Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

President J.Malinzi nina maswali mawili.
1. Kwakuwa viwanja vingi vinamilikiwa na CCM na wakati huo wakivijenga ulikuwa ni mfumo wa chama kimoja. Je, kwanini TFF isiishauri Serikali kumiliki viwanja hivyo ili ibaki mali ya watanzania wote na ukizingatia sasa ni mfumo wa vyama vingi kitu ambacho kitasaidia viwanja kutunzwa vizuri na kuboreshwa zaidi?
2. Kama namba 1 hapo juu ni vigumu na najua kwamba mwenyekiti wa CCM (JK) ni mpenda michezo, kwanini sasa usiutumie muda huu akiwa madarakini ukamshauri kwa uzuri kabisa chama chake kitenge bajeti ya kukarabati viwanja vyake ikiwa ni pamoja na kubadili pitch ziwe za nyasi bandia?
 
Huyu ni president wa kuigwa,unatenga muda kujadili na wadau,umechukua hatua kutaka kulinusuru taifa kuwa kichwa cha mwandawazimu,hata kama ukifeli kwenye crash programe sio mbaya umeonesha njia umeplay part yako kilichobaki ni wachezaji na kocha wao,big up,wenye majungu weka pembeni,halafu swala la watunza kumbukumbu sijui kama ofisi yako inawatu wa masijala,mh hawa watu ni muhimu ktk kila taasisi ushauri tu

kutengeneza data base ni jambo la muhimu na la haraka,tunalifanyia kazi.
 
President J.Malinzi nina maswali mawili.
1. Kwakuwa viwanja vingi vinamilikiwa na CCM na wakati huo wakivijenga ulikuwa ni mfumo wa chama kimoja. Je, kwanini TFF isiishauri Serikali kumiliki viwanja hivyo ili ibaki mali ya watanzania wote na ukizingatia sasa ni mfumo wa vyama vingi kitu ambacho kitasaidia viwanja kutunzwa vizuri na kuboreshwa zaidi?
2. Kama namba 1 hapo juu ni vigumu na najua kwamba mwenyekiti wa CCM (JK) ni mpenda michezo, kwanini sasa usiutumie muda huu akiwa madarakini ukamshauri kwa uzuri kabisa chama chake kitenge bajeti ya kukarabati viwanja vyake ikiwa ni pamoja na kubadili pitch ziwe za nyasi bandia?

SaaMbovu kwa maoni yangu mimi naona njia rahisi ni TFF kuwa na kampuni tanzu ambayo itaingia ubia na wamiliki wa viwanja.TFF itaweza kupata mtaji kupitia joint venture kuweza kuendeleza na kusimamia viwanja hivi.Kikubwa iwepo nia.
 
Last edited by a moderator:

Asante. Ushauri wako mzuri na ni vizuri ukaufanyia kazi. Maana si lazima tujiandae kwa kucheza AFCON tu bali kujiandaa hata kuweza kuwa wenyeji wa AFCON miaka ya mbele kitu ambacho kitawezeshwa na ubora wa viwanja pamoja na mengine.
 
Last edited by a moderator:
Habari bwana Malinzi,
Mimi naomba nishauri vitu viwili kwa sasa.
- Wachezaji wengi wanapata shida sana kupata video zinazoonyesha highilights zao. Ni vigumu sana mchezaji kupata ushirikiano kutoka katika makampuni ya media (TV) ili aweze kupata video mbalimbali alizocheza ili atengeneze video fupi kama CV. Mchezaji kuwa na video nzuri inasaidia sana kutengeneza interest kutoka kwa klabu inayotafuta mchezaji. Kwa mfano, mimi kama Wakala, naweza nisiwe na mchezaji katika portofolio yangu anayecheza katika nafasi fulani, lakini naweza kujua timu inatafuta mchezaji fulani. Inakuwa rahisi kwangu kuja kuomba video (kwa mfano kutoka TFF) ya mchezaji anayecheza nafasi hiyo na kuipeleka katika klabu yenye mahitaji ya mchezaji.
Nashauri, kwa mchezaji yeyote anayeitwa timu ya Taifa, basi atengenezewe video highlights ya dakika 5 hadi 8 tu na kopi iwepo hapo TFF.

- Kuna wachezaji wanaenda mashindano ya U-17, kama Airtel mwaka jana, au Copa Coca Cola South Africa mwaka jana au juzi. Nimejaribu kufuatilia video zao, highlights tu za mashindano hayo, nimegonga mwamba. Kuna kiongozi wa msafara wa Airtel nilimwomba ushirikiano nipate hizo video. Sielewi hata kwanini sikupata huo msaada. Nikawa najiuliza, hizi kampuni zinafanya marketing kwaajili tu ya kutafuta soko la wananchi bila kuwa na nia ya kuwasaidia hawa vijana au inakuwaje? Vijana hawa wa timu za vijana wako marketable zaidi ya timu za wakubwa. Please seize this moment. Naomba unisaidie kutafuta video za vijana wa Airtel mwaka jana, na Copa Coca Cola (aidha kutoka Coca Cola au Supersport wenyewe). Na mnapopeleka hawa vijana, hakikisheni hamuondoki bila mikanda ya highlights....otherwise, it beats the purpose of all the hardwork.

Nitakuja na maswali/mawazo mengine huko mbeleni.
 
dfk-agent:
1.Ninakiri na ugeni wangu TFF sina uhakika kama kuna mikanda recorded uya mashindano ya vijana ya huko nyuma.
2.Kwa kuanzia mechi za inter region kuboresha Taifa stars next week zote tumeamua zitakuwa video recorded.
3.Ukiweza naomba tuwasiliane kipitia jamalmalinzi@yahoo.com au +255754815543
 
Last edited by a moderator:
Muheshimiwa rais wa tff
Dunianiakote timu bora ya taifa hutokana na ligi bora ya nchi husika pamoja na timu bora zinazocheza ligi hiyo
Swali: huu mpango wa kuunda sijui kikosi kazi cha makocha kwenda kutafuta vipaji nchi nzima na kiwachuja na kuwaweka shule sijui kambi mmeupata wapi na kwa mtazamo wangu watakuwa vijana wa tff nyinyi mnaona ni sahihi?
2: kuna mdhamini coca cola ambaye anadhamini mashindano ya vijana kwa nn msitumie mashindano yake kupeleka wataalam kila mkoa au wilaya ili wasaidie kuchagua vijana sahihi ili waje kucheza mashindano hayo na hapo ndio patumike kutangeneza hiyo timu ya vijana?
 
Asante. Ushauri wako mzuri na ni vizuri ukaufanyia kazi. Maana si lazima tujiandae kwa kucheza AFCON tu bali kujiandaa hata kuweza kuwa wenyeji wa AFCON miaka ya mbele kitu ambacho kitawezeshwa na ubora wa viwanja pamoja na mengine.

Viwanja ni muhimu sana. nimebahatika leo kutembelea idara ya mashindano Makao makuu ya CAF Cairo wameniambia tunapojiandaa kuomba fainali za vijana Afrika mwaka 2019 lazima nyasi za viwanja vya mazoezi zifanane na za mashindano yenyewe.
 
Muheshimiwa rais wa tff
Dunianiakote timu bora ya taifa hutokana na ligi bora ya nchi husika pamoja na timu bora zinazocheza ligi hiyo
Swali: huu mpango wa kuunda sijui kikosi kazi cha makocha kwenda kutafuta vipaji nchi nzima na kiwachuja na kuwaweka shule sijui kambi mmeupata wapi na kwa mtazamo wangu watakuwa vijana wa tff nyinyi mnaona ni sahihi?
2: kuna mdhamini coca cola ambaye anadhamini mashindano ya vijana kwa nn msitumie mashindano yake kupeleka wataalam kila mkoa au wilaya ili wasaidie kuchagua vijana sahihi ili waje kucheza mashindano hayo na hapo ndio patumike kutangeneza hiyo timu ya vijana?
Mjasiria Akili si kila nchi yenye timu bora ya taifa ina ligi bora,mfano ni Zambia performance ya vilabu vyao afrika unaijua ukilinganisha na Chipolopolo,na si kila nchi yenye ligi bora ina timu nzuri ya taifa na mfano ni South Africa ambapo orlando Pirates majuzi tu kazi yao imeonekana.
Sipendi kuongelea sana copa coca cola ,ni mashindano mazuri tunashukuru lakini kazi ya ziada inahitajika ili tuweze kufikia malengo ya mashindano yenyewe.
Swali kubwa la kujiuliza ni je tukishawapata hawa vijana ,iwe ni tokana na copa coca cola ,uhai cup au airtel rising stars tunawatunza na kuwaendeleza vipi na kwa gharama za nani? That is the big question,wadau wote kwa pamoja tutafute jibu la swali hili.
 
Last edited by a moderator:
Viwanja ni muhimu sana. nimebahatika leo kutembelea idara ya mashindano Makao makuu ya CAF Cairo wameniambia tunapojiandaa kuomba fainali za vijana Afrika mwaka 2019 lazima nyasi za viwanja vya mazoezi zifanane na za mashindano yenyewe.

Asante sana. Hiyo ni Habari njema.
 
Mjasiria Akili si kila nchi yenye timu bora ya taifa ina ligi bora,mfano ni Zambia performance ya vilabu vyao afrika unaijua ukilinganisha na Chipolopolo,na si kila nchi yenye ligi bora ina timu nzuri ya taifa na mfano ni South Africa ambapo orlando Pirates majuzi tu kazi yao imeonekana.
Sipendi kuongelea sana copa coca cola ,ni mashindano mazuri tunashukuru lakini kazi ya ziada inahitajika ili tuweze kufikia malengo ya mashindano yenyewe.
Swali kubwa la kujiuliza ni je tukishawapata hawa vijana ,iwe ni tokana na copa coca cola ,uhai cup au airtel rising stars tunawatunza na kuwaendeleza vipi na kwa gharama za nani? That is the big question,wadau wote kwa pamoja tutafute jibu la swali hili.

Mr President,

Hili la kuchukulia mfano wa Zambia na South africa mimi sikubaliani na we kwa sababu hizi.
1) South africa, ni kama DRC ambao tumeona TP Mazembe inafanya vizuri saana katika mashindano ya kimataifa, lakini timu yao ya Taifa ya DRC si ya kutisha. hii ni kwa sababu angalia ni wachezaji wangapi kwenye hii timu ya TP Mazembe ni raia wa DRC? The same to Orlando Pirates ya South africa.

Hii hata Ulaya tumeliona, Inter Milan, ilichukua kikombe cha klabu bingwa ya ulaya, ikiwa timu ya kwanza iliyoko uwanjani, hamna mchezaji wa kitaliano, aliyekuwezpo ni Materaz na yeye alikuwa mchezaji wa akiba.

Angalia Chelsea, imechukua ubingwa pia ni wachezaji wangapi walikuwa raia wa England, kama sikose walikuwa 3, sasa utaona ni vipi timu za taifa hazikunafaika. tazama arsenal ina wachezaji wangapi wazawa, man City wangapi wazawa wa england, hapo kweli unategemea kuwe na impact kwenye timu ya England?

Sasa angalia timu ya Taifa ya Spain, ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa ni wachezaji wangapi walikuwa wanatoka Barcelona? Na in fact, hata patten na uchezaji wake ulikuwa unafata uchezaji wa Barca. Mafanikio ya Barcelona yameonekana dhahiri kuinufaisha timu ya Taifa, kwa sababu timu ya barcelona ina idadi kubwa ya wazawa kwenye kikosi cha kwanza. Hivyo impact yake inaonekana.

Ukiwa na vilabu vizuri viwe na idadi kubwa ya wazawa na vikawa na mafanikio mtakuwa na wachezaji wazuri saana. Tazama Nigeria, impact ya Enyimba, Egypt impact ya vilabu vyao.

Takwimu unazotumia za mifano za nchi mbili, hazikidhi haja ya kuhalalisha kuwa lingi na vilabu imara si muhimu kujenga timu nzuri, ndo maana narusi msaidizi wako apindike kufanya utafiti yakinifu.

2) Ni ukweli usiofichika bila kuwa na vilabu vizuri na ligi nzuri, ni vigumu kuwa na timu ya taifa yenye mafanikio.
 
Yombayomba huu mjadala ni mrefu na mpana sana.Kwa taarifa yako leo hii UEFA wanafikiria kuweka cap kwenye usajili kwamba vilabu vya Ulaya visajili wachezaji 25 tu na kisha viruhusiwe kutumia "unlimited home grown players",ni mjadala mzito na unaendelea. na hata hapa nyumbani hebu jiulize kama Federation unaanzaje kuingilia uhuru wa vilabu kusajili,kumbuka vilabu vinataka ushindi wa "leo leo" ili wanachama na wapenzi wao wafurahi hivyo wakitaka magoli watamnunua Tambwe,Okwi,Kipre n.k.Ndio maana ninapendelea maamuzi yanayohusu masuala nyeti kama haya yapitie kwenye vikao.
 
Last edited by a moderator:
Mr President,

Nakubaliana na wewe kabisa huu mjadala wa wachezaji wa nje, ni mkubwa saana kwa mataifa mengi. Mimi nilikuwa nataka tu kukuonyesha uwiano wa mafanikio katika timu ya taifa na mafanikio ya klabu katika nchi.

Nina uhakika na imani kuwa tukiwa na vilabu imara, tukawa na ligi nzuri tutaona matunda yake, cha muhimu ni wadau kukaa na kuona je ni jinsi gani swala la wachezaji wa nje liwe, kwangu namba tuliyonayo si mbaya kabisa, kwanza inawafanya wachezaji wetu (wazawa) wakazane na kupambana kupata namba.

Tukirejea kwenye kuporomoka kwa kiwango cha timu yetu ya Taifa, sijui kama wewe binafsi na wadau wengine kweli tulijiuliza nini lilikuwa tatizo la timu yetu kuanguka vibaya chini ya mwalimu Kim?

Maximo, alitutoa kwa kweli ICU, na kwa kiasi fulani alirudisha morali mkubwa kwa watanzania kuipenda timu yao, pia naweza kusema uchaguzi wake wa wachezaji ulikwenda na kiwango na nidhamu. Tazama Burkina Faso, wamewezaji kujijenga muda mfupi?

Sasa kuja kwa huyu Kim ambaye mpaka sasa yupo, hebu tujiulize, ilifikia anachagua wachezaji ambao hata kwenye timu yao hawachezi, ni wachezaji wa akiba, akachagua wachezaji wamefungiwa hawajacheza miezi karibuni minnne. hivi kweli tulitegemea timu ifanye vizuri?

Kuna watu watasema oooh, tumezoea u Simba na Yanga, hapana kwa hili hivi nini kilikuwa chini ya carpet kati yake na Azam? matokeo yake kaua upenzi wa watanzania kwa timu ya Taifa. Binafsi sitashangaa wala kustushwa kuwa alikuwa paid kuiuza azam kwa kuwachukua wachezaji wake.

Na tukiendelea na Kim, sishangai kama hatutakosa wafadhili kwa timu ya Taifa, itakuwa bora waende wakafadhili Simba na Yanga.
 
Mkuu Jamal Malinzi Heshima yako na pole na majukumu,

Nina swali moja tu.. Kuna mpango wa kuhamisha Ofisi za sasa za TFF na kuhamia PPF TOWER sababu kubwa ni kupisha urekebishaji wa miundombinu ili iwe tayari kwa uwekezaji, Je Uwekezaji huo ni wa kisoka ama wa kibiashara?

-Lakini taarifa zilizosambaa miongoni mwa wanahabari ni kwamba uliwahi kutamka kwamba ofisi za sasa za TFF ziko eneo la biashara na HAZINA HADHI ya TFF, Pengine utufafanulie "Hadhi ya ofisi ya TFF ni ipi?

-Kuna hili suala la kwamba Viwanja VYOTE vya Michezo/ Mpira vilivyoko mikoani si mali ya TFF bali ya Ccm..jambo hili lina ukweli kiasi gani?

La mwisho, Kwa hili lililotokea Jijini Mbeya..Nini mtazamo wako kama kiongozi wa shirikisho la soka nchini!?

Mbeya.jpg

Wasalaam,

Adrian Stepp!
 
Yombayomba leo nilikuwa na Dr Danny Jordan Rais wa Federation ya South Africa wameweka kanuni ya 5+6 yaani dimbani wazawa sita wageni watano kwa kila mechi,lakini je italeta tija,Rais wa Federation ya Nigeria kaniambia kwao ni hela yako tu we sajili tu,kiukweli hakuna fixed formula kwenye kuweka uwiano wa wageni na wazawa katika usajili.
Hili la kocha wa timu ya Taifa hapa sio mahali pake mimi kuliongelea,ila kama ni kukuelewa nimekuelewa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Jamal Malinzi Heshima yako na pole na majukumu,

Nina swali moja tu.. Kuna mpango wa kuhamisha Ofisi za sasa za TFF na kuhamia PPF TOWER sababu kubwa ni kupisha urekebishaji wa miundombinu ili iwe tayari kwa uwekezaji, Je Uwekezaji huo ni wa kisoka ama wa kibiashara?

-Lakini taarifa zilizosambaa miongoni mwa wanahabari ni kwamba uliwahi kutamka kwamba ofisi za sasa za TFF ziko eneo la biashara na HAZINA HADHI ya TFF, Pengine utufafanulie "Hadhi ya ofisi ya TFF ni ipi?

-Kuna hili suala la kwamba Viwanja VYOTE vya Michezo/ Mpira vilivyoko mikoani si mali ya TFF bali ya Ccm..jambo hili lina ukweli kiasi gani?

La mwisho, Kwa hili lililotokea Jijini Mbeya..Nini mtazamo wako kama kiongozi wa shirikisho la soka nchini!?

View attachment 140772
 
Mr President,

Nashukuru kwa ufafanuzi wako, na hata mimi sikutaka jibu kwenye swali la pili kwani hapa si mahala pakee, lakini kwangu mimi ambaye si mjumbe wa kamati kuu ya utendaji hapa ndo pa kueleza paungufu tuliyaona, ili na ni kipi na wengine mkitazame ili kuijenga timu yetu.

Natumaini kwa wote tuliona, yaani inafikia wachezxaji wakoma kwenda kwenye mashindano, inapidi Marsha awabembelelze, hiyo ilikuwa fedheha kubwa kwa Taifa letu, kwani mahali popote duniani, ni heshima kubwa kuchezea timu ya Taifa, kwa mchezaji its a very prestige kuchezea timu ya taifa na kuvaa nembo ya Taifa lako kifuani.

Nakutakia kila la kheri
 
Habari bwana Malinzi,
TFF ina Wakala gani ambao wako chini yake? Kupitia mtandao wa FIFA naona majina ya Ally Saleh, Mehdi Remtulla na John Ndumbaro tu.
Asante
 
Mkuu dfk kadito mawakala wanaotambulika na fifa toka tanzania ndio hao hao hata mi nimeona majina hayo hayo kwenye mtandao wa fifa
 
Back
Top Bottom