Matajiri wanaoishi Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na kwingine wanatumia wamasai wawafugie maelfu ya ngombe Ngorongoro, sasa wanafadhili maandamano

Hivi inaingia akilini kwamba mtu ana ng'ombe wake Mwanza, Dar au Mara na Arusha awapeleke ng'ombe wake hao akamkabidhi Mmasai asiyemfahamu wala ili amchungie? Ningeelewa kama huyo tajiri angemwajiri huyo Mmasai amchungie ng'ombe wake hapo hapo aishipo yeye tajiri; sawa na watu wa Dar walivyokuwa wakiajiri Masai walinde makazi yao.
 
Nina wasiwasi ata jinsia yako huijui.
 
Hii ndo propaganda mliyopewa kupush Kwa 7000 Kwa siku? Mbona ya kitoto? Nani aliwapa Wamasai Ng'ombe wa kuingiza Ngorongoro mwaka 1953?
 
Hili jambo dogo sana serikali iwape kwanza hati miliki ya ng'ombe wote hao wamasai wanaoandamana na iwalinde asitokee yeyote akasema hizo ng'ombe sio za h8yo mwandamaji

Kuna taarifa wakenya wengi matajiri wana ng'ombe zao ngorongoro.Serikali italicised zote ikabidhi masai hao watanzania kama mtu ni mchunga ng'ombe tu apewe aondoke nao mvomero na serikali iwasaidie kuwakimbizia Mvomero

Na hao wachungaji wasiogope huu ndio wao wa kuvuna utajiri

Tuone kitakachotokea
 
ukweli mtupu dah 🐒
 
Uwongo mtupu
 
Hiyo mifugo ambayo si ya wana Ngorongoro kama ipo si wakamatwe.
 
Hii ndo propaganda mliyopewa kupush Kwa 7000 Kwa siku? Mbona ya kitoto? Nani aliwapa Wamasai Ng'ombe wa kuingiza Ngorongoro mwaka 1953?
Hao wa 1953 wote wameondoka, wako Msomera, humo kwa sasa kuna ngombe za Mbowe na genge laje, pamoja na matajiri wengine
 
chiembe we bonge la mjinga yaani hata kama huu unalipwa kuandika huu upuuzi hujisikia vibaya? Kwann uwahamishe watu maeneo yao ya asili kwa faida ipi?
Uwe unajisikia hata aibu halafu kama unalipwa kuandika hizi propaganda acha kupokea hizo pesa ni laana kubwa kwa sababu hili linapita sijui utakuwa na hoja gani? Adui mkubwa wa hii nchi ni Serikali ya Chama cha MapinduZi na sio sababu za kijinga mnazohangaika kuziandika humu. Kama kweli Wewe una ubavu toka humu nenda umasaini kaitishe mkutano wa hadhara uyaseme hadharani haya unayoyaandika humu
 
Na ndio maana ukikuta sisi wananchi tunaisema serikali usivundumke tu na kuanza kuishambulia ....

Kuna watu wanataka kuziangusha serikali kwa kule kutaka KUZISUJUDISHA kwa maslahi yao....hao hawajali amani na utulivu wa wengine.....

Ukimsoma Mao Tse Tung unaona mengi ya fikra zake tunduzi.....

UBEBERU NA MABEBERU wako kila mbari ,kila uzao ,kila taifa....

Chambilecho baba wa taifa ,Ubepari ni UNYAMA....

Ona wanavyoweza kununua watu mitandaoni....ona wanavyolobby mpaka wanaharakati wa nje na vyombo vyao.....

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa serikali yetu inakandamiza raia wake....

Hilo halipo....

Na si kweli....

NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY AS IT IS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE [emoji7]

#Serikali mbili za JMT Milele dumu ,aaamin aaamin[emoji7]
 
Kuna kipindi Jamiiforrum ilikuwa ukipost uzi kama huu unafutwa chap kwa haraka. Lakini kwa Jamii forum ya leo hii huu uzi utabaki na kukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…