Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Uswisi inaratajia kuwaalika washiriki zaidi ya 160 kutoka mataifa mbalimbali katika mkutano utakaolenga kuleta amani na upatanishi wa Ukraine na Russia.
Mkutano huo unatarajia kufanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 15 hadi 16 katika Hoteli ya Bürgenstock Hotel nchini humo.Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mamlaka ya Mambo ya Nje ya Uswisi ilieleza kuwa waalikwa hao ni wanachama kutoka mataifa saba yenye nguvu kubwa ya uchumi (G7), G20, Umoja wa Ulaya (EU) Nchi wanachama wa Brics isipokuwa Russia.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waalikwa wengine ni mashirika mbambali ya kimataifa na kidini.
“Hii itakuwa ni jitihada za tano kunurusu hali ya amani kati ya Russia na Ukraine. Wageni watatoka pia mataifa ya Afrika Kusini, Misri, Senegal, Congo-Brazzaville, Comoro, Zambia na Uganda ambao wataongozwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa,” ilieleza taarifa hiyo.