Mbepo yamba
JF-Expert Member
- Aug 5, 2012
- 1,262
- 1,773
1. Kwa mujibu wa maandiko, Mungu alimpa amri Adam na Hawa wasile matunda ya mti wa katikati. Hakuwaambia kuwa ni wa ujuzi wa mema na mabaya na wala hakuwaambia ungewafungua macho. Shetani yeye akawaambia watu hizo dondoo kuuhusu huo mti na matunda yake. Je, Shetani alisema ukweli?
2. Mungu alimuumba mwanadamu ‘kwa ukamilifu’. Kama kulikuwa na ukamilifu ikawaje udhaifu wa dhambi ukawa ndani ya mwanadamu?
Ikiwa mwanadamu aliumbwa na udhaifu, na udhaifu ukapelekea yeye kuanguka dhambini. Kwa nini Mungu amuadhibu huyu mwanadamu ikiwa yeye Mungu ndiye aliyeachilia udhaifu kwa mwanadamu?
3. Kuhusu Farao. Maandiko yako wazi kuwa alikubali mara kadhaa kuwaachia wana wa Israeli waende lakini Mungu akaugeuza moyo wa Farao hata akawazuia kila mara. Hatimaye akawaadhibu wamisri kwa misiba.
Sasa kosa la wamisri hapo lilikuwa wapi na ikiwa walikubali kuwaachia waisraeli waende?