Matajiri kumi Tanzania ni hawa


Ksij sio kampuni bali ni dini...huyo sabodo kama sikosei ndio miliki wa wa Colosseum apprtmnt opost golden tulip
 
Hii listi ni wafanyabiashara wenye mifumo rasmi ya kupata fedha na zinapitia benki bila kificho. Kama wangeweka pia orodha ya waajiriwa au wanasiasa waliopata fedha za wizi lazima wangekuwepo wengi

Hilo nakubaliana na wewe 100%. Kuna jamaa anaitwa Zakaria mwenye kiwanda cha korie na impoter wa sukari ya matumizi na viwandani. Huyo jamaa wamuache kama alivyo. Hao akina manji na mo wanasubiri sana.
 
Hakuna huu ni upuuzi..haiwezekani diamond akosekane kwenye hii listi
 

Hiyo list mbona imeshapitwa na wakati jombaaaa.Mwaka 2014 Rostam Aziz alikuwa wa kwanza kwa utajiri wa $1bn,Akifuatiwa na Bakhresa na Dewji halafu Mengi na Ali Mafuruki.Hebu fuatilia vizuri kwenye forbes.
Mwaka huu Mohamed Dewji ametajwa kuwa kijana mwenye pesa mingi barani Afrika na amefikia utajiri wenye thamani $1bn.
Usikurupuke fuatilia vizuri hiyo orodha ni ya zamani sana.
 
Na mimi ngoja nipigane na maisha nikifika miaka 50 nione account yangu inasoma dola ngapi
 

Afu MO katika utajiri wake Takribani zaidi Us$400 million amekopa mwaka jana na mwaka huu, sasa sijui na debts zinahesabika kama sehemu ya utajiri au ni liabilities zile?
 
Nakumbuka 2005 wakati JK akizunguka kufanya campaign aliahidi kutengeneza mabilionea watano akiingia madarakani...sijui km hao wamo kwny hiyo orodha ya matajiri 10!
 
Umegusa ukweli kwa 100%. Hizi nywele ngumu ni shida. Yaani mtu akishapata mali anafurahi sana kuona ndugu zake wakiteseka ,kujikomba, kujinyenyekesha kwake wakiomba msaada. Yeye kwake ni fahari....

Sasa kama hao ndugu hawakuwa na ustaarabu wa kukutambua ulipokuwa kwenye struggle ya kutafuta, kukukwepa, kukusengenya na kukutenga, kuna haja gani ya wewe kuwasaidia pale unapofanikiwa?
Watu weusi tuna matatizo mengi. Kuna watu wako tayari wakeshe nje kwenye baridi, washinde bila kula ili mradi tu wahakikishe fulani hafanikiwi na kibaya zaidi ukute ni ndugu yao, ustaarabu wa kusaidiana tuwaachie wenye utamaduni huo. Mbona hata Wazungu hawana time na mambo ya kupigana tafu kijingajinga kwa vile tu kuna undugu?
 
Vipi kuhusu Mengi mkuu

Yupo vizuri sana si wa kubeza huyo jamaa.Handeni Gold inampa pesa mingi tu kutokana na dhahabu na Bonite Bottlers Ltd inamuingiza noti nzuri.Kuingia tano bora si jambo dogo.Mfuatilie kwenye forbes magazine utapata taarifa zake vizuri.
 
tuna kitu cha kujifunza toka kwa hawa jamaa, waarabu shule ndogo lakini wanajua kujipanga ki maisha.
 

Asante mzee lakini nafikiri umekosea kidogo Mohamed Dewji hakutajwa kuwa tajiri mwenye pesa nyingi barani Afrika bali ametajwa kuwa jeje ni tajiri kijana katika bara la Afrika
 

Ili uwe na amani na furaha ktk maisha yako ucwaweke kwenye mawazo hao
 
Asante mzee lakini nafikiri imekosea kidog Mohamed Dewji hakutajwa kuwa tajiri mwenye pesa nyingi barani Afrika bali ametajwa kuwa jeje ni tajiri kijana katika bara la Afrika

Ukitaka upate taarifa nzuri na zilizo sahihi usitumie vyanzo kama bongoland na hizi blogspot za udaku watakupoteza.We nenda zako Forbes utapata orodha nzuri sana kwani taarifa hizo huandaliwa na watu wenye weledi wa uchumi na fedha.
Hivyo viwango vilivyotajwa vya utajiri wa hao watu hapo juu vyote si sahihi na hata matajiri wenyewe walivikana.
 
Ili uwe na amani na furaha ktk maisha yako ucwaweke kwenye mawazo hao

Mkuu nafikiri mawazo kama haya ndio yanafanya sisi watanzania wenye asili ya Kiafrika tujiulize na tutafakari wapi tumekosea,nchi yetu utajiri wete lakini matajiri wanakwa wageni,,,

Sina ubaya kwa watanzania wenye na asili isyokuwa ya kiafrika kuwa matajiri na kutajirika na rasilimali zilizokuwepo nchini...lakini kila siku huwa najiuliza kosa liko wapi kiasi mambcho wenzetu wanatuacha kiasi hiki,tukilijua kosa ndio tunaweza kuwa sambamba nao .....

naunga mkono hoja 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…