Malinzi,
Hivi CECAFA, inashirikisha vyama wanachama katika kuanadaa mashindano(ratiba) yake, i.e klabu bingwa? Na je nia hasa haya mashindano ni nini? kukuza mpira ukanda huu, biashara, kukuza maelewano ya viongozi? Nauliza hivi, kwa sababu, nikiangali tu tuchukulie mfano wa wawakilishi wa Tazania bara (Tanganyika) Yanga, hivi kweli tunategemea wafanye vizuri? au wanakwenda tu kushiriki si kupigania kuchukua kombe? Kwa nini nasema hivi?
1) Yanga inawachezaji wengi kwenye timu za taifa za ukanda huu, hawa wachezaji wanamaliza mashindano tarehe 4 August, na mashindano yanaanza tarehe 8 August. Yanga inaweza kuwa pata tarehe 5, ikiwa ina bahati, sasa watacheza vipi na wenzao? wana kocha mpya na mfumo mpya? kuna haki kweli hapo, yaani wafanye mazoezi siku moja?
2) Hawa wachezaji, toka ligi iishe hawajapumzika vya kutosha, in fact, wanatakiwa angalau wapumzike wiki moja kabla ya kuungana na kalbu zao, miili yao imechoka, hata kimawazo, kweli tunategemea wafanye vizuri?
3) Kama TFF inajali kukuza kiwango cha timu, nakuomba uishauri na kuiunga mkono Yanga iwakilishwe na kikosi cha under 20, ili kuwapa fursa vijana na kujenga timu ya baadae, timu A, itawaharibia maandalizi ya ligi tu. CECAFA haina faida katika kukuza mpira kwa mwendu huu walioonyesha.