Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimepokea taarifa kuhusu tukio lililotokea tarehe 8 September 2026 katika eneo la Lugalako, Kinondoni, Dar es Salaam, linalomhusisha Dkt. Conrad Agonza Kahyoza ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila na Askari wa Ulinzi wa Barabarani mwenye namba F.8886 SGT.
Baada ya tukio hilo, uongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) umefanya mazungumzo na Jeshi la Polisi Tanzania, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muro, na kufahamishwa kwamba Dkt. Agonza alipata majeraha na kupelekwa haraka hospitalini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya dharura na hali yake imeimarika. Kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay na taratibu za kisheria zinaendelea.
Chama cha Madaktari Tanzania kinamsisitizia yafuatayo:
Kwanza: kwa kuzingatia hali ya Dkt. Agonza na mahitaji yake ya matibabu, MAT inaendelea kufuatilia kwa karibu ustawi wake na kuhakikisha kwamba anapata huduma stahiki za matibabu kwa wakati wote atakapohitaji.
Pili: Uongozi wa MAT kupitia wanasheria wake unaendelea kufuatilia taratibu za kisheria kuhakikisha anapata msaada wa kisheria wa haraka ikiwa ni pamoja na dhamana.
Tatu: MAT kwa kushirikiana na muajiri wa Dkt. Agonza (Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila) pamoja na familia itaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kulingana na mwenendo wa shauri hili.
Soma Pia: Polisi: Conrad Agonza Kayoza anashikiliwa kwa kumshambulia kwa ngumi na mateke Askari wa Usalama barabarani
Chama cha Madaktari Tanzania kinaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu na kitaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa mamlaka husika, huku kikilinda maslahi, utu na haki za mwanachama wake kwa mujibu wa sheria.