Maswali na ushauri kwa Malinzi

kama mm malinzi ningetangaza timu hiyo makocha wazawa na wandishi wa habari simamieni timu tff tulipa gharama za timu mkishindwa muirudishe tff
 
tff mnaongozwa na kaburu alikuwa akitangaza kwenye mabar kuwa wachezaji wa kigeni mwisho saba na leo mmetangaza saba naamini hata kufungwafungwa kwa star mnamsililiza kaburu
 
Hivi Jamali MALINZI, hudhani kwamba kama unashindwa kufikia mafanikio ya mtangulizi wako (achilia mbali kuyazidi) ni uzembe, na kwamba kujiuzulu nako ni sehemu ya uwajibikaji? Embu jipime na uone kama unatosha kuongoza TFF.
 
Last edited by a moderator:
kufanya vibaya kwa timu yetu ya taifa mimi naona chanzo ni uwongozi mbovu wa Jamali Malinzi,kwasababu ukirudisha nyuma kumbukumbu nyuma kipindi cha Tenga ilikuwa na kauwene tulikuwa tunaotea kidogo,yote ilitokana na mikakati aliyokuwa akiiweka bwana Tenga kuendeleza soka la letu lkn kwa Malinzi ni tabu tupu hakuna mipando ya kuendeleza soka letu
 
Jamal Malinzi angeamua tu kutuachia timu yetu. Hapa shida ni uongozi na si kocha. Hata hao akina Boniface na Moroco watapata shida tu. Hapa wanapewa timu ili TFF waje kusema si mmeona wazawa wameshindwa!

Timu kushindwa namna hiyo inatakiwa viongozi wawajibike tu hakuna kingine. Nilipata uchungu sana kusikia eti tumefungwa na Swaziland yenye watu 1.4 million tu huku tukiwa na watu zaidi ya 45 million!

Malinzi tutendee haki
 
Wakuu, kwanza kabisa nikiri kuwa sijasikiliza kile alichokisema Malinzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari. Lakini pamoja na hilo, ziko hoja kadhaa ambazo zinanifanya niamini kuwa Malinzi hana tena sifa za kuongoza TFF.

1. BILA ACADEMY HATUFIKI POPOTE
Kwa mpenzi yeyote wa soka hii si hoja ngeni kwa nchi yetu. Jambo hili limeongelewa sana hata kabla Tenga hajaanza kuiongoza TFF.

Wakati ni kweli kwamba academies ni msingi mzuri na wa uhakika kwenye soka, si kweli kwamba bila hizo hatuwezi kupata matokeo mazuri. TFF si shirikisho jipya, kipya ni jina tu. Na kama mtakumbuka wakati maalim Muhidin Ndolanga anang'olewa kwa mbinde TFF (enzi hizo FAT), timu yetu ya taifa ilikuwa katika kipindi kibovu sana. Alipoingia Tenga alianza na mtazamo wa kuinua soka la vijana na ndipo hapa tukapata Serengeti boys iliyofuzu michuano ya vijana Africa lakini ikapokonywa ushindi.

Tofauti na kina Malinzi, rais Tenga alitumia mfumo sahihi wa kukuza soka la vijana kwa kuzijengea uwezo klabu la ligi kuu. TFF ilibaki kuwa msimamizi mkuu wa soka la Tanzania ikiwemo kupanga sera. Ni wakati huu ndipo tulipoona hata soka la wanawake likiinuka kwa kasi sana.

Jamal Malinzi na vigogo wenzake wanatumia mfumo opposite na huo ulioanzishwa na akina Tenga. Leo hii vilabu ndio vinatoa pesa kwa TFF kuchangia maendeleo ya soka la vijana ambayo kimsingi hulelewa na vilabu. Swali ninalo jiuliza: TFF ina mpango wa kuanzisha timu zake binafsi? Ama kuna mpango wa kuanzisha Akademi za TFF? Kwani jukumu la TFF hasa ni nini?

Je, Rwanda waliotufunga wana Akademi ngapi? Vipi Uganda, Kenya, Burundi, DRC? Zambia ziko Akademi ngapi? Sipingi hoja ya kuwa na Academy la hasha, ila tu katika taasisi yoyote huwa kuna malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Kina Tenga walifaulu kwa kiasi kikubwa sana kwenye malengo ya muda mfupi. Kwa TFF hii mambo ni shagala bagala, hakuna kinachoeleweka. Mapesa yanamiminika TFF halafu wimbo ni ule ule, bila Academy hatufiki popote. Hivi huyu Malinzi amewekwa TFF ili akatafiti sababu ya taifa stars kufanya vibaya, au alete suluhisho la matokeo mabovu?

2. WACHEZAJI HAWAFUNDISHIKI
Kuna mahali nilisoma kuwa Cameroon ni mojawapo ya nchi zenye academies bora kabisa barani mwetu. Nakumbuka nyakati za Malcio Maximo na taifa stars yetu isiyo na Academy. Jinsi tulivyiwanyesha wahitimu wa Academy ambapo almanusuru tufuzu kwa michuano afrika. Ni wakati huu tulipothubutu kuwatunishia msuli miamba wa soka Brazil, huku timu moja ya Academy toka ulaya iliyofuzu world cup tukiinyoa kwa mabao manne.

Nabaki kujiuliza, kutofundishika kwa wachezaji wetu kumeanza lini? Kwa akili ya Malinzi waganda wanafundishika lakini si watanzania. Je, hatukuwa na akina Dani na Simon Sserunkuma hapa Tz? Je, walifua dafu kwa hawa maimuna wetu? Tatizo letu ni nini hasa?

Kwa mtazamo huu wa Malinzi nitashangaa sana kama mchezaji yeyote wa ligi kuu ataitwa timu ya taifa akaitikia wito. Hii ni dharau kubwa sana kwa vijana ambao wanacheza soka la kitabuni wawapo kwenye vilabu vyao.

3. HAMASA YA SOKA KWA TAIFA
Bila kupepesa macho tunarudi zama za giza. Wakati Tenga anaingia madarakani watanzania tulishajitenga na timu ya taifa. Ilibidi ifanyike kampeni kubwa kujaribu kurejesha hamasa ya watanzania kuipenda timu yao. Hili lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini leo tunarudi tulikotoka kwa kasi kubwa ajabu. Watu wamesusa timu ya taifa. Mpira umebaki ngazi ya vilabu ingawa wachezaji inasemekana hawafundishiki.

MTAZAMO WANGU
Kwa kuzingatia haya,sasa ninaamini kuwa Malinzi aliingia TFF pasipo kuwa na maono yoyote. Ameingia akiwa haelewi msingi wa timu kufanya vibaya. Ameingia kwa sababu tofauti na kukuza soka letu.

Namshauri bwana Jamal Malinzi aachie ngazi kwa amani kuliko kuzidi kulididimiza soka letu. Sasa inatosha, tunahitaji viongozi wenye maono sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Amepoteza sifa???

Ni lini alishawahi kuwa na sifa mpaka azipoteze???
 
Amepoteza sifa???

Ni lini alishawahi kuwa na sifa mpaka azipoteze???

Mkuu, maadam watu walimchaguay, alidhaniwa kuwa ana sifa. Mimi binafsi niliwahi kumwandikia kwenye thread moja humu kabla ya uchaguzi kuwa hafai kuongoza TFF akanishutumu kwa personal attack.
 
Mpira wa Tanzania Umejaa SIASA nyingi,hatutaki kuwekeza ktk soka,ona AZAM wanachokifanya sasa na kupitia kwao ilitakiwa tupate funzo,lakini wapi mchawi aliyeturoga kafa na tunguri zake
 
Mpira wa Tanzania Umejaa SIASA nyingi,hatutaki kuwekeza ktk soka,ona AZAM wanachokifanya sasa na kupitia kwao ilitakiwa tupate funzo,lakini wapi mchawi aliyeturoga kafa na tunguri zake

Ni wapi katika Tanzania hii ambako siasa haitamalaki? Kuanzia kwa machinga mpaka kanisani. Ndio maana nikasema tunahitaji kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kufufua soka letu. Tenga alianza vizuri, lakini kama ilivyo desturi yetu kaja Malinzi na kufuta kila alichokifanya Tenga na kuleta mfumo wake. Kwa mwendo huu kila siku tutakuwa tunajenga msingi na kubomoa.
 

Hahahahaha
Jamaa alihama hadi ofisi na kwenda kukodi,bila FIFA kung'aka asingerudi.Lakini ndio ilivyo kwa Tanzania,bado ipo safari na kazi ya kufanya
 
Hivi Jamali MALINZI, hudhani kwamba kama unashindwa kufikia mafanikio ya mtangulizi wako (achilia mbali kuyazidi) ni uzembe, na kwamba kujiuzulu nako ni sehemu ya uwajibikaji? Embu jipime na uone kama unatosha kuongoza TFF.

wabongo mnakuwaga vigeu geu sana kpindi cha tenga wakati anambeba maximo mlimponda sana Leo amegeuka kuwa malaika
 
Last edited by a moderator:

mnakosea mnapomlaum malinzi peke yake khs suala la maendeleo ya time yetu ya taifa hebu jiulize vilabu vyetu pendwa vimefanya nini kusaidia mpira wetu?kumbuka vilabu pia vina nafasi kubwa kufanya time ya taifa iwe bora rejea ishu ya Spain na kuwa ba wachezaji wengi kutoka LA masia.....sasa jiulize LA masia ye2 iko wapi? ikiwa timu zetu hta viwanja vya mazoezi hawana?
 
Mkuu unafahamu wajibu wa TFF katika soka la Tanzania? Na pia kama unafahamu kwamba Malinzi ndiye kiongozi wa TFF basi utafahamu kwa nini Malinzi alaumiwe.
 
J malinzi usituhadae wadau wa michezo kwa wale wanaotoa rushwa ile sheria feki ya kadi tatu za njano hapo kulikua na rushwa asilimia 100 halafu tff mkajifanya mnaifuta hiyo sheria bila maelezo ya kina inadhihirisha sheria ilikuwa mifukoni.
leo unamtafuta mtoa rushwa usitake kutufanye wadau wajinga swala la rushwa umeshindwa au unamtafuta mnyonge ndio umkamate?
 
Jamal Malinzi mambo ya January Makamba Uwanja wa Taifa jana aibu sana~!
Mnalazimisha kuingiza siasa kwenye soka la Tanzania!Mlianza wkt wa mashindano ya COSAFA sasa mnakuja tena na madudu ya jana!

Soka kuongoza limekushinda,2020 kagombee udiwani kwenu Bilele
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…