Matajiri wana mfumo wa kuvuta hela na maskini wana mfumo wa kuvuta majungu

Matajiri wana mfumo wa kuvuta hela na maskini wana mfumo wa kuvuta majungu

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
MATAJIRI WANA MFUMO WA KUVUTA HELA NA MASKINI WANA MFUMO WA KUVUTA MAJUNGU.

Maskini anajua wapi apate umbea wa moto yaani kama unataka umbea kwake utaupata ila tajiri anajua wapi kuna mchongo wa pesa yaani anajua nani amtafute apate mchongo wa pesa.

Hapa nazungumzia maskini wa asili na aliyeridhika kubaki kwenye mfumo wa kimaskini ambaye anaamini utajiri ni dhambi , huyu muda wake mwingi utamkuta kwenye umbea kuutafuta na kusambaza.

Kuwa kwenye mfumo wa kimaskini/kitajiri sio bahati mbaya lazima kuna namna uliingia kama sio wewe basi umeingizwa na familia yako hivyo kama upo kwenye mfumo wa kimaskini basi juhudi za kutoka huku zinakuhusu.

Toka taratibu kwenye huo mfumo na anza na marafiki kama rafiki zako muda mwingi wanakupa tu umbea na majungu jua tayari upo kwenye mfumo wa kimaskini na utakuwa tajiri wa majungu hivyo kata huo mfumo.

Matajiri wanamfumo wa michongo ya pesa ndio maana ukiwa maskini wa kwenye mfumo utashuhudia matajiri wakipata fursa na wewe ukikosa kwa sababu upo nje ya mfumo.

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Instagram@fikia Ndoto Zako
 
Back
Top Bottom