Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

hahahaaha kibiashara swali tata hili!

Ndugu Rais Navyojua mimi Vodacom ni mdhamini wa ligi kuu na wala si mdhamini wa TFF sasa kwa kuzingatia hilo kisheria mpo huru nyie kama TFF kushirikiana na makampuni mengine shindani na Voda kwenye kitu kingine chochote nje ya product wanayoidhamini ambayo ni ligi kuu....I stand to be corrected.
 
mbona ujenzi wa uwanja wa nyamagana hauanzi wakati halmashauri ya jiji la mwanza walishatoa pesa zote walizotakiwa kutoa?
 
Hivi azam media..imeingia mkataba na tff kurusha mechi za taifa stars?...nimeona mara nyingi toka azam media imeingia wamekua wakirusha live mechi za stars....
Nazungumzia..mkataba wa haki za kuonesha. Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:

Ngokongosha kuna document jiji mwanza walikuwa hawajasaini na FIFA walisema ujenzi hauanzi mpaka isainiwe.Imesainiwa tayari hivyo mkandarasi wakati wowote ataanza kazi
 
Last edited by a moderator:
Hivi azam media..imeingia mkataba na tff kurusha mechi za taifa stars?...nimeona mara nyingi toka azam media imeingia wamekua wakirusha live mechi za stars....
Nazungumzia..mkataba wa haki za kuonesha. Jamal Malinzi

Kipaji Halisi mwenye haki ya matangazo ya Afcon qualifiers ni shirikisho la mpira wa miguu Afrka CAF
 
Last edited by a moderator:
Soka la Tanzania linasuasua sana na haya ni matokeo ya kutokuwa na shule za uhakika na makini za soka la watoto na vijana,nakushauri ongea na watu wa JKT Ruvu muanzishe shule ya soka ya mfano na makini yenye viwango vya kimataifa ,nimependekeza Ruvu JKT kwa sababu tiyari wanayo timu ya ligi kuu,wana eneo kubwa, wana viwanja vitatu vya soka ambavyo viwili vinafaa kwa mazoezi na kimoja kwa mechi,kuna shule za msingi na sekondari maeneo karibu na kambi,Pia kambi ya Ruvu ipo mahali panapofikika kwa urahisi.

Mnaweza kushirikisha wadau wengine kwenye suala hili na hiyo shule ya soka mtakuwa mnaimiliki TFF na JKT.

Pia tengenezeni sheria za kulinda wachezaji wa hizo academy ,mtu unaweza kuanzisha academy yako baaada ya kutengeneza wachezaji timu nyingine zinakuja kuwachukua kiurahisi.
 
Wangekua na nia kweli ya kureta mabadiliko huu ushauri wako sio wakupuuza...!!
 
Daraja la miti muda si mrefu tutaanza zoezi la kujua ramani ya mpira Tanzania, ni kweli Ruvu JKT inaweza kufaa kwa mipango ya shule ya kukuza na kulea vipaji lakini je ni Ruvu peke yake?

Lazima tupate ramani ya nchi nzima tujue tukifanya mashindano ya kitaifa umri chini ya miaka 13 vipaji vitakavyoibuliwa kimaeneo vitapelekwa kwenye local academies zipi? Gharama za kuwatunza tujue zitakuwa kiasi gani?

Malezi yao kimpira watahitaji tournaments ndani na nje ya nchi je gharama za ushiriki wao zitakuwa kiasi gani? Vifaa,malipo ya walimu,tiba nk zitakuwa kiasi gani? Youth development inahitaji uwekezaji mkubwa,lakini tusiogope tukiamua tunaweza.
 
Wangekua na nia kweli ya kureta mabadiliko huu ushauri wako sio wakupuuza...!!

Jaslaws nia ya dhati ya kuwekeza kwenye maendeleo ya mpira wa vijana ipo,tukijaliwa oktoba tutazindua program ya taifa ya maendeleo ya mpira wa vijana.
 
Last edited by a moderator:
kambi ya timu ya taifa inawekwa tukuyu sehem yenye hali ya baridi.kisha timu inaenda kucheza dar kwenye joto jingi,ivi wataalam wa soka hili hawalioni kuwa nitatizo pia?
 
kuna sheria gani ya kumlinda mwekezaji anayeanzisha shule ya soka,kuhusu kuibiwa wachezaji wake?
 
Mkuu hili swali aliulizwa mheshimiwa ila majibu yake nilistaajabu mwenyewe. Pekuapekua kwenye huu uzi utayapata.
 
Malinzi,

Hivi CECAFA, inashirikisha vyama wanachama katika kuanadaa mashindano(ratiba) yake, i.e klabu bingwa? Na je nia hasa haya mashindano ni nini? kukuza mpira ukanda huu, biashara, kukuza maelewano ya viongozi? Nauliza hivi, kwa sababu, nikiangali tu tuchukulie mfano wa wawakilishi wa Tazania bara (Tanganyika) Yanga, hivi kweli tunategemea wafanye vizuri? au wanakwenda tu kushiriki si kupigania kuchukua kombe? Kwa nini nasema hivi?

1) Yanga inawachezaji wengi kwenye timu za taifa za ukanda huu, hawa wachezaji wanamaliza mashindano tarehe 4 August, na mashindano yanaanza tarehe 8 August. Yanga inaweza kuwa pata tarehe 5, ikiwa ina bahati, sasa watacheza vipi na wenzao? wana kocha mpya na mfumo mpya? kuna haki kweli hapo, yaani wafanye mazoezi siku moja?

2) Hawa wachezaji, toka ligi iishe hawajapumzika vya kutosha, in fact, wanatakiwa angalau wapumzike wiki moja kabla ya kuungana na kalbu zao, miili yao imechoka, hata kimawazo, kweli tunategemea wafanye vizuri?

3) Kama TFF inajali kukuza kiwango cha timu, nakuomba uishauri na kuiunga mkono Yanga iwakilishwe na kikosi cha under 20, ili kuwapa fursa vijana na kujenga timu ya baadae, timu A, itawaharibia maandalizi ya ligi tu. CECAFA haina faida katika kukuza mpira kwa mwendu huu walioonyesha.
 
kambi ya timu ya taifa inawekwa tukuyu sehem yenye hali ya baridi.kisha timu inaenda kucheza dar kwenye joto jingi,ivi wataalam wa soka hili hawalioni kuwa nitatizo pia?
D2050 mambo yanayohitaji uweledi tuwaachie makocha,mfano kambi ya botswana mimi nilishafanya mpango timu iende Amman Jordan kocha akasema hapana anahitaji high altitude na baridi,ni mtaalam ana sababu zake,tumheshimu na tumwache afanye kazi yake.
 
kuna sheria gani ya kumlinda mwekezaji anayeanzisha shule ya soka,kuhusu kuibiwa wachezaji wake?

FIFA wametunga kanuni za kuwalinda wawekezaji wa soccer academies,sasa hivi below 17yrs of age transfer haziruhusiwi,ndo maana majuzi Barcelona walifungiwa na FIFA,wame appeal
 
Malinzi,

Hivi CECAFA, inashirikisha vyama wanachama katika kuanadaa mashindano(ratiba) yake, i.e klabu bingwa? Na je nia hasa haya mashindano ni nini? kukuza mpira ukanda huu, biashara, kukuza maelewano ya viongozi? Nauliza hivi, kwa sababu, nikiangali tu tuchukulie mfano wa wawakilishi wa Tazania bara (Tanganyika) Yanga, hivi kweli tunategemea wafanye vizuri? au wanakwenda tu kushiriki si kupigania kuchukua kombe? Kwa nini nasema hivi?

1) Yanga inawachezaji wengi kwenye timu za taifa za ukanda huu, hawa wachezaji wanamaliza mashindano tarehe 4 August, na mashindano yanaanza tarehe 8 August. Yanga inaweza kuwa pata tarehe 5, ikiwa ina bahati, sasa watacheza vipi na wenzao? wana kocha mpya na mfumo mpya? kuna haki kweli hapo, yaani wafanye mazoezi siku moja?

2) Hawa wachezaji, toka ligi iishe hawajapumzika vya kutosha, in fact, wanatakiwa angalau wapumzike wiki moja kabla ya kuungana na kalbu zao, miili yao imechoka, hata kimawazo, kweli tunategemea wafanye vizuri?

3) Kama TFF inajali kukuza kiwango cha timu, nakuomba uishauri na kuiunga mkono Yanga iwakilishwe na kikosi cha under 20, ili kuwapa fursa vijana na kujenga timu ya baadae, timu A, itawaharibia maandalizi ya ligi tu. CECAFA haina faida katika kukuza mpira kwa mwendu huu walioonyesha.

MLUGU umejenga hoja za msingi,umesikika
 
Last edited by a moderator:
TFF tunzeni vipaji vinavoibuliwa katika mashindano mbalimbali kama rolling stone,copa coca cola,umiseta n.k kwa kuingiza timu ya vijana katika ligi kuu itasaidia kulinda vipaji na kuwakomaza madogo hili ndo pekee linaloendana na umaskini wetu.Wadau wa michezo ktk hili upi msimamo wenu?
 
Back
Top Bottom