Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Habari zenú, niende moja kwa moja kwenye mada. Kutokana na kuwa mimi si mtaalamu kuna maswali najiuliza kuhusu kinachoendelea mashariki ya DRC lakini nakosa majibu. Naomba mwenye utaalamu/ ufahamu anisaidie kujibu.
1. Kwanini jumuiya ya Afrika mashariki ipo kimya na haikemei kile kinachofanywa na Kagame kule Congo? Yaani hata sisi Tz tunamualika Kagame kwenye sherehe za Uhuru ilihali tunajua anaua wakongomani.
2. Kwanini Tchisekedi anamuamini Kagame kiasi cha kwenda kufanya nae mazungumzo ya kusitisha vita. Kwanini Rais wa Congo bado anaenda kwenye meza ya mazungumzo ilihali mwenzie Kagame hana mpango wa kusitisha mauaji kule DRC?
3. Kwanini DRC haifungi mpaka wake na Kongo. Mfano Niger imefunga mpaka wake na Benin kwa sababu Bénin inatumiwa na Ufaransa kuwapa mafunzo magaidi . Niger imegoma kufungua mpaka zaidi ya mwaka sasa hadi Bénin iache kuwa chimbo la magaidi wa Ufaransa.Kwanini Kongo hawafanyi hivyo?
4. Kwanini DRC haiiondoi MINUSCO ambayo imeshindwa kuleta amani nchini Congo kwa kipindi cha miaka 25 waliyokaa hapo. Pia kuna tuhuma kwamba kazi ya MINUSCO ni kuhakikisha vita Kongo havikomi ,tuhuma za kuwafadhili waasi na vilevile kuwa kikwazo kwa majeshi ya Afrika yanayoenda kulinda amani kwa kuwapa masharti mfano msiue waasi lindeni raia, msitumie silaha nzitonzito, mara sijui kuwapa askari coordinates za uongo wakipiga hawapati kitu n.k Mfano mwingine ni kwamba nchini Mali mashambulizi ya magaidi yalipungua pale kikosi cha Umoja wa Mataifa kilipofukuzwa.
Baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi, kitu cha kwanza alichofanya kiongozi wa kijeshi wa Mali ni kuondoa hicho kikosi cha Umoja wa Mataifa. Na baada ya kuwaondoa ghafla magaidi wakawa kama wamelegea . Jeshi la Mali likawaua balaa.
5.Je haiwezekani DRC kuhamishia jeshi lake hapo mashariki Ili kuwachakakaza hao M23 kama ambavyo wanajeshi wa Tanzania walihamia Mtwara enzi zile za wale magaidi kutoka Msumbiji waliokuwa wanafadhiliwa na Ufaransa . Ina maana Kongo hawawezi kupigana na hao M23 wakawapelekea moto kwelikweli?
6. Umoja wa Ulaya umeingia mkataba na Rwanda kununua madini ya wizi kutoka Congo, Kwanini Congo haijavunja uhusiano wake wa kidiplomasia na umoja wa Ulaya? Kwanini hawajamfukuza balozi wa EU nchini DRC?
7. Je Kagame anaidharau Kongo? Mfano hapo Kagera kuna mahali pana madini ya Cobalt hayajaanza hata kuchimbwa bado. Kwa tarifa nilizonazo ni kwamba maandalizi ya kujenga mgodi na kuanza kuyachimba yameshaanza. Lakini ukitazama hilo eneo lenye madini ni sehemu ya kawaida hata hapajaendelea bado.Nawaza mbona Kagame hajawahi kutuma hao M23 wake wakachote hiyo Cobalt ya bure kama wanavyoenda kuchota Cobalt huko Kongo?
Nadhani anajua watanzania hatutavumilia kuona wenzetu Kagera wanauwawa na M23 , anajua tutashusha kipondo. Lakini bila wasiwasi anawatuma M23 huko Kongo, ina maana anadharau jeshi la Kongo na anaona hawatamfanya chochote?
8.Siwaoni raia wa Kongo angalau wakiandamana kupinga hayo mauaji ya wakongo wenzao. Natamani nione wakongo wanaoishi Kinshasa,Lubumbashi n.k angalau wakiandamana kupinga kinachofanywa na Rwanda lakini naona wako kimya tu. Mfano, Raia wa Niger waliposikia ECOWAS imeidhinisha wavamiwe mwaka jana walienda kujaza barabara za mji mkuu kupinga uvamizi wa ECOWAS.
Wengine waliamka alfajiri kwenda kujiandikisha kujitolea kupigana. Kuna video niliona misururu ya vijana wadogo wa Niger wamesindikizwa na wazazi wao kujiandikisha kupigana, mbona sioni Kongo angalau wanaandamana tu.
9. Je hali ikiendelea hivi tutarajie vita kati ya Rwanda na Kongo?
Asanteni