Matambiko sio Ushetani

Matambiko sio Ushetani

Joined
Jun 26, 2015
Posts
55
Reaction score
62
Waafrika wengi, tuna dhana ya kufikili kua matambiko ni uwovu na ushetani.

Lakini kimsingi hakuna dini ambayo haifanyi matambiko, haijalishi iwe dini mbaya au ni dini nzuri.

Waafrika wakifanya matambiko, inachukulia kama ushetani, kutokana na kazi kubwa kubwa iliyo fanywa na wamissionary ku kandamiza tamaduni za jamii walizo zivamia .

Kwenda kwenye ibada, ni kutambika, kutembea barabarani na ekaristi takatifu ni kutambika, kula mwili wa bwana ni kutambika.

Tofauti ya matambiko ya waafrika na matambiko ya dini za ki abrahamic (uislamu, na ukristu). dini za kiafrika zinatumia nature kwenye matambiko au ibada zao.
  • Wanayama
  • Mimea
  • Majani
  • Milima
  • Maji
  • Mawe
  • Milima n.k
Dini zilizokuja ni nzuri, lakini zinafanya kazi kubwa kushetanisha ibada za kiafrika.
 
Kama ni hivyo basi tukubaliane hakuna shetani,,, [emoji848][emoji849][emoji19]
shetani yupo, anatenda kazi vyema kabisa. kila jamii ina namna ilivyo mchora shetani wake na mungu wake. hadithi za kufikilika hizi. lakini zinaukweli bayana kabisana katika maisha yetu ya kila siku.

Shetani wa waisraeli ni tofauti na shetani wa Aguni na hata wa giriki, majina hawafanani, lakini sifa karibia zote ni zile zile : kwamba ni mbaya, na ubaya ni yeye.
 
shetani yupo, anatenda kazi vyema kabisa. kila jamii ina namna ilivyo mchora shetani wake na mungu wake. hadithi za kufikilika hizi. lakini zinaukweli bayana kabisana katika maisha yetu ya kila siku. shetani wa waisraeli ni tofauti na shetani wa Aguni na hata wa giriki, majina hawafanani, lakini sifa karibia zote ni zile zile : kwamba ni mbaya, na ubaya ni yeye.
Shetani ni utendaji mwovu, hata binam akiwa mwovu sana tunaweza kumwita shetani,

Sasa pengine mtoa mada hajui hathari hasi za matambiko, madhara ya kutambikia miungu au mizimu!

Mimi ninae andika hapa najua tena nayajua haswa! Nimeyafanya kiuhalisia (practicing) sio dhana tu ya kuandika au kusikia! Na baada ya kuona madhara yake tukakimbia huko!

Matambiko ni ibada ya shetani totally! Kuabudu mizimu (miungu) kwa kutoa mnyama kama kafara etc Mbuzi, kondoo, kuku au ng'ombe! Vyakula , mimea au vinywaji ni kuabudu shetani! Na wanaofanya hivyo either kwakujua or kutokujua ni mawakala wa shetani! Either wanajua or hawajui! Amkeni!
 
Shetani ni utendaji mwovu, hata binam akiwa mwovu sana tunaweza kumwita shetani...
pole kwa kutwa na tukio hilo, kuna mambo mengi yanaweza kuchangia. rudi kwa wazee wakuelimishe, lakini sio lazima kutambika kiafrika, unaweza tambika kiroma au kiarabu kama inafanya kazi kwako.
 
pole kwa kutwa na tukio hilo, kuna mambo mengi yanaweza kuchangia. rudi kwa wazee wakuelimishe, lakini sio lazima kutambika kiafrika, unaweza tambika kiroma au kiarabu kama inafanya kazi kwako.
Ndio maana nakwambia wewe to naandika kitu usichokijua na Sina muda wa kuandika story ndefu hapa,

Haya mambo ya matambiko sisi wenzako tumeishi nayo na tumeyafanya kwa zaidi ya miaka 30, sio mambo ya kusema "rudi kwa wazee wako!" Au "tambika kwa kitoroma au kiarabu!" Sisi tumepractise hayo mambo kwa miaka na miaka na tunayajua nje ndani, na hao wazee unao wasema ndio walikuwa makasisi wakuu wakuongoza ibada hizo mbovu!

Tukaona madhara yake makubwa na mabaya yakutusha sana! Tena yakutisha mno! Usichukulie poa! Tukakimbia mbio! Sasa wewe either umeyasoma au kuyasikia mahali ukaamua kuyapa support kwakuwa huyajui kiuhalisia na kiundani wake! Wenzako wako huko wanataka kujitoa wanashindwa! Huko ni kifungo kibaya sana! Ni utumwa mbaya mno! Usisikie!
 
Ndio maana nakwambia wewe to naandika kitu usichokijua na Sina muda wa kuandika story ndefu hapa,

Haya mambo ya matambiko sisi wenzako tumeishi nayo na tumeyafanya kwa zaidi ya miaka 30, sio mambo ya kusema "rudi kwa wazee wako!" Au "tambika kwa kitoroma au kiarabu!...
nakijua ndio maana nakiongelea. na sitaki kujifanya najua kuliko wewe. kwasababu unachokisema kimekutokea ni kweli inatokea, na si kwasababa ya ubaya wa tambiko, bali kwasabab za mtu binafsi. vile vile naushuhuda wa mambo hayo hayo kwa watu wa dini za kibrahamu. ni swala la kukaa na viongozi wako na kulieleza.
 
Pengine kweli umepitia huko! Sipingi, lakini tunatofautia uzoefu na ufahamu! Na ujuzi wangu na uzoefu wangu hauwezi lingana na wako!

Na najua exactly tatizo lilikuwa nini!! Pia sio kwangu tu! Bali kwa familiar nzima hata ukoo na jamii inayotuzunguka inayofanya hayo matambiko pia!

Kiujumla hao viongozi unao wazungumzia walizidiwa kete! Matambiko yakiwa "serious" ni hatari sana hata kuliko uchawi! Achana nayo! Unaweza kuzunguka dunia nzima na usipate dawa! Ashukuriwe Mungu anaeweza yote!

Nakushauri ndugu yangu achana na hayo madudu tena epuka sana kuwaingiza wanao kwenye laana hiyo! Utakuja kuwapa tabu ya buree kujitoa humo! Maana matambiko ni kuuza nafsi yako kwa shetani kwahiari yako binafsi! Be aware bro!
 
sijui kuhusu uzoefu wetu.

kama kweli ulikua ndani ya imani hio, kuna namna nyingi za kutatua haya mambo. yanatokea kwenye kila imani.

kweli najua hata dini zingine, watu kuna forms nyingi za religious experience, zikikuzidia unaweza kua hatari. na hio hio dini ambayo unasema ni nzuri ikageuka kua mbaya.

mimi siwezi kuachana nayo, coz najua the uzuri wake na hatari yake. so nacheza hapo kati. vile vile kwenye imani zingine zikizidi sana unakua mtu mbaya unaweza kua hata gaidi, au ukatelekeza familia au ukaua watu kwasabab ya religious experiences.
 
Pengine kweli umepitia huko! Sipingi, lakini tunatofautia uzoefu na ufahamu! Na ujuzi wangu na uzoefu wangu hauwezi lingana na wako...
tambiko ni tukio adhimu la kidini lenye mfululizo wa vitendo vinavyofanywa kwa utaratibu uliowekwa. so kua makini na tukio unalo fanya, sio kila tambiko ni jema au zuri kwa afya ya roho yako.
 
sijui kuhusu uzoefu wetu.

kama kweli ulikua ndani ya imani hio, kuna namna nyingi za kutatua haya mambo. yanatokea kwenye kila iman...
Imani ni kitu Cha ajabu sana! Wengine useme imani ni kama kuvuta bangi! Ukizidiwa na imani bila maarifa na ufahamu matokeo yake ndio hayo ya ugaidi, ukibwetere na hata kuonekana mtu wa ajabu ajabu!

Naheshimu uamuzi wako, kwani imani iko moyoni mwa mtu husika! Na kuamini ni uhuru na uchaguzi binafsi wa mtu! Lakini kwangu binafsi na uzoefu wangu aisee mtu hawezi kunirudisha huko! Hata kwa bunduki!

Matambiko yanaweza kuonekana kama kitu cha utamaduni au kitu cha asili chenye kuheshimu na kulinda asili yetu! Kisicho na madhara yoyote! Lakini nyuma ya matukio hayo/ibada hiyo kuna agenja mbaya sana iliyojificha ambayo kiukweli inahitajika neema kubwa sana kuitambua hiyo Siri!
 
tambiko ni tukio adhimu la kidini lenye mfululizo wa vitendo vinavyofanywa kwa utaratibu uliowekwa. so kua makini na tukio unalo fanya, sio kila tambiko ni jema au zuri kwa afya ya roho yako.
Kwenye kila matambiko (ibada) kuna madhabahu ! Kwenye kila madhabahu kuna Mungu/miungu/mizimu anaye/inayo abudiwa hapo! Kwenye kila Mungu/miungu/mizimu kuna agenda yake ya kuabudiwa na matakwa yake!

Huyo Mungu au miungu inayoabudiwa hapo unaijua ni miungu gani?! Na ina mkataba gani na hao wazee wako (Kuna agano gani liliwekwa kati yao na miungu/mizimu hiyo hapo zamani)?! Na je, inaweza au imeshaweza kuachilia madhara/laana kiasi gani kwa wale wasio mtii/mwabudu au kutimiza matakwa yake(miungu/mizimu hiyo)?!
 
Imani ni kitu Cha ajabu sana! Wengine useme imani ni kama kuvuta bangi! Ukizidiwa na imani bila maarifa na ufahamu matokeo yake ndio hayo ya ugaidi, ukibwetere na hata kuonekana mtu wa ajabu ajabu...
sawa, lakini sio tambiko letu(jamii yangu)
 
Kwenye kila matambiko (ibada) kuna madhabahu ! Kwenye kila madhabahu kuna Mungu/miungu/mizimu anaye/inayo abudiwa hapo! Kwenye kila Mungu/miungu/mizimu kuna agenda yake ya kuabudiwa na matakwa yake!

Huyo Mungu au miungu inayoabudiwa hapo unaijua ni miungu gani?! Na ina mkataba gani na hao wazee wako (Kuna agano gani liliwekwa kati yao na miungu/mizimu hiyo hapo zamani)?! Na je, inaweza au imeshaweza kuachilia madhara/laana kiasi gani kwa wale wasio mtii/mwabudu au kutimiza matakwa yake(miungu/mizimu hiyo)?!
maswali yako hayana majibu, kwababu unaongelea matambiko lakini kwa mtazamo wa imani za dini za kiabrahamu. (hapo una kosea) na unaongelea uungu kwa tafsiri na imanai za dini hizo za kislamu na kikristu (hapo pia unakosea)

mizimu hatuabudu tunai activate.

mzimu ni neno la kishona, tafsri yake ni mizizi yangu, MIDZI-MIZIZI /////UMU-WANGU (MIDZIUMU)

na inaishi kwenye DNA za kila mmja wetu. sasa hapa ni swala la amani, mimi naamini babu yangu anaishi na mimi kila siku coz yupo kwenye DNA yangu.

kuna matambiko specila kwaajili ya ku activate DNA za mtu. hii ikikuingia sana, ndio unaanza kupata experience za kumuona babu yake ukilala. kama ambavyo walokole wanamuona yesu wakilala.(yesu wa kwenye picha za ukutani)

na mzimu hauwezi kua mtu yyte, bali yule alieishi vyema. na huyo ndio tuna activate DNA yake.

huwezi ku activate DNA yake kama hujawahi kumuona au hujawahi kusikia story yake, ili uwe inspired.

kuna mangi ku unpack kuhusu afrikan philosophy. lakini wakoloni hawakua na muda wa kustudy hio filosofi, wakaipachika jina na devilish practices.
 
sawa, lakini sio tambiko letu(jamii yangu)
Naendelea kukariri kwamba "naheshimu imani yako!"

Lakini kila matambiko yana madhara yake! Miungu au mizimu hiyo inayoabudiwa hapo ina masharti (maagano) yake! Hakuna mizimu au miungu itakuwa inakulinda au kukufanikisha BURE BURE TU lazima kuna MAAGANO! upande chanya (mafanikio) na upande hasi (madhara au laana)!

Mizimu au miungu mingine inayofanyiwa hayo matambiko itakuja kuachilia KICHAA, mingine itakuja kuachilia MAUTI unakuta kila mwezi September tarehe 20 au 22 lazima mtu afe kwenye ukoo wenu, inaweza kuwa kila mwaka au baadaa ya miaka miwili ,mitatu au minne! Mingine kila mtoto wakwanza wakiume lazima afariki piga ua! Mingine wanawake wote kwenye ukoo hawaolewi hata wawe wazuri vipi na wasomi vipi, hata wakiolewa lazima waachike! Na ni wote sio mmoja au wawili! Mingine kila baada ya mwaka fulani lazima mtu kwenu avunjike mguu au mkono either kwaajali ya gari au atadondoka tu ghafla akiwa bafuni, kwenye kiti au hata kitandani na kuvunjika either mfupa wa mguu au mkono!

Unaweza kusema kwetu hayo mambo hakuna! Vyema sana! Lakini kaa chonjo hakuna ulinzi wabure au manufaa ya bure kwa mizimu au miungu bila kulipia! Ndio maana nakwambia wewe bado hujafika decree hiyo! Sasa usije kufika ukiwa umechoka sana au umeumia sana (too late)! Haya mambo hayanaga huruma ndugu! Shetani hana huruma hata kidogo! Akiamua kuanza kula faida yake utajuta! Matambiko sio kitu kidogo kama unavyodhani au unavyoambiwa nyuma yake Kuna Siri kubwa! Shtuka ndugu!
 
Back
Top Bottom