Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Jamal Malinzi ni member JF.Njoo utueleze kwa nini hukusimamia maamuzi yako ya awali.Pia kwa nini ulihamisha ofisi za TFF Karume hadi katikati ya jiji? Umefanya maamuzi mengi yasiyo na maana,lakini kwa gharama kubwa.

bato nitazungumzia la kuhama Karume,mengine yako mahakamani kuyazungumzia hapa sio mahali pake.
Karume tunajenga maduka kuzunguka uwanja,ukumbi na hoteli ya ghorofa 7.Tutafanya uwekezaji huu bila kuingia ubia wala kukopa.Mapema July michoro itakamilika na tutaomba kibali cha ujenzi,tukijaaliwa ujenzi utaanza August.
 
Last edited by a moderator:
Salute kwako mh rais Malinzi! ili kuleta maendeleo ya soka, nadhani kuna mkakati wa mda mfupi na wa mda mrefu. Umelezea ktk huu uzi wako kuhusu walimu kuwa na ujuzi wa masuala ya soka ili wawafundishe hawa vijana wadogo/wanafunzi. Huu ni mkakati wa mda mrefu. Naomba utujuze mkakati wa mda mfupi wa TFF kuboresha soka letu kwa sasa? je, kuna utafiti wote uliofanyika kama kuna matatizo mengine kama ya kimazingira ya ukanda huu wa A. Mashariki ktk maendeleo ya soka, nauliza hivo make ktk soka ni kama tunafanana na km tofauti ipo ni ndg sana. Isije ikawa tunapiga kelele nyingi kumbe kuna sababu nyingine ya mazingira au biolojia ya watu wetu tofauti na watu wa A. Magh na Kask. vp kuhusu UMISETA na UMITASHUMTA mmeangalia kama zina mchango ktk kuibua vipaji vya wachezaji wachanga? Je, zipo shule za vipaji maalum ya soka? Viwanja vya baadhi ya mikoa na wilaya ni vibovu, hali hii pia huchangia ligi za madaraja ya chini kuwa mbovu, mkakati wenu upoje kuhusu viwanja hivi? Nawasilisha!!!!

Bayyo TFF hivi sasa iko kwenye hatua za mwisho za kuandaa program endelevu za maendeleo ya soka la vijana.Mipango ya Serikali na taratibu zake kama kuandaa Umitashumta itajumuishwa katika program hii.
 
Last edited by a moderator:
Mi swali langu ni kuhusu uchaguzi wa simba ulivyousimamisha je ni kwa sheria zipi au kwa misingi ipi umeamua kuisimamisha?
Je kutokuwa na kamati ya maadili ni sababu tosha? kama ndio kwann kipindi hiki na sio kipindi cha kabla?

chumvichumvi midhali hili suala liko mahakamani tusilozungumzie,ila nikihakikishie kila lililofanywa,kuamuliwa na kutangazwa na TFF katika suala hili lilifanywa kwa nia njwma na thabiti ya kuendeleza ustawi wa mpira wetu.
 
Last edited by a moderator:
Mi nawaombeeni dua mfanikiwe na huo ujenzi wa hapo karume kwa imani ya kwamba sio maneno matupu ila ushauri wangu ni vyema swala ilo la ujenzi ukaliweka bayana kwa uwazi zaidi kwa maana ya chanzo chenu cha pesa makadirio yenu, bajeti na kadhalika yanayohusu ujenzi huo sababu bila kufanya hivyo kama utujuavyo sisi watanzania atutakawia kukushtu uko mbeleni kwasababu tu misingi haikufahamika mapema
 
Positioning with "the powers to be".....could be a wrong move, either

unnamed+(5).jpg
 
nimeingia kwenye website yenu ya TFF kwa nia na madhumuni ya kupata katiba na nyaraka zingine zingine zinazohusu TFF kwa bahati mbaya cjabahatika kukuta chochote kuhusiana na ivo naomba kama utojali unielekeze wapi pa kuipata au uni-uploadie maana nipo arusha kwa sasa nanina shida nayo sana
 
Mi nawaombeeni dua mfanikiwe na huo ujenzi wa hapo karume kwa imani ya kwamba sio maneno matupu ila ushauri wangu ni vyema swala ilo la ujenzi ukaliweka bayana kwa uwazi zaidi kwa maana ya chanzo chenu cha pesa makadirio yenu, bajeti na kadhalika yanayohusu ujenzi huo sababu bila kufanya hivyo kama utujuavyo sisi watanzania atutakawia kukushtu uko mbeleni kwasababu tu misingi haikufahamika mapema

chumvichumvi hakuna usiri kwenye bajeti ya uwekezaji uwanja wa Karume.Tunajenga kwa awamu tatu:
Ya kwanza ni fremu za maduka 72 kuzunguka uwanja,tunaanza mwezi ujao,gharama 1.4bn Tsh.
Ya pili ni kujenga ukumbi wa mikutano,tunaanza May mwakani,gharama Tsh 450m,
Ya tatu na mwisho ni hoteli ya ghorofa saba,Bills of quantity zinaandaliwa.
Yote haya TFF itayafanya kwa vyanzo vyake yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
nimeingia kwenye website yenu ya TFF kwa nia na madhumuni ya kupata katiba na nyaraka zingine zingine zinazohusu TFF kwa bahati mbaya cjabahatika kukuta chochote kuhusiana na ivo naomba kama utojali unielekeze wapi pa kuipata au uni-uploadie maana nipo arusha kwa sasa nanina shida nayo sana

chumcichumvi naomba nikiri katika hili TFF imewaangusha wadau,nipe muda
 
Last edited by a moderator:
chumcichumvi naomba nikiri katika hili TFF imewaangusha wadau,nipe muda

Tena hili la kuboresha website ndugu Rais ukiamua linafanikiwa mara moja mapendekezo yangu muajiri system administrator haraka awe chini ya Wambura awe ni mtu mwenye passion na mpira na mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano, website ya TFF inaweza kujiendesha ata kibiashara kupitia wadhamini wa ligi zetu kama AZAM, VODACOM na ata wadhamini wa National Team TBL kinachotakiwa kufanyika ni kuiboresha iwe soooo updated muda wote kwa maana tukio kubwa la football likitokea isipite masaa mawili liwe kwenye website ya TFF ili wapenzi na washabiki wa soka tuone ndio source imara na ya uhakika.
 
chumvichumvi hakuna usiri kwenye bajeti ya uwekezaji uwanja wa Karume.Tunajenga kwa awamu tatu:
Ya kwanza ni fremu za maduka 72 kuzunguka uwanja,tunaanza mwezi ujao,gharama 1.4bn Tsh.
Ya pili ni kujenga ukumbi wa mikutano,tunaanza May mwakani,gharama Tsh 450m,
Ya tatu na mwisho ni hoteli ya ghorofa saba,Bills of quantity zinaandaliwa.
Yote haya TFF itayafanya kwa vyanzo vyake yenyewe.

Fremu 72 kwa Tshs 1.4Bn?
 
Malinzi,

Eneo hilo ni zuri saana kwa executive business center.
Hamtakiwi kujenga maduka, kuzunguka hapo na kuweka hotel, kumbuka unapoweka hayo maduko ya frame, hali ya usalama inakuwa ni mbaya saana, na hata watu wa kulala hapo unahatarisha maisha yao.

Kilichokuwa kinatakiwa na kujenga maofisi, na hotel ambayo kwa uhakika uwekezaji huo ungekuwa na tija zaidi na kuongeza madhari ya hapo.
 
Tar 18/07 timu yetu under 17 inacheza na South africa,muda wowote timu ya taifa under 23 itaingia kambini kujiandaa na mtoano wa Olympics Rio 2016.

Vipi maandalizi Kwa timu za wanawake..?...huwa hamchelewi kusema hamna bajeti ..
 
Bayyo TFF hivi sasa iko kwenye hatua za mwisho za kuandaa program endelevu za maendeleo ya soka la vijana.Mipango ya Serikali na taratibu zake kama kuandaa Umitashumta itajumuishwa katika program hii.

Asante kwa majibu mkuu! ombi langu kwako ni ujitahidi kujibu hoja za wadau, naamini wengi wana mawazo mazuri yenye kujenga ili mwisho wa siku tufikie malengo. Kama ambavyo tunashuhudia sasa hivi kivumbi cha kombe la dunia Brazil, matarajio ya Watz ni kuwa siku moja timu yetu ya taifa pia ishiriki. Ni kwa vp tunaweza kushiriki, nadhani nyie TFF mna mikakati, mtutimizie ndoto zetu watz. Mimi nakutakia kazi njema.
 
Last edited by a moderator:
Malinzi,

Tunaomba utume hesabu za gharama zilizotumika kuweka watu Lushoto, na Zanzibar kujadili kuboresha timu ya Taifa. Pia naomba gharama zilizotumika katika zoezi la kwenda kutafuta wachezaji mikoani, pamoja na kuwaweka kambini Tukuyu. Nadhani hizo hazitakiwi kuwa ni siri, hamna chochote cha kufanya kuwa ni siri. Na ikiwezekana tupe mchanganuo wa majina ya walioshiriki, na kulipwa pesa.
mluga kwani wewe una wasi wasi na gharama tulizotumia? Hebu nisaidie kitu kimoja,kwa maoni yako ni gharama kiasi gani inatakiwa kuibua na kumwendeleza mchezaji mmoja hadi afikie kiwango cha kuchezea National team yoyote ile duniani? Hivi unazo taarifa kuwa timu hii ya Taifa ya sasa ina wachezaji WANNE ambao wametokana na hii programme? Kwa taarifa timu ya Taifa ya umri chini ya miaka 23 itakayoingia kambini punde kujiandaa na mtoano wa kwenda Olyimpics Rio 2016 asilimia kubwa itatokana na vijana walioibuliwa kwenye program hii.
nikukumbushe tu kuwa sehemu nyingi duniani jukumu la kuibua na kulea vipaji ni la VILABU,hapa Tanzania hilo limekuwa tatizo la muda mrefu na ndio maana TFF tukaamua kuibua wenyewe na sasa hivi vilabu vya ligi kuu vinasajili hao vijana waliotokana na program ya maboresho,hivyo imekuwa vice versa lakini ndio hali halisi.Hata program ya Taifa umri chini ya miaka 13 under 13 ilitakiwa ifanywe na vilabu lakini kwa kuwa havifanyi hiVyo TFF hatuwezi kuruhusu hali ibaki hivyo hivyo tutaubeba huo msalaba ambao ni wa gharama kubwa.Tusitarajie maendeleo ya mpira,hasa wa vijana,kama tutakwepa gharama,hakuna nchi iliyokwenda WC Brazil ambayo miaka ya nyuma haikuwekeza pesa kwa vijana,tuliowaibua hakuna anayezidi umri miaka 23,they are our future.
 
Jamal Malinzi ni member JF.Njoo utueleze kwa nini hukusimamia maamuzi yako ya awali.Pia kwa nini ulihamisha ofisi za TFF Karume hadi katikati ya jiji? Umefanya maamuzi mengi yasiyo na maana,lakini kwa gharama kubwa.
bato kikubwa kilikuwa ni kuangalia ustawi wa klabu ya Simba na sio kupimana vifua,tunashukuru mwanachama wetu kamaliza uchaguzi salama,tuwaombee walioshinda waongoze vyema waimarishe klabu yao.
tulihama Karume kupisha ujenzi,utaanza punde.
 
Last edited by a moderator:
Fremu 72 kwa Tshs 1.4Bn?
Hayo ni makisio ya awali,michoro ikikamilika zitaandaliwa bills of quantities,tenda itatangazwa mchana kweupe na kila mkandarasi ataleta quotation yake.Hiyo hesabu tulitaka tupewe na wataalam kama makisio ya awali ili tujipime kama tunaweza,na tunaweza kama ikibidi kutumia kiasi hicho.
 
Vipi maandalizi Kwa timu za wanawake..?...huwa hamchelewi kusema hamna bajeti ..
Kuna siku tulisaini mkataba wa sponsorship ya kombe la Taifa la wanawake,naamini hiyo taarifa uliiona kwenye media.
youth development programme tunayoiandaa itahusisha women football.
 
Back
Top Bottom