MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Watanzania wengi hukerwa sana pale wanaskia mgeni amepewa wadhifa ndani ya nchi yao, lakini wengi hawataki kukabiliana na ukweli au kujiuliza maswali ya msingi.
Nakumbuka jitihada za kupata kibali cha kazi na cha makazi (work and residential permits) Tanzania, kwanza kabla upate cha makazi inabidi ufuate cha kazi ambacho kinatolewa na wizara ya kazi na ajira. Wale jamaa wanahoji balaa, hawatoi tu kibali moja kwa moja, wanatathmini umuhimu wako, na kwanini hiyo nafasi isipewe Mtanzania, imekuaje au iweje wewe mgeni upewe hiyo nafasi.
Kampuni ya Kitanzania inayokualika inabidi kutolea maelezo na kushawishi sana, na kuweka viambatanisho vingi tu ili kuwaridhisha jamaa kwamba kuna umuhimu mkubwa kwanini wewe upewe kibali. Na hayataishia hapo tu, wanatuma maafisa wao kwenda kwenye kampuni husika kufanya uchunguzi wa kina, kuna nini huko cha maana ambacho kampuni inakifanya hadi aalikwe Mkenya au Mhindi na ambacho mamilioni ya Watanzania walio barabarani wakitafuta ajira hawakiwezi.
Baada ya hapo wanaandaa ripoti, ambayo pia inachukua muda sana kufanyiwa kazi. Wakimaliza na kuridhika kwamba wamekukubali, msala unahamishwa kwenda kwa uhamiaji, na wao pia wanaanza mchakato ambao pia umejaa maswali lukuki, pia na wao wanatembelea kampuni husika. Wanauliza kila aina ya maswali na kutathimini umuhimu wako kwenye nchi hiyo. Yaani ni shughuli ndefu, ambayo inaweza ikakwama kwenye hatua yoyote na ombi lako likapigwa chini.
Kumbuka yote hayo utalipia ada, tena hela ndefu. Yakikamilika yote, sasa kampuni inaanza shughuli za kukulipia nauli ya ndege, kukulipia makazi na kugharamia utakacho kula na kunywa na kuishi, na pia mshahara wako.
Sasa swali la msingi, kwanini kampuni inayomilikiwa na Watanzania iingie gharama zote hizi kumfuata Mhindi, Mkenya, Mchina au raia wa Afrika Kusini na kuwaacha mamilioni ya Watanzania na vyeti vyao wakizunguka na kutafuta ajira. Mnafaa kujiuliza hili swali kwenye kila jukwaa, kwenye kila aina ya mahojiano, na kubaini nini cha kuboresha kwenye nguvu kazi zenu na raslimali watu.
Na pia makampuni yanayomilikiwa na wageni kama vile Vodacom, kwanini wasiangalie ndani ya nchi kwanza ilibidi wafuate nchi jirani, maana kwa kweli lazima wawe makini kwa sababu mkurungezi wanayemleta lazima awahakikishie kwamba
- Kampuni itaendelea kuongeza faida kwenye P&L
- Ataanzisha mikakati na kuisimamia
- Atawajibika kwenye bodi ya wakurungezi
- Atasimamia na kuhakikisha utenda kazi wa waajiriwa zaidi ya 500
- Ataendesha vikao vya washika dau na kuwaridhisha kwenye kila hatua na pia vikao vya mwaka (AGM)
- Atahakikisha sheria za nchi zinazngatiwa na kukwepa mahakama ama uingiliwaji na serikali
- Uimara wa kampuni kwenye soko la hisa
- Bidhaa kama mpesa zitaendelea kuimarika kwenye mazingira yenye ushindani mkubwa
- Kuwezesha kampuni kutanua na kusambaa kote kote huku wakiwa makini kwa kila hatua
- Kuwathibiti matapeli kila siku na pia dhidi ya wahujumu hata walio ndani ya kampuni
Yaani orodha ya majukumu ni ndefu ambayo sio kila mtu atatamani kuvaa hivyo viatu.
Hivyo, nawasilisha tu kama kitu mnachofaa kukijadili kwa kina bila kulea machungu, wivu na chuki