Moshilabusara
New Member
- Dec 20, 2018
- 4
- 13
Matangazo ya mara kwa mara kuhusu El Niño yameanza kuwapa hofu baadhi ya wananchi. Wakati mwingine mtu anafikia hatua ya kusita hata kufanya mambo ya msingi kwa sababu anawaza, “Itakuwaje?” Maana ukweli ni kwamba, nyumba nyingi tunazoishi ni za hali ya kawaida tu na si kila mtu ana uwezo wa kukabiliana na mafuriko au mvua kubwa.
Ni muhimu serikali kuendelea kutoa tahadhari, lakini sambamba na tahadhari hizo, tungependa kuona maandalizi ya vitendo yakiongezeka zaidi.
Kama kuna maeneo yanayotajwa kuwa hatarishi, tuone magari kama Yutong yakitumiwa kuwatoa wananchi mapema na kuwapeleka maeneo salama na yenye mwinuko. Serikali iwe na maeneo maalumu ya dharura katika kila eneo, pamoja na akiba ya mahema na vifaa vya msingi kwa ajili ya wananchi endapo dharura itatokea.
Tanzania imewahi kuhamisha wananchi wakati wa majanga. Kama tuliweza kufanya hivyo wakati mwingine, kwa nini tusijiandae mapema pale tunapoona dalili za hatari?
Pia tuone:
Kuna madhara mengine ya kutia hofu kupita kiasi. Mkulima anaweza kuogopa kuwekeza au kulima kwa kujiamini akiamini mvua itakuwa kubwa sana, halafu mvua isipokuwa kama ilivyotangazwa. Mwisho wa siku tunaweza kujikuta tunakutana na changamoto ya chakula mwaka unaofuata, si kwa sababu tu ya mvua, bali pia kwa sababu watu waliogopa kuchukua hatua.
Hata watoto wetu wanaanza kuuliza nyumbani: “Baba, hii El Niño ikija kwenye hii nyumba tutakufa?” Hili linaonyesha kwamba namna tunavyowasilisha tahadhari inaweza pia kuathiri kisaikolojia jamii.
Tahadhari ni muhimu, lakini tahadhari iende sambamba na maandalizi.
Tusiwatishe wananchi tu kuhusu mvua inayokuja. Tuambie pia: “Hii ndiyo hatari, na haya ndiyo tunayofanya ili kuwalinda.”
Tanzania imepitia misiba na majanga makubwa na tumeyavuka. Tuendelee kuwa tayari, lakini pia tuendelee kuishi, kufanya kazi, kulima na kujenga maisha yetu kwa matumaini.
Kama inanyesha, inyeshe. Mungu atusaidie na atupe hekima ya kujiandaa.
🇹🇿 MUNGU IBARIKI TANZANIA. NAKUPENDA TANZANIA.

- Mitaro ikisafishwa kabla ya mvua kubwa.
- Mitaro iliyoziba ikizibuliwa.
- Maeneo yenye uhitaji mkubwa yakijengewa mifereji.
- Wananchi wanaoishi maeneo hatarishi wakitambuliwa mapema.
- Maeneo yenye vyanzo vya maji yakitumiwa vizuri kwa kilimo cha umwagiliaji, ili kama mvua haitatosha, uzalishaji wa chakula usisimame.
- Vijana na watu wenye uwezo wa kuwekeza wawezeshwe kutumia fursa hizo.