The mountain lion
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 1,153
- 418
Mkuu nafikiri mawazo kama haya ndio yanafanya sisi watanzania wenye asili ya Kiafrika tujiulize na tutafakari wapi tumekosea,nchi yetu utajiri wete lakini matajiri wanakwa wageni,,,
Sina ubaya kwa watanzania wenye na asili isyokuwa ya kiafrika kuwa matajiri na kutajirika na rasilimali zilizokuwepo nchini...lakini kila siku huwa najiuliza kosa liko wapi kiasi mambcho wenzetu wanatuacha kiasi hiki,tukilijua kosa ndio tunaweza kuwa sambamba nao .....
naunga mkono hoja 🙂
Kosa kubwa la kwanza ni kutokuwa na utamaduni wa kufanya biashara.Idadi kubwa inapenda kutafuta ajira na akiipata basi yeye anaridhika.Wapo watu wenye vipato vikubwa lakini hawataki kabisa kuwekeza wenzetu wao wamejikita kwenye biashara na ndo zinawafanya wawe matajiri.
Wachaga ni mfano mzuri sana wamejikita kwenye biashara angalia jinsi walivyofanikiwa sana.
Hawa wa-asia walipokonywa mali zao nyingi tu wakati wa Nyerere lakini walijipanga upya wakajikita kwenye biashara na sasa ni matajiri tena.
Huu sio wakati wa kujilaumu ni wakati wa kuanza kujifunza matajiri wanafanyaje mpaka wanafika hapo na siri kubwa ni hiyo.
Lazima tuwe na utamaduni wa kuwekeza na kufanya biashara ndo tutakuwa na pesa mingi tuking'ang'ania miajira tutabaki kuwa watumwa kwenye nchi yetu wenyewe.