Matajiri wa Qatar kuinunua Man United kwa £6b ambayo ni sawa na Tshs trilioni 16.9

Matajiri wa Qatar kuinunua Man United kwa £6b ambayo ni sawa na Tshs trilioni 16.9

Kaka Yaoh

Senior Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
190
Reaction score
361
Kikundi cha wawekezaji kutoka Qatar wapo tayari kutoa ofa ya kuinunua Manchester United, ambayo haitowezwa kufikiwa na matajiri wengine wanaotaka kuinunua timu hiyo.

Familiya ya Glazer, ambao ndio wa miliki wa klabu hiyo wanataka kuiuza kablu hiyo katikati mwa mwezi huu wa February.

Mtandao wa The Daily Mail umeripoti kuwa kikundi cha matajiri kutoka Qatar wamejiandaa kutoa ofa kubwa ya £6b ambayo ni sawa na Tshs 16,962,270,000,000 katika siku siyo nyingi na wapo tayari kumpa kocha Erik ten Hag fungu kubwa la usajili mara tu watakapo nunua klabu hiyo.

Kikundi cha matajiri kutoka Qatar sio pekee wanaotaka kuinunua klabu hiyo hata tajiri mkubwa kutaka Uingereza Sir Jim Ratcliffe ameshatangaza hadharani kuwa yupo tayari kuinunua klabu hiyo.
 
Kwa dau hilo, ni wazi wanabeba timu yao.
 
Tafuta mtu akufunze hesabu ? Yaani £6b iwe billion mia 8 za kitanzania???
 
Kikundi cha wawekezaji kutoka Qatar wapo tayari kutoa ofa ya kuinunua Manchester United, ambayo haitowezwa kufikiwa na matajiri wengine wanaotaka kuinunua timu hiyo...
Mkuu tangu lini Man U ikauzwa kwa Bilioni 800 za kitanzania? hiyo hata mo si anaweza kununua man u na chelsea kabisa na Arsenal. Umekosea kufanya hesabu Pound 6 Billion ni Tsh 16,959,311,880,051 za madafu
 
Back
Top Bottom