Asante kwa majibu mazuri....Jitahidi utekeleze hiyo dhamira yako ya Uwazi katika Mikataba , ukifanya hivyo utakuwa Mkombozi wa kweli wa Soka la Tanzania. Pia suala la makato kwa Vilabu ni la kulizingatia sana....Haiwezekani Timu zinaintiza milioni 160 halafu zenyewe zinapata milioni 40 kila moja na nusu ya Mapato hayo inakatwa na kugawanywa kwa watu ambao kwangu mimi naona hawastahili.....Mfano ni DRFA....
Pia TFF ibuni vyanzo vingine vya mapato badala ya kutegemea mapato ya mechi ama Misaada ya FIFA....TFF wawe na wadhamini wao ambao watasaidia kuongeza Kipato...Jaribuni Kujenga viwanja vyenu wenyewe na kufungua miradi/vitega uchumi mfano Hostel ama TFF House ambayo itakuwa na vyumba vitakavyokodishwa kwa wafanyabiashara...Pia Jezi za Timu ya Taifa zianze kuzalishwa na TFF na kuuzwa kwa wapenzi wa Soka hivyo kuiingizia mapato TFF....
Kingine jitahidini muifanye Ligi yetu iwe na sura ya Kulipwa zaidi badala ya Ridhaa....Tukiwa na Ligi ya Kulipwa itakuwa ni hatua nzuri kuelekea mafanikio ya Soka letu...Tuwe na Ligi ya aina ya PSL ya RSA....Klabu zihimizwe kuingia katika mfumo wa Kampuni badala ya kumilikiwa na wanachama kama ilivyo sasa. Pia mliangalie vizuri suala la kupunguza Idadi ya wachezaji wa Kimataifa kutoka watano mpaka watatu, binafsi sioni sababu ya kuwapunguza kwani uwepo wao unaleta changamoto kwa wachezaji wazawa na wao kupata hamasa ya kutafuta timu nje ya nchi tofauti na sasa ambapo wachezaji wengi wazawa kwao kuchezea Simba ama Yanga ndio malengo yao....
Si vibaya kwenye Kamati zako ukawa unawakumbuka baadhi ya Members wa JF ambao nina uhakika watakua msaada mkubwa sana kwako licha ya kwamba wengi wao wanatumia majina ya vificho, cha msingi ni kuwasiliana na
Invisible au
Maxence Melo wataona namna ya kukusaidia.