Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Haya habari ndiyo hiyo Blatter kakubali kutoisumbua mahakama, kina Jamal Malinzi mna mipango gani? Treni la FBI ndio hilo linakuja south of Meditteranean sea
 
Mwenye picha za jezi mpya za taifa starz naomba aweke nizione
 
Ni lini Jamal Malinzi ataacha kufanya maamuzi ya kukurupuka na yasiyo na tija kwa Taifa Stars? Lini ataacha kutafuta suluhisho rahisi(mfano kubadili jezi za timu) kwa matokeo mabaya ya T. Stars ?
 
Mwenye picha za jezi mpya za taifa starz naomba aweke nizione

Zipo online now ni kichefuchefu kabisa kwa ubunifu wa hovyo!

Then TFF wamesema kwa umaridadi wa jezi hizi mpya wana uhakika sasa Taifa Stars itaanza kushinda games zake

Ehehehehe TFF kweli watz tunayo
 
hata aje nani pale tff hatuwezi kufuzu mashindano yoyote kwa sasa, malinzi mnamuonea tu, tena tatizo kubwa ni team nyamlani ndio inahujumu soka letu

Hao timu Nyamlani ndio walimfukuza Poulsen na kumleta huyo babu Nooj?
Ndio walihamisha ofisi za TFF kutoka Karume hadi Posta?
 
Zipo online now ni kichefuchefu kabisa kwa ubunifu wa hovyo!

Then TFF wamesema kwa umaridadi wa jezi hizi mpya wana uhakika sasa Taifa Stars itaanza kushinda games zake

Ehehehehe TFF kweli watz tunayo

Kama ushindi ungekuwa unapatikana kutokana na uzuri wa jezi basi Barcelona ingekuwa daraja la kumi na mbili.
 
J Malinzi maombi ya azamfc na yanga kutaka kuzidisha wachezaji wa kigeni mbona hamlitolei jibu kwa nini mda unaenda wachezaji wanagharamikiwa kukaa kwenye mahoteli naomba ulitolee ufafanuzi mapema

Jamal Malinzi njoo huku ukate kiu ya wadau,otherwise futa huu uzi wako kama huna majibu. Kumbuka hata mkulu alipoingia pale alianzisha kujibu maswali live lakini maswali yalipokuwa magumu alisepa hadi leo ameamua kuishi angani. Nawe nakupa ushauri wa bure kama mambo yamekuwia magumu,FUTA UZI HUU ili tusiwe tunapoteza resources kuja humu
 
kwa hili J Malinzi tunaomba utujuze:
kuna habari kilimanjaro bia wanataka kudhamini ligi kuu kwa hela ndefu lakini kuna tv moja inayoonyesha inakuzuia eti haiwezi kutangaza pombe je ni kweli?


usipolijibia hili tutajua madai hayo ni kweli
 
Hatumuitaji huyo kocha wako . Angalia jirani zetu Rwanda,Uganda na Kenya sisi wakufungwa Tatu bila na samata na ulimwengu ndani . Achia madaraka malinzi
 
Jamal Malinzi ulipotufikisha na team ya Taifa hatuwezi kukusamehe!Ulikoseatoka siku ya kwanza kwenye teuzi zako,ukakosea zaidi kwa kumuondoa kocha anayejua KIM sababu tu aliletwa na Tenga!

TAIFA STARS inacheza kama vilema!Team inafungwa na na Swaziland utamfunga vipi Pharao?Malinzi ni kiongozi wa hovyo hovyo kabisa kupata kuonwa na mm
 
Last edited by a moderator:
Sijajua hadi leo why alimuondoa Kim kamleta huyu mwehu wake

Anajua yeye mwenyewe,watu tunafungwa na timu za hovyo,taifa lina watu mil 47 hamna wachezaji 11 wa maana wakati kuna nchi wapo mil kama 4 na wanajielewa,huyu jamaa ajiuzulu
 
-Malinzi huyu jamaa wa hovyo sana, alimtimua kim poulsen akatuletea huyu mcheza cinema Mart Nooij.
-Akaleta kanuni ya kadi tatu za njano mchezaji kuchagua mechi za kukosa kucheza.
-Ni huyu malinzi alithubutu kuhamisha ofisi za tff pale karume.
 
Mnapoteza muda bure kwenye huu uzi, Jamali malinzi hawezi kuja tena hapa kwenye huu uzi (mark my words)

Labda tuwaombe Moderator waufunge tu hauna maana tena kuwepo hewani ikiwa mhusika amesepa!

likewise JK aliingia na gia hii hii ya kujibu maswali kupitia mitandao (twitter) maswali yalipokuja kuwa magumu na majibu hamna hata kudanganyia akatokomea na hiyo accounts kusikojulikana hadi leo!

vivyo hivyo kwa malinzi majibu ya maswali haya na fedheha tunayopata hana majibu yake ndio maana ameamua atokomee kusikojulikana!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: PNC
Mechi 4 tumepigwa bila kuscore a single goal, bado Malinzi kamkumbatia huyu babu, hii naiona kwako
 
Kim Alikua na mpango mizuri sana hopeful tungekua somewhere kwa ile trend
 
Malinzi, jana nimekushuhudia ukisema kwa kinywa kipana kabisa kwamba Kamati ya Utendaji ya TFF ilishampa majukumu kocha wa Timu ya Taifa na hivyo hawezi kutoka. Ukasema Kamati ya Utendaji ya TFF imempa kazi ya kuipekeka CHAN timu ya Taifa na hivyo hata ikifungwa kocha hawezi kutolewa. Atatoka tu ikiwa atashindwa kuipeleka timu CHAN! Watu wanataka kocha aende zake tupate kocha atakaye tuletea ushindi lakini wewe unasema Kamati ya Utendaji ilishaamua, hivi Kamati ya Utendaji ni kwa ajili ya nini? Tunataka mpira, tunataka ushindi, hatutaki maamuzi ya Kamati ya Utendaji ambayo hayatusaidii.

Unataka hadi tufungwe na nchi gani ndio Kocha aondoke? Tumefungwa na Swaziland ambayo ni nchi unayoweza kuizunguka kwa siku moja, bado tunataka tufungwe na nani ili kocha aonekane hafai?

Hivi Ndugu Malinzi kwa maana hiyo Kuipeleka timu AFCON siyo jukumu la Kocha? Kwa nini tunatumia pesa zetu kuipeleka timu nje ya nchi kwenye mashindano ya AfCON? Naona kwa hakika kuna shida kubwa huko TFF.

Malinzi tunataka mpira, tunataka kocha wa kuleta ushindi, hatutaki utetezi wa maamuzi ya kamati ya utendaji ambayo yahatusaidii.
 
Mushaija kalala mbele..... ila Malinzi anatutisha wengi..... pamoja na madhaifu ya Tenga lakini kulikuwa na uelekeo, matumaini.....sasa hivi tumerudi zero.....
 
wadau wenzangu mbona siku hizi malinzi hajibu maswali ya wadau kufumgwa kwa stars ndio ashindwe kuwajibu
 
Back
Top Bottom