ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,651
- 2,790
"TRUMP ASITISHA MISAADA YA NJE KWA SIKU TISINI,
WHO YAAHA KUTAFUTA NJIA YAKUJIKWAMUA KWA KITISHO CHA TRUMP
" Anaekulisha anakutawala anae kuvisha anataka umnyenyekee alisema Castro badae Sankara Kisha Traole Sasa ni wakati wawaafrika kuamka kwenye usingizi. Mzito uliojaa ndoto butu zakuitegemea misaada ya kigeni, swali ni kwamba je tutaendelea Kuwa wanyonge mpaka lini je tutaendelea kutegemea cha ndugu mpaka lini kwanini tusiumbe chetu Trump anatukumbusha wajibu wetu tunapaswa kuikimbia mifumo ya Kuwa omba omba tutumie rasilimali zetu kuitishia Dunia kwa matokeo chanya wakati tunapoteza muda kuyafikilia mahamuzi ya Trump tunapaswa tuichukue kama fursa ya kutoka ktk udhariri wa kigeni
Afrika Ina ardhi yenye rutuba lakini tunategemea misaada ya chakula kutoka nje tuna Rasilimaliwatu vyanzo vya maji vya kutosha kwanini tuendelee Kuwa omba omba na watu wasio na maana wakati tumebarikiwa... Hii ni shime kwa serikali za Afrika kuhacha kuleta siasa kwenye vitu vya msingi Uwekezaji uliotukuka ndilo jibu lakuziinua nchi zetu "Mungu ameisha tubariki huu ni wakati wa kuchukua hatua
😥😥
MSIBA MKUBWA: waafrika kumshabikia Trump.
Rais Donald Trump ana mashabiki wengi Afrika pengine kuliko alio nao ndani ya nchi yake ya Amerika. Ziko sababu kadhaa na zote zinahizunisha:
1. Amesaini maagizo ya kirais (Executive orders) kutekeleza sheria kadhaa ambazo zililala muda mrefu bila kutekelezwa. Yaani sheria zilishindwa, rais Trump anatumia 4WD ili zitekelezwe!
2. Amediriki kugusa jambo la ushoga ambalo linaogopwa na wengi. Tukumbuke tunao mashoga wengi kabatini kuliko tunavyojifanya kupinga ushoga hadharani. Siku yaja tutaumbuka.
3. Ametamka mambo kadhaa kuzisema nchi kiafrika na uzembe wake. Wananchi wakashangilia; viongozi wakanuna. Mgawanyiko huu si dalili ya ugonjwa bali ugonjwa wenyewe.
4. Mashangilio ya Waafrika kwa Trump ni ushahidi wa kutamani ubabe na kuichoka demokrasia bandia. Waafrika wengi wanatamani makombo katika nchi huru kuliko keki katika demokrasia bandia. Kuna hatari ya watoto kuwasaidia majambazi kumuua baba!
5. Maagizo ya kirais (Executive orders) yana masharti makuu 3: Yawe yamepitishwa na bunge, hayapingani na katiba, na rais asiwe na maslahi binafsi. Yote matatu hayawezekani Afrika na kwa hiyo marais wetu wana nguvu kuliko mabunge, wana nguvu kuliko katiba, na rais kutokuwa na mgongano wa maslahi ni uzembe Afrika.
6. Rais wa pili anayeshabikiwa sana Afrika ni wa Burkina Faso ni Kapteni Ibrahim Traore. Aliongoza mapinduzi ya kijeshi mwaka 2022. Kushabikia rais aliyepindua serikali ni msiba kwa bara la Afrika. Tuna watoto wanatamani wazazi wafe ili waweze kupokea misaada ya watoto yatima kutoka wafadhili. Viongozi wangu mpo?
7. Tumeambiwa kuwa ili demokrasia na utawala bora vije kwetu Tanzania, sharti Yesu arudi! Yesu hapigi kura wala hapigiwi kura. Alirudi jana, mbona demokrasia na utawala bora hatuvioni? Mnatamani msichokijua, kikija mtakichukia.
8. Nimekuwa katika mikutano na majadiliano: Duseldolf, Wuppertal, Hamburg, Frankfurt, Wiesbaden, Davos, Bonn na Krefeld. Nimekutana na wajumbe toka Sweden, Italia, Marekani, Poland, Uswiss, Checkslovakia, Hungry, Belgium na Ujerumani. Kote siasa za mlengo wa kulia zimetamalaki. Vimelea vya Trump, Hitler, Stalin na Musolini vimechipuka. Huko nyumbani, JPM anaongoza kwenye kura za maoni. Ukweli si tusi na si sababu ya uadui. Anayelipenda taifa letu, akubali mjadala wa wazi. Kutekana, kutumbuana na kufukuzana havimzuii Trump kushabikiwa.
9. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Washauri wa mamlaka wanaolipwa kwa kushauri waendelee na kazi yao. Washauri wasiolipwa wasikilizwe. Wataliokoa bara letu dhidi ya bundi anayelinyemelea. Mama mwenye hekima, huonjea mchuzi kiganjani siyo kwa kijiko.
10. Watu tunao. Ardhi tunao. Siasa safi, nina mashaka. Uongozi bora, tuwaulize wapiga kura. Kwa nini hatuendelei? Trump tumewahi kuwa naye. Tulijuta. Plato tulikuwa naye, tunamuenzi bila kukumbuka yaliyotupata naye. Tatizo si mwanamme wala mwanamke. Msumari uliolemazwa na nyundo, hauwezi kunyoshwa na jiwe. Tusahau vyama, tuanze upya.
Januari kwaheri. Februari karibu, tusindane kupendana na kusalitiana 14/2.
PhD-Bagonza
✍🏿✍🏿✍🏿
Hii ni falsafa(FUMBO) gumu nani awezaye kulitegua? Afrika ni bara la wajinga linalioongozwa na wendawazimu. Mkuu nimesikitishwa na moja ya sheria ya kusitishwa kwa misaada iliyokuwa inapitia WHO kitengo kimojawapo ni dawa za kufubaza VVU maarufu kama ARV mimi sio mtumiaji lakini ni mtumiaji kwa njia nyingine kutokana na ndugu,jamaa na marafiki zangu kuwa watumiji/tegemezi wa ARV tutegemee watu kufa kwa hofu maana serikali za kiafrika hazitaweza kununua dawa hizi badara yake wataendelea kununua maV8 ili watawala waendelee kuishi peponi uku watawaliwa wakichalazwa wakiteswa na VVU.
Tutegemee kuona wagonjwa wa UKIMWI katika hali ya miaka ya 1980-1990.
Kwa upande mwingine kutokana na andiko lako nampongeza Trump kwa uwezo wake wa kuficha unafiki wa Wazungu kutaka Afrika isimame yenyewe kuliko kusimamia miguu bandia ya Wazungu hii ni fimbo kwa watawaliwa kuliko watawala ila inaweza kugeuka kuwachapa watawala kama watawaliwa wataamua kuitumia vizuri.
Kule kwetu wanasema "omuigo gwaindika akami kang 'embwa" iwe demokrasia iwe mapinduzi ya kijeshi au nguvu ya UMMA wananchi wakijua nguvu waliyonayo dhidi ya watawala majambazi najua Afrika itajitegemea tukichukua mfano wa Burkina Faso.
Maandiko aya ni chachu kwa watawaliwa kuchukua hatua kukomesha demokrasia uchwara zinazowafanya watawala kuishi kama wako paradiso uku watawaliwa(walipa kodi) wakiishi jehanamu kabla ya wakati (hukumu)
NB: Tunawataka kina Traole wengi ili kutimiza matamanio ya Trump Afrika.