Matamshi ya Mzee Yusufu Makamba yasiyo na busara, yameiadhiri CCM kwa kiasi fulani!

Marhabaaa
 
Busara ni kusema nini na wakati gani, na nini kinachokusudiwa.

Mambo ya Mwendazske na mambo mengi yasiyo ya kistaarabu aliyoyaonyesha hadharani ,si vizuri kuyajibu hadharani.
Ila ni vema yasirudiwe na kuyasahihisha.
Mwalimu miaja ya 76/77 aliwahi kuiambia CCM, TUJISAHIHISHE.

Alichofanya Makamba ni kusheherekea kifo cha mwendazake, na najua alitesa wengi, lakini Mungu ndio hulipiza ubaya wote wa binadamu.

Tunajua kulikuwa na vita ya chini kwa chini kati ya makundi ya Team JK na Team JPM, lakini kusheherekea hadharani badala kuwaweka pamoja watanzania, hapo naona si busara hata kidogo.
 
Ila ilikuwa poa alipoongelea ubatizo wa moto kwa wapinzani!

“Ukishaanza kula nyama ya binadamu huachi”.
 
Sio kabla ya kuongea bali asipewe tena maiki!
 
Tulia kijana hutoamini kitatokea. Mzee amelitafuta asilo lijuwa nilidhani kwa kukaa kwake jeshini anajuwa silence war ila ametoka nje ya mstari.
Acha mikwara.....hayo yashapita tayari
 
Hiki chama kimebaki cha wajinga tu.
Wanatanguliza njaa/tamaa kuliko utu.
Mbona aliyekuwa kiongozi wa chama Philip Mangula akulopoka
Makamba + kikwete waache Ubinafsi
HEKIMA 10.

Hekima 1
Unaweza kuwa kiongozi mzuri bila kuanika madhaifu ya mtangulizi wako Rekebisha kwa kadri unavyoweza matendo yatasema yenyewe.

Hekima 2
Unaweza kueneza Imani yako bila kuisema vibaya Imani ya watu wengine. Elezea uzuri wa imani yako wakivutiwa watakuja wenyewe.

Hekima 3
Usitafute mafanikio kwa kumkosesha mwingine. Dunia haijawahi kuishiwa kitu cha kumhudumia kila mtu kwa sababu hata mwenye vingi akiondoka anaacha vyote.

Hekima 4
Mchawi akija kwako bila kuonekana usimuangamize kwa kuonekana. Ukifanya hivyo wewe ndio utakuwa mhalifu na yeye mwenye haki.

Hekima 5
Usifikiri kuwa, kile unachokijua ndio usahihi wa maisha ya watu. Binadamu wote ni wanafunzi siku zote mpaka wanapoondoka Duniani.

Hekima 6
Mama yako akikuficha Baba usimlaumu. Alichokibeba anajua akikishusha kwako huwezi kustahimili.

Hekima 7.
Ukipata nafasi ya kuongea, ongea machache. Hakuna mwenye maneno mengi yakakosa hila ndani yake.

Hekima 8
Usiifanye pesa ichukue nafasi ya uwepo wako katika matukio ya kijamii. Kuna siku jamii itatuma pesa kwenye tukio lako bila uwepo wake.

Hekima 9
Usipakue chakula kingi kwa sababu ya hisia za njaa kubwa. Ni heri kuongeza kuliko kubakiza na kutupa.

Hekima 10
Kila unapopanda ngazi ya maisha waheshimu unaowaacha chini. Hao ndio watakupokea wakati unashuka.

 
Miaka ya nyuma niliwahi kuandika kuwa CCM inaweza kufa chini ya Ukatibu Mkuu wa Yusufu Makamba.
Wakati nakusoma kabla ya kufikia kwenye mstari huu, nilikuwa nataka kuuliza swali linalohusiana na mstari huo: kwamba, Yusuf amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama, je, huko kukosa busara kulianza lini?

Lakini mkuu 'Jidu', wewe na mimi tunaelewana sana kutokana na maandiko yetu humu JF kwa muda kitambo sasa, na hasa kuhusiana na swala hilo hilo la chama hiki ambacho mara zote hujitambulisha kuwa wewe ni mmoja kati yao.
Swali langu siku zote limekuwa ni lile lile kwako: hivi hii CCM unayojivunia kuwa mwanachama wake, ni kipi hasa kinachoendelea kukuvutia wewe, hata bila ya kuwafikiria akina Yusuf, kwa sababu najua wapo wengi sana ndani ya chama hicho sasa hivi.
 
Kwani mkutano wote ule wewe ulisikia busara gani kama wote haukuwa umejaa pumba tupu. Ulimsikia mtu yeyote akizungumza kuhusu sera za kuiendeleza nchi zaidi ya kupambiana kuhusu urais tu?

Makamba alishasema kuwa mtoto wake lazima awe waziri na kweli ikawa hivyo, sasa hivi anasema atakuwa rais tu hata kama anaongea pumba.

Makamba huyu ndiyo aliyekuwa ameiua kabisa CCM ikawa inazomewa mitaani, sasa hivi wanajitutumua baada ya heshima ya CCM kuwa imerudi na wako mbioni kuibomoa tena kwa pumba kama hizi. Hata Kikwete mwenyewe alisimamama akaongea pumba tupu.

Huko CCM ya sasa busara za namna hii hazipo tena.


 
Pia pamoja na kauli ya rais Samia kumuombea radhi haitoshi,watu mkutanoni wameondoka na donge kadhalika watanzania kwa ujumla wamehudhunika wapo ambao hawawezi samehe kauli hiyo.
Kifupi ujuaji mwingi mbele giza
Ni vigumu kusamehe maneno ya kishenzi kama hayo.
Ambao tumefiwa na ndugu zetu waliokuwa wazuri kabisa kwenye familia na kwenye jamii, then anakuja mshenzi mmoja kutuambia kuwa wamekufa kwa kuwa walikuwa wabaya, huo ni ushetani kuliko hata ibilisi mwenyewe.
Watu wamefiwa na watoto wao wakiwa bado wachanga, hawajui mema wala mabaya, then ibilisi mmoja anasema eti walikufa kwa kuwa walikuwa waovu. Huko ni kumkufuru Mungu ambaye anapanga kifo cha kila mmoja wetu. Huyu mzee ni shetani.
 
yanaiadhiri ccm vipi kwani huo ni msimamo wa ccm?
 
Noted.
 
Tupo katika wakati mgumu kisiasa.
Transission ya uongozi baada ya Magufuli imepewa kipaumbele na CCM katika mkutano uliopita badala ya utatuxi wa kero za wananchi.
CCM inaelekea kuupa kipaumbele ubinafsi kuliko kile wananchi walichotaka kisikike- utatuzi wa kero na sera za maendeleo.
Low point mkutano mzima ni kumpa Yusufu Makamba kuongea utumbo usiosameheka.
Hatujasahsu jinsi alivyokiingiza shimoni chama alivyokuwa katibu mkuu.
 
Mkuu uko sawa, mimi mwana CCM, kada.
Nisingependa kurudia historia ya karibuni ya chama, lakini kiini cha kubomoka kimaadili, kimsimamo na kisiasa ni uroho wa madaraka na ubaguzi wa kikanda.
Kiini hiki tunaweza kutofautiana lakini baada ya kuundwa "Mtandao" ndani ya chama, hiki chama kikawa cha watu fulani.
 
Sisi hayatuhusu malizaneni wenyewe
 
Nimekusoma mkuu 'Jidu'.
Search your soul country mate.

Aliyokuandikia hapo mkuu 'Kichuguu, na kukuwekea "ushahidi" wa hotuba, bila shaka umekuchoma moyo ipasavyo.
 
Mtu mzee akikosa busara hugeuka mpumbavu. Huyo babu kavimbiwa posho ndio maana ana bwatuka tu.
Hajawahi kuwa na busara from a way go. Tusichanganye kuvaa baraghashia na busara wala nywele nyeupe mnvi na busara wala uzee na busara wala ubwabwajaji na upepetaji mdomo na busara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…