za ndumbaro kwa hoja bora kabisa uone kama kuna atakae kua against... Ubabe wa kutumia Rungu la madaraka kumdhibiti wanao question utendaji si uadirifu... Jamal tulikutegemea, na naamin ukirekebisha tutaendelea kukutegemea kwenye maendeleo ya mpira hapa kwetu... #Advise
 

punguzeni mahaba jamani, kipindi cha tenga kuna watu hadi walifungiwa maisha au umesahau? bila jk kuingilia kati kuna watu tungewasahau kabisa kwenye mpira wetu
 
Last edited by a moderator:
punguzeni mahaba jamani, kipindi cha tenga kuna watu hadi walifungiwa maisha au umesahau? bila jk kuingilia kati kuna watu tungewasahau kabisa kwenye mpira wetu
Sifa kubwa ya Tenga ni kwamba ametuachia mfumo mzuri (structures) za uendeshaji wa mpira wetu.Tuheshimu mfumo tuliojiwekea,penye malalamiko tufuate taratibu kuelezea ambalo hatujaridhika nalo,good governance.
 
Mimi na kamati yetu ya utendaji hakuna mwoga wa changamoto,i cherish a good healthy debate,lakini utaratibu ufuatwe.
 
Sifa kubwa ya Tenga ni kwamba ametuachia mfumo mzuri (structures) za uendeshaji wa mpira wetu.Tuheshimu mfumo tuliojiwekea,penye malalamiko tufuate taratibu kuelezea ambalo hatujaridhika nalo,good governance.

Wajua shida ya viongozi wengi hivi sasa ni mwataka kutawala na si kuongoza.

Kiongozi mzuri ni mwenye kuketi na waongozwa wake ambao ndo kwa haki viongozi wake wampe namna ya vile watakavyo wao walio mchagua naye afanze mashauriano nao.

Sasa hizo taratibu uzisemazo kimaandishi ni kweli hivyo ndo ipasavyo, walaakin sie tulopembeni yenyu twakuoneni maneno yenyu tofauti kabisa kabisa tena kabisa na matendo yenyu.


Haya we are waiting good governance by actions not by writing and reading in the office and media.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa nakufuatiza yako majawaba.
 
Mimi na kamati yetu ya utendaji hakuna mwoga wa changamoto,i cherish a good healthy debate,lakini utaratibu ufuatwe.
Seriously? Wewe na kamati yako mnafuata utaratib? Mnamfungia mtu 7years kwa ku advocate wateja wake?? No wonder hakukua hata na nafasi ya natural justice... B'se mtuhumiwa yuko Usa... Tena kama ni maamuzi ya kamati i sniff rat on our football fate... Collective measures?? Sio decision ya mtu mmoja? Basi hatuna viongozi trust me....
Nakupa mfano... Hans Pope alitoa msimamo wa Wamiliki wa malori ya mafuta kugoma kodi za WAZIRI tena mkorofi... Serikali/Wizara haikumfungia Pope unajua kwa nn? He is just a representative (chairman) wa Wamiliki wa malori ya mafuta...
Lean between the line brother mpira na maendeleo yake ni manufaa ya Taifa/África... Ndio maana hua tunaishangilia Cameron, Nigeria.
Nafasi bado ipo rekebisha io... Kutereza si kuanguka..
 
Mh. Malinzi juzi wewe na uongozi wako mmetimiza mwaka mmoja tangu mliposhinda uchaguzi mkuu TFF,
BIRTHDAY itakuwa wapi tukate keki??
 

Simbajr kwa mfumo wa kimahakama tuliojiwekea si vyema adminstrators tukazungumzia maamuzi ya judicial commitees,nikuhakikishie haki ilitendeka.
 
Last edited by a moderator:
Hehehehehe... I trust u bro!!
All the best.... Kama unaona la kukufaa naamini utachukua... Kama hamna achana nalo... My bad.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…