MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
- Thread starter
- #21
Kwa hili la Niger,Niko tayari kukupinga MK254 Tena hadharani.
Tena ujue Mimi ni mkenya mwenzako.
Thubutu...mamaeeé!💪
Tutatoka vijana Africa nzima Hadi Arabuni kusimama na waafrika wenzetu waNiger.
Usikurupuke bro, ninachopinga ni utawala wa kijeshi, mengine hayo unayobwatuka mara Mfaransa sijui Muarabu, mara Ukenya siko huko, utawala upokezwe kwa raia na nchi iongozwe kwa misingi ya kidemokrasia.
Hata Kenya, licha ya ninavyochukizwa na utawala kwenye baadhi ya namna wanavyoboronga, ila siwezi kutamani nchi ichukuliwe na kutawaliwa na wanajeshi, tulumbane kama raia, tubishane, tusukumane mpaka kieleweke ila tubaki humu humu uraiani.
Wanajeshi wakiichukua nchi huwa ni balaa nyingine, kwanza wanajeshi wetu Afrika ni mafisadi kupita maelezo, bajeti zao hazijadiliwi wanajificha kwenye kivuli cha eti ni masuala ya usalama na nyeti pia, wanaiba hela sana wale, sasa wakichukua uongozi wataiba bila kukosolewa, na pia wenyewe watapigania uongozi maana tayari wameonja, utakuta kanali sijui brigedia mara generali wanapinduana.