Hon. Jamal Malinzi naomba nikupongeze kwa jinsi unavyotenga muda kujibu maswali ya Wakuu hapa jamvini. Endelea na moyo huo wa kiungwana na Mungu akubariki ufanikiwe zaidi katika kazi zako zote.
Huyu ni president wa kuigwa,unatenga muda kujadili na wadau,umechukua hatua kutaka kulinusuru taifa kuwa kichwa cha mwandawazimu,hata kama ukifeli kwenye crash programe sio mbaya umeonesha njia umeplay part yako kilichobaki ni wachezaji na kocha wao,big up,wenye majungu weka pembeni,halafu swala la watunza kumbukumbu sijui kama ofisi yako inawatu wa masijala,mh hawa watu ni muhimu ktk kila taasisi ushauri tu
President J.Malinzi nina maswali mawili.
1. Kwakuwa viwanja vingi vinamilikiwa na CCM na wakati huo wakivijenga ulikuwa ni mfumo wa chama kimoja. Je, kwanini TFF isiishauri Serikali kumiliki viwanja hivyo ili ibaki mali ya watanzania wote na ukizingatia sasa ni mfumo wa vyama vingi kitu ambacho kitasaidia viwanja kutunzwa vizuri na kuboreshwa zaidi?
2. Kama namba 1 hapo juu ni vigumu na najua kwamba mwenyekiti wa CCM (JK) ni mpenda michezo, kwanini sasa usiutumie muda huu akiwa madarakini ukamshauri kwa uzuri kabisa chama chake kitenge bajeti ya kukarabati viwanja vyake ikiwa ni pamoja na kubadili pitch ziwe za nyasi bandia?
SaaMbovu kwa maoni yangu mimi naona njia rahisi ni TFF kuwa na kampuni tanzu ambayo itaingia ubia na wamiliki wa viwanja.TFF itaweza kupata mtaji kupitia joint venture kuweza kuendeleza na kusimamia viwanja hivi.Kikubwa iwepo nia.
Asante. Ushauri wako mzuri na ni vizuri ukaufanyia kazi. Maana si lazima tujiandae kwa kucheza AFCON tu bali kujiandaa hata kuweza kuwa wenyeji wa AFCON miaka ya mbele kitu ambacho kitawezeshwa na ubora wa viwanja pamoja na mengine.
Mjasiria Akili si kila nchi yenye timu bora ya taifa ina ligi bora,mfano ni Zambia performance ya vilabu vyao afrika unaijua ukilinganisha na Chipolopolo,na si kila nchi yenye ligi bora ina timu nzuri ya taifa na mfano ni South Africa ambapo orlando Pirates majuzi tu kazi yao imeonekana.Muheshimiwa rais wa tff
Dunianiakote timu bora ya taifa hutokana na ligi bora ya nchi husika pamoja na timu bora zinazocheza ligi hiyo
Swali: huu mpango wa kuunda sijui kikosi kazi cha makocha kwenda kutafuta vipaji nchi nzima na kiwachuja na kuwaweka shule sijui kambi mmeupata wapi na kwa mtazamo wangu watakuwa vijana wa tff nyinyi mnaona ni sahihi?
2: kuna mdhamini coca cola ambaye anadhamini mashindano ya vijana kwa nn msitumie mashindano yake kupeleka wataalam kila mkoa au wilaya ili wasaidie kuchagua vijana sahihi ili waje kucheza mashindano hayo na hapo ndio patumike kutangeneza hiyo timu ya vijana?
Viwanja ni muhimu sana. nimebahatika leo kutembelea idara ya mashindano Makao makuu ya CAF Cairo wameniambia tunapojiandaa kuomba fainali za vijana Afrika mwaka 2019 lazima nyasi za viwanja vya mazoezi zifanane na za mashindano yenyewe.
Mjasiria Akili si kila nchi yenye timu bora ya taifa ina ligi bora,mfano ni Zambia performance ya vilabu vyao afrika unaijua ukilinganisha na Chipolopolo,na si kila nchi yenye ligi bora ina timu nzuri ya taifa na mfano ni South Africa ambapo orlando Pirates majuzi tu kazi yao imeonekana.
Sipendi kuongelea sana copa coca cola ,ni mashindano mazuri tunashukuru lakini kazi ya ziada inahitajika ili tuweze kufikia malengo ya mashindano yenyewe.
Swali kubwa la kujiuliza ni je tukishawapata hawa vijana ,iwe ni tokana na copa coca cola ,uhai cup au airtel rising stars tunawatunza na kuwaendeleza vipi na kwa gharama za nani? That is the big question,wadau wote kwa pamoja tutafute jibu la swali hili.
Mr President,
Hili la kuchukulia mfano wa Zambia na South africa mimi sikubaliani na we kwa sababu hizi.
1) South africa, ni kama DRC ambao tumeona TP Mazembe inafanya vizuri saana katika mashindano ya kimataifa, lakini timu yao ya Taifa ya DRC si ya kutisha. hii ni kwa sababu angalia ni wachezaji wangapi kwenye hii timu ya TP Mazembe ni raia wa DRC? The same to Orlando Pirates ya South africa.
Hii hata Ulaya tumeliona, Inter Milan, ilichukua kikombe cha klabu bingwa ya ulaya, ikiwa timu ya kwanza iliyoko uwanjani, hamna mchezaji wa kitaliano, aliyekuwezpo ni Materaz na yeye alikuwa mchezaji wa akiba.
Angalia Chelsea, imechukua ubingwa pia ni wachezaji wangapi walikuwa raia wa England, kama sikose walikuwa 3, sasa utaona ni vipi timu za taifa hazikunafaika. tazama arsenal ina wachezaji wangapi wazawa, man City wangapi wazawa wa england, hapo kweli unategemea kuwe na impact kwenye timu ya England?
Sasa angalia timu ya Taifa ya Spain, ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa ni wachezaji wangapi walikuwa wanatoka Barcelona? Na in fact, hata patten na uchezaji wake ulikuwa unafata uchezaji wa Barca. Mafanikio ya Barcelona yameonekana dhahiri kuinufaisha timu ya Taifa, kwa sababu timu ya barcelona ina idadi kubwa ya wazawa kwenye kikosi cha kwanza. Hivyo impact yake inaonekana.
Ukiwa na vilabu vizuri viwe na idadi kubwa ya wazawa na vikawa na mafanikio mtakuwa na wachezaji wazuri saana. Tazama Nigeria, impact ya Enyimba, Egypt impact ya vilabu vyao.
Takwimu unazotumia za mifano za nchi mbili, hazikidhi haja ya kuhalalisha kuwa lingi na vilabu imara si muhimu kujenga timu nzuri, ndo maana narusi msaidizi wako apindike kufanya utafiti yakinifu.
2) Ni ukweli usiofichika bila kuwa na vilabu vizuri na ligi nzuri, ni vigumu kuwa na timu ya taifa yenye mafanikio.
Mr President,
Nakubaliana na wewe kabisa huu mjadala wa wachezaji wa nje, ni mkubwa saana kwa mataifa mengi. Mimi nilikuwa nataka tu kukuonyesha uwiano wa mafanikio katika timu ya taifa na mafanikio ya klabu katika nchi.
Nina uhakika na imani kuwa tukiwa na vilabu imara, tukawa na ligi nzuri tutaona matunda yake, cha muhimu ni wadau kukaa na kuona je ni jinsi gani swala la wachezaji wa nje liwe, kwangu namba tuliyonayo si mbaya kabisa, kwanza inawafanya wachezaji wetu (wazawa) wakazane na kupambana kupata namba.
Tukirejea kwenye kuporomoka kwa kiwango cha timu yetu ya Taifa, sijui kama wewe binafsi na wadau wengine kweli tulijiuliza nini lilikuwa tatizo la timu yetu kuanguka vibaya chini ya mwalimu Kim?
Maximo, alitutoa kwa kweli ICU, na kwa kiasi fulani alirudisha morali mkubwa kwa watanzania kuipenda timu yao, pia naweza kusema uchaguzi wake wa wachezaji ulikwenda na kiwango na nidhamu. Tazama Burkina Faso, wamewezaji kujijenga muda mfupi?
Sasa kuja kwa huyu Kim ambaye mpaka sasa yupo, hebu tujiulize, ilifikia anachagua wachezaji ambao hata kwenye timu yao hawachezi, ni wachezaji wa akiba, akachagua wachezaji wamefungiwa hawajacheza miezi karibuni minnne. hivi kweli tulitegemea timu ifanye vizuri?
Kuna watu watasema oooh, tumezoea u Simba na Yanga, hapana kwa hili hivi nini kilikuwa chini ya carpet kati yake na Azam? matokeo yake kaua upenzi wa watanzania kwa timu ya Taifa. Binafsi sitashangaa wala kustushwa kuwa alikuwa paid kuiuza azam kwa kuwachukua wachezaji wake.
Na tukiendelea na Kim, sishangai kama hatutakosa wafadhili kwa timu ya Taifa, itakuwa bora waende wakafadhili Simba na Yanga.
Mkuu Jamal Malinzi Heshima yako na pole na majukumu,
Nina swali moja tu.. Kuna mpango wa kuhamisha Ofisi za sasa za TFF na kuhamia PPF TOWER sababu kubwa ni kupisha urekebishaji wa miundombinu ili iwe tayari kwa uwekezaji, Je Uwekezaji huo ni wa kisoka ama wa kibiashara?
-Lakini taarifa zilizosambaa miongoni mwa wanahabari ni kwamba uliwahi kutamka kwamba ofisi za sasa za TFF ziko eneo la biashara na HAZINA HADHI ya TFF, Pengine utufafanulie "Hadhi ya ofisi ya TFF ni ipi?
-Kuna hili suala la kwamba Viwanja VYOTE vya Michezo/ Mpira vilivyoko mikoani si mali ya TFF bali ya Ccm..jambo hili lina ukweli kiasi gani?
La mwisho, Kwa hili lililotokea Jijini Mbeya..Nini mtazamo wako kama kiongozi wa shirikisho la soka nchini!?
View attachment 140772