DOKEZO Matangazo na barua za vitisho zashamiri kwa wataokaidi kuhudhuria Sherehe za Mei Mosi kitaifa Morogoro. Sheria ikoje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tujitahidi sana tusiwe watumwa wa kipato kwa kuwategemea waajiri. Tunaweza kuepukana na jambo hili kwa kufanya kazi za kujitegemea kama kulima na kufuga. Najua si kazi rahisi, ila ndio njia pekee ya kuwa huru katika nchi hizi za Ki-Afrika palipojaa ubabaishaji wa waajiri.

Ewe mwajiriwa, kabla ya kutumia mkopo wako kujenga nyumba ya kuishi, hakikisha hapo kwako una angalau Ng'ombe wawili wa maziwa, mbuzi watano wa kienyeji watakakuwa wanaongezeka taratibu na kuku angalau 50-100 wa mayai au nyama. Lasivyo tutaendelea kuwa watumwa mpaka siku ya kiama (kama ipo).
 
Kwanini Sherehe Hizi Hazina Tofauti Na Mwenge Maana Kuna Kulazimishana Kwa Chini Chini Huku Wakuu Wakijifanya Kama Hawajui Lolote
 
Wafanyakazi ni wanyonge siku zote kwa sababu "waliuza" uhuru, haki na nguvu yao kwa Trade Unions.

Siku wakiitaka tena hiyo nguvu yao budi watoke huko, wasimame kwenye "collective bargain".

Ngumu lakini ndio tiba pekee sahihi na ya uhakika.
 
Acheni unyonge hao Tucta na mwajiri wako wanaanzaje kukulazimisha mtu na akili yako uko home kwako na ni public holiday umewasha TBC unasikiliza Mh Rais live kama atasema chochote kuhusu maslahi yako kuanzia mwaka wa fedha unaoanza tarehe 1 july .Msipoangalia hao waajiri wenu watawaagiza kufanya hata mambo yaliyo kinyume na standing order
 
Nadhani wengi huwa wanashiriki. Kuna posho sehemu nyingi so wengine huenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…