Well said Mkuu
Naanza kuhisi huo mfumo umekuwa so strong kiasi kwamba hata raisi akiwa na nia ya kuuvunja anaweza kupata matatizo yeye - kiasi kwamba anakuwa na option moja tu - to join them. Ni lazima kwamba huo mfumo kwa sasa unafanya kazi kama kaji-association, kaji-mafia ka viongozi wa serikali na wale waliokuwa serikalini huko nyuma, na nimesema katika thread nyingine, inawezekana kabisa ndio walio nyuma ya utekaji na uuaji, wakifanya hivyo sio kama serikali, bali kwa kutumia vyombo vya serikali isivyo rasmi. Nasikia hata wana mtandao wao wa WhatsApp.
Ndio maana tetesi kwamba Magufuli alihujumiwa na kuuawa zinakuwa na mshiko, kwamba alijaribu kuuvunja huo mfumo na akazidiwa. Mtandao kama huo kama ni kweli, sioni mtu kama raisi Samia akiwa na uwezo wa kuuvunja. It is too big for her.