Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Tujitahidi sana tusiwe watumwa wa kipato kwa kuwategemea waajiri. Tunaweza kuepukana na jambo hili kwa kufanya kazi za kujitegemea kama kulima na kufuga. Najua si kazi rahisi, ila ndio njia pekee ya kuwa huru katika nchi hizi za Ki-Afrika palipojaa ubabaishaji wa waajiri.Wapo watumishi wasioona mafanikio ya kutatuliwa kero zao za kiutumishi siku ya Mei Mosi, wapo watumishi wasio wanachama licha ya kukatwa mishahara yao ili kulipia michango ya vyama vya wafanyakazi, wapo watumishi wanao amini michango yao inaliwa tu na viongozi wa vyama hivi kwa kujilipa mishahara mikubwa na posho nyingi. Wanaamini wanaostahili kuandamana ni viongozi wa vyama na viongozi wakubwa wa serikali. Kumekuwa na tabia ya waajiri kuwalazimisha watumishi kuhudhuria sherehe hizi hasa watumishi waliopo katika eneo ambalo sherehe hizi zinafanyika kitaifa. Humu ndani Kuna wabobezi wa sheria za kazi, watusaidie je, usipohudhuria ni kosa kisheria na mwajiri anaweza kukuchukulia hatua?
Ewe mwajiriwa, kabla ya kutumia mkopo wako kujenga nyumba ya kuishi, hakikisha hapo kwako una angalau Ng'ombe wawili wa maziwa, mbuzi watano wa kienyeji watakakuwa wanaongezeka taratibu na kuku angalau 50-100 wa mayai au nyama. Lasivyo tutaendelea kuwa watumwa mpaka siku ya kiama (kama ipo).