Maswali ya Muungano yanayokosa majibu ya kweli kwa vijana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Maswali ya Muungano ambayo vijana wetu wa sasa wanakosa majibu yanayowatosheleza kutoka kwa wazazi wao ni haya:

1. Kwanini Tanganyika haipo lakini Zanzibar ipo?
2. Kwanini kuna Rais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar lakini hakuna Rais wa Tanganyika?

3. Kwanini Zanzibar wana ligi yao na hawamo kwenye ligi Tanzania?
4. Kwani Zanzibar wana bendera na wimbo wao wa taifa?

5. Kwanini kuna vitambulisho vya wazanzibar?

Haya ni baadhi ya mambo ya wazi ambayo vijana wa leo ni rahisi sana kuyaona kwa macho yao ya nyama.

Hakuna mtu anaewapa majibu sahihi ya maswali haya, labda ndio maana elimu ya muungano haifundishwi kwa vijana wetu mashuleni kwakuwa hakuna majibu ya wazi wa majibu haya.

Inawezekana Zanzibar iko kwenye muungano kwasababu ambazo hata vijana wa Zanzibar hawazijui kwa uwazi.

Inaonekana kuwa sababu kuu ya muungano ni usalama tu na sio kitu kingine. Tuliungana kwa kumuogapa Sultani, Mreno na Makaburu baaasi labda ndiyo maana muungano huu umedumu mpaka leo. Jeshi ndilo linaloulinda muungano wetu.
 
Kuna mbunge mmoja tu aliyekuwa na uthubutu wa kuhoji mambo ya muungano, Ally Kessy, sijui yupo wapi masikini.
 
Hakuna mtu mwenye ubavu wa kutoa elimu ya Muungano kwa vijana, maana muungano una maswali yasiyotakiwa kupewa majibu ya ukweli.

Tafakari tu ni kwanini haya yafuatayo yalifanyika:

1. Kwanini Mzee Karume alikubali muungano muda mfupi tu baada ya mapinduzi.

2. Kwanini Karume alikubari muungano kwenye mambo machache tu baaasi, sio yote.
3. Kwanini Nyerere harakaharaka aliifuta serikali ya Tanganyika.

4. Kwanini Karume alikataa Azimio la Arusha

5. Kwanini Nyerere alitangaza chama kushika hatamu muda mfupi tu baada ya ASP na TANU kuungana

6. Kwanini Aboud Jumbe aliachishwa Urais wa Zanzibar.
 
Zanzibar ina katiba yao iko wapi katiba ya wadanganyika?
 
Maswali ya Muungano ambayo vijana wetu wa sasa wanakosa majibu yanayowatosheleza kutoka kwa wazazi wao ni haya:

1. Kwanini Tanganyika haipo lakini Zanzibar ipo?
2. Kwanini kuna Rais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar lakini hakuna Rais wa Tanganyika?

3. Kwanini Zanzibar wana ligi yao na hawamo kwenye ligi Tanzania?
4. Kwani Zanzibar wana bendera na wimbo wao wa taifa?

5. Kwanini kuna vitambulisho vya wazanzibar?

Haya ni baadhi ya mambo ya wazi ambayo vijana wa leo ni rahisi sana kuyaona kwa macho yao ya nyama.

Hakuna mtu anaewapa majibu sahihi ya maswali haya, labda ndio maana elimu ya muungano haifundishwi kwa vijana wetu mashuleni kwakuwa hakuna majibu ya wazi wa majibu haya.

Inawezekana Zanzibar iko kwenye muungano kwasababu ambazo hata vijana wa Zanzibar hawazijui kwa uwazi.

Inaonekana kuwa sababu kuu ya muungano ni usalama tu na sio kitu kingine. Tuliungana kwa kumuogapa Sultani, Mreno na Makaburu baaasi labda ndiyo maana muungano huu umedumu mpaka leo. Jeshi ndilo linaloulinda muungano wetu.
Watanganyika wamedanganyika kabisaaa, wameuza nchi eti kwa gharama ya usalama wao, Kiufupi bila Zanzibar salama katu Tanganyika isingekuwa salama
 
Back
Top Bottom