ha ha ha ha ha ha ha ha! Hii inaitwa too much logic my friend sio kwamba sikuungi mkono ajenda yako ila ni kwamba hizi inshu za kupeana solution za maisha zimekuwa kama ndio chanzo cha kufeli kwenyewe. Kwa nijuavyo mimi kufanikiwa katika haya maisha ni juhudi ya mtu binafsi kufanya kile ambacho anakipawa nacho sana tu.......leo kuna watu kama akina joti na mpoki kupitia vituko wameweza kujenga maisha na kupata mianya ya kutajirika, kuna watu kupitia urembo wapo juu, wengine ni hata kilimo cha bangi kimewatoa, sasa sidhani tabia tuu ndio msingi wa kufanikiwa ila na mazingira yanayokusapoti nayo ni muhimu sana. Si wafahamu kuwa kugeza geza humfanya mtu kupata ukichaa wa muda. Miaka ya nyuma watu waliamini kusoma ndio ufunguo wa utajiri leo wasomi ndio wanaofeli maisha kulingana na mfumo wa elimu uliopo. Maisha hayana formula, unaweza ukawa unatumia social media kwa saa zaidi ya 10 but muda wote huo kazi zingine zinakwenda freshi na unaingiza kipato.........mimi hapa unavyoniona napenda sana kula movie na kucheza playstation michezo ya magari na mission na adventure lakini nina kipato cha wastani wa 60,000+ kwa siku na kinaongezeka maana nafanya uwekezaji mdogo miradi ya migodi na cement nimewaachia akina dangote na babaaa kylin, nafanya hivi kwasababu hata MUNGU baba yetu hapendi atuone tukiishi kwa sheria ngumu za kibinadamu wakati anapenda tuishi kwa amani na utulivu. Relax bro, haya maisha hayataki stress.........pupa za nini utajiri unaweza kukujia kwa kasi ndani ya mwaka m'moja cha muhimu ni kujua nini kimekuleta sasa haya mambo ya kuishi kama zombie eti unataka kuwa tajiri basi unajiwekea makanuniiiiii na masheria utadhani roboti au msabato au swala tano kama ustaadhi ally inakuwa ni kama unajifunga kuishi. Ishi kwa utulivu na amani, fanya unachojisikia, kuwa na adabu ya pesa heshimu kazi za wengine, timiza wajibu, jiwekee mipaka itakayokuzuia kufanya uzembe utakaokurudisha nyuma, tenga muda mwingi sana wa kuwa katika dunia yako, jiwekee malengo, punguza stress za kijinga, mfano unataka kuwa na demu ambaye anatamaa ya pesa we unafosi kumtaka, unakopa kiasi cha pesa ambacho hujui utarejeshaje, unakaa na watu ambao hawakukubali au ambao hamuendani kabisa kwa namna zote hii yote ni kutafuta stress.
Hebu nunua t.v set ya size unayotaka, jenga nyumba hata ya room moja piga fensi ili watu wasikuletee mazoea, cheki movie, sikiliza muziki, jiulize unataka kitu gani ndani ya wakati gani iwe mwanamke, mtoto, gari, nyumba, sim, biashara, then evaluate kiasi cha pesa kinachotakiwa ili upate hiyo kitu, then tafuta namna yako ya kupata pesa ya kupata hiyo kitu MUNGU hatakutupa kwa maana anapenda watu wasiocopy formula za binadamu wengine wakati yeye katuumba sawa kabisa kwa kufanana sasa kwanini uchukue kanuni sijui za dangote, sijui poor dad rich dad, sijui billgates, sijui Mengi, sijui Bakhressa, huo ni uzembe katika kuishi. Live your way define your life acha kuiga formula za wengine kudefine maisha yako sisi binadamu sio maroboti kusema tufanane operating system.
So asante kwa somo zuri rafiki ila sitapokea, nasita na ninakataa kufanana na kila mtu nataka kila mtu ajue yeye ni zawadi katika hii dunia, aliletwa kuja kuleta kitu kipya kwa wengine hebu tujifunze kuwa tofauti. Ni hayo tu naomba kuwasilisha mchango wangu katika ,mada hii.