Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Mheshimiwa Rais kuna maswali nimekuuliza hapo juu...Tangu jana usiku....Kama haitojali naomba unijibu mkuu....Umegonga msumari mahali pake,kusema kweli zipo gharama za mchezo ambazo zinapaswa kuwa fixed na sio kutegemea mapato ya siku hiyo.
Ndugu Rais kuna hili suala la wachezaji wa kigeni kupungua kutoka watano hadi watatu, mimi binafsi siungi mkono hoja hii ukizingatia idadi hiyo ya watano si wengi kiukweli halafu pia timu zenye hao wachezaji ni Tatu tu AZAM SIMBA na YANGA na COASTER mmoja na ligi ina timu 14 zinazosajiri wachezaji 30 kila timu hivyo katika jumla ya wachezaji 420 wa kigeni ni 16 nadhani hapa kuna ukurupakaji waliofanya maamuzi hawakufanya utafiti na tathmini ya kisoka ata kisayansi please liangaliwe kwa makini nani hajui MBUYI TWITE anavyowapa changamoto washambuliaji wetu nani hajui HAMIS TAMBWE anavyowapa changamoto mabeki wetu na KIPRE hivyo hivyo.
hoja yako MKALIKENYA ni ya msingi club vs country ni mgongano wa dunia nzima,hata uingereza wanalia na hili jambo.Upande mmoja unasema Kipre tcheche na hamis tambwe wanawazibia nafasi john bocco na jerry tegete,upande wa pili unasema bila twite,kiiza na owino ligi hainogi,kama Federation lazima utafute balance,swali ni je huo uwiano ni wachezaji wangapi wa nje? Mmoja,wawili,watano au kumi?na kigezo ni kipi? Wadau tusaidiane katika hili maana TFF ni waratibu na wasimamizi tu, ligi ni ya watanzania wote.
Jamal...
Kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya Mkataba wa Azam TV ambao ni dhahiri haukuuingia wewe na safu yako.....Kwa maono yako unaonaje juu ya malalamiko haya ya vilabu hususan Klabu ya Yanga?....Je kuzipa Kalbu Tshs. 100,000,000/= kwa msimu kunazisaidia Timu?....
Ni kwa nini Timu zisipewe fursa ya kushiriki katika majadiliano ya Mikataba baina ya TFF na Wadhamini (hasa ule wa VodaCom)....
Pia mna mpango gani na Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen ambaye tayari ameonekana hana msaada wowote kwa Timu hiyo?
Na mwisho, mbona makato ya mapato kwa mechi za Ligi Kuu yamekuwa ni mengi na hayavisaidii vilabu?
Nadhani wachezaji wa5 wa kigeni wanatosha ila sheria iwe wa3 katika mechi 1. Ila kwa kimataifa wawatumie wote tu.
Hapo nitapishana na wewe,what is the point klabu iingie gharama kumsajili mchezaji kwa mamilioni halafu iambiwe akae benchi?
Asante kwa majibu mazuri....Jitahidi utekeleze hiyo dhamira yako ya Uwazi katika Mikataba , ukifanya hivyo utakuwa Mkombozi wa kweli wa Soka la Tanzania. Pia suala la makato kwa Vilabu ni la kulizingatia sana....Haiwezekani Timu zinaintiza milioni 160 halafu zenyewe zinapata milioni 40 kila moja na nusu ya Mapato hayo inakatwa na kugawanywa kwa watu ambao kwangu mimi naona hawastahili.....Mfano ni DRFA....Balantanda:
1. Ni kweli makato ya milangoni formula yake nakiri ina utata,tutaifanyia kazi,vilabu kupata chini ya 50% ya mapato si haki.Wao ndio wavuja jasho.
2.Mkataba wa AzamTv pamoja na mikataba mingine ni vyema siku za usoni vilabu vikashiriki tena kwa uwazi.TFF haina chanzo kikubwa cha mapato zaidi ya ligi lakini huwezi kuamini loyalty /mrahaba ambayo TFF inalipwa tokana na mapato ya milangoni ni zero/sifuri % percent,unaweza kuamini?Mambo haya inabidi yaongeleke kwa uwazi.
2.
Balantanda naomba unitumie email jamalmalinzi@yahoo.com au nipigie au ni sms 0754815543Asante kwa majibu mazuri....Jitahidi utekeleze hiyo dhamira yako ya Uwazi katika Mikataba , ukifanya hivyo utakuwa Mkombozi wa kweli wa Soka la Tanzania. Pia suala la makato kwa Vilabu ni la kulizingatia sana....Haiwezekani Timu zinaintiza milioni 160 halafu zenyewe zinapata milioni 40 kila moja na nusu ya Mapato hayo inakatwa na kugawanywa kwa watu ambao kwangu mimi naona hawastahili.....Mfano ni DRFA....
Pia TFF ibuni vyanzo vingine vya mapato badala ya kutegemea mapato ya mechi ama Misaada ya FIFA....TFF wawe na wadhamini wao ambao watasaidia kuongeza Kipato...Jaribuni Kujenga viwanja vyenu wenyewe na kufungua miradi/vitega uchumi mfano Hostel ama TFF House ambayo itakuwa na vyumba vitakavyokodishwa kwa wafanyabiashara...Pia Jezi za Timu ya Taifa zianze kuzalishwa na TFF na kuuzwa kwa wapenzi wa Soka hivyo kuiingizia mapato TFF....
Kingine jitahidini muifanye Ligi yetu iwe na sura ya Kulipwa zaidi badala ya Ridhaa....Tukiwa na Ligi ya Kulipwa itakuwa ni hatua nzuri kuelekea mafanikio ya Soka letu...Tuwe na Ligi ya aina ya PSL ya RSA....Klabu zihimizwe kuingia katika mfumo wa Kampuni badala ya kumilikiwa na wanachama kama ilivyo sasa. Pia mliangalie vizuri suala la kupunguza Idadi ya wachezaji wa Kimataifa kutoka watano mpaka watatu, binafsi sioni sababu ya kuwapunguza kwani uwepo wao unaleta changamoto kwa wachezaji wazawa na wao kupata hamasa ya kutafuta timu nje ya nchi tofauti na sasa ambapo wachezaji wengi wazawa kwao kuchezea Simba ama Yanga ndio malengo yao....
Si vibaya kwenye Kamati zako ukawa unawakumbuka baadhi ya Members wa JF ambao nina uhakika watakua msaada mkubwa sana kwako licha ya kwamba wengi wao wanatumia majina ya vificho, cha msingi ni kuwasiliana na Invisible au Maxence Melo wataona namna ya kukusaidia.
Lengo la azimio la bagamoyo lilikuwa kuongea wachezaji wazawa kupata kucheza zaidi. Sasa wakipunguzwa wakatakiwa kucheza wa3 kwa kila mechi basi nao watakupunguza kusajili pia n mwisho wa siku wazawa watapata nafasi
huyu muhaya huyu anapenda sana show off
Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014
Jamal MalinziHapo nitapishana na wewe,what is the point klabu iingie gharama kumsajili mchezaji kwa mamilioni halafu iambiwe akae benchi?
Kwani hizo nafasi za wazawa ziko Simba, Azam na Yanga tu? Mi nadhani tujiulize maswali mawili:
1. Ni kwa nini hatutoi nje wachezaji wetu wengi mpaka tuzing'ang'anie Simba na Yanga?
Ni mtazamo wangu mh. Jamal Malinzi
Jamal Malinziuko sahihi kabisa na ninaomba nikuhakikishie muda si mrefu tutaanzisha mashindano kama FA cup ya Uingereza.
Jamal MalinziMokoyo kwa vyovyote vile tutaongeza timu za premier league na kuanzisha mashindano mapya ili vijana wetu wapate angalao mechi 40 za kucheza kwa mwaka.Mabadiliko haya yatakuja msimu ujao.