Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,958
- 70,721
Nimepitia nyuzi nyingi sana naona wanazi wa kwenda zake wakianza kumponda mama Samia kwa kufungua mipaka ma Kenya.
Hoja zao zilizokufa:
1. Ooh Kenya iko juu kiuchumi watatuzidi tukiwapa gesi
2. Ooh Kenya wana viwanda vingi vyetu vitakufa kisoko.
3. Ooh Kenya watafaidika kuliko sisi n.k.
Sasa kama mtanzania unaogopa changamoto katika maisha utajijuaje kama una akili? Mama kashafungua mipaka na uadui uliowekwa na mwenda zake.
Kama hauko tayari kuzidiwa na Kenya kiuchumi unachukua hatua gani? Ww endelea kulia lia wenzio tayari washaona fursa.
Katika malalamiko hayo huwezi kukuta mchaga analalamika ujinga kama huo sababu tayari ni fursa.
Asante mama Samia kwa kurahisisha biashara, naona unatembelea njia ya JK
Mtembea bure si sawa na mkaa bure jifungieni nchini mwenu wenzenu tayari wanaranda kupiga pesa.
Naunga hoja kwa nguvu zote! Tuamke .how come unamhofia binadamu mwenzako? Aisee hili taifa lina laana sana