Matani

Matani

Hapa kuna mawili ama ulikulia bandarini...maeneo ya masoko ya mazao, karibu na shughuli za "CREW" za Tanesco...au kule Mwaloni.
 
Jamani nilipokuwa mdogo hii ndo ilikuwa hobby yangu maana kwa umbo langu dogo sikuweza kupigana ila ukinikosea kidogo..nitakupa neno utakaa kimya mwenyewe!
Najikumbushia tu...(usinichukie...)

Unataka matani.. Nyani Ngabu, una bichwa kubwa mpaka shuleni ulikuwa unaitwa Headboy! twende twende..
fidel 80, wewe umekonda mpaka ukisimama kwenye ukuta unakaa kama crack...
:Mzee mwanakijiji demu wako amekonda mpaka akivaa t-shirt ya bluu anafanana na sim card ya tiGO.. Asprin unamashavu kama mimba ya panya..
Na wewe TUKUTUKU uso kama shamba la matuta...
Unataka unataka..
Mwangalie kwanza, wewe Bigirita yaani wewe ni mbaya mpaka hutumia lotion inayoitwa 'why bother!'..teh teh..
Zak wewe ni mweusi mpaka ukirushiwa jiwe linarudi kuitisha tochi...

PS: On a light touch...

Hahahaaa ww ni noumerrr..BIG UP MCHONGOANO (SHUJAAZ)
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahaa we Mentor una vituko kweli kweli muone kwanza unapiga hodi mpaka kwenye lift.
 
Last edited by a moderator:
Tehtehteh mi cmo

Ndo maana wewe ni mfupi hadi unaweza kutembea chini ya uvungu!

Hapa kuna mawili ama ulikulia bandarini...maeneo ya masoko ya mazao, karibu na shughuli za "CREW" za Tanesco...au kule Mwaloni.

TUJITEGEMEE, wewe ni mrefu mpaka siku nyingine malaika wakiboeka wanaanza kukusuka matuta.

Hahahaaa ww ni noumerrr..BIG UP MCHONGOANO (SHUJAAZ)


kwenu watakatifu mpaka ugali mnasongea msalaba

Ndio maana wewe hutoroka kazini ili uje kuteleza na soksi nyumbani!

Utani mwingine unawe ukaumia moyoni...japo usioneshe hasira zako. Hata mie nimeikubali. Huyo jamaa ni munoma.

Ndevu mbili ninyi kwenu wachoyo mpaka mkipika kuku mnakula bila kuwasha taa!

Ulikula sabuni ukajinyea mapovu.

Ulimeza kaseti ya Awilo ukajamba ndombolo!

Muone mdomo kama raba ya bubu

diuretic: nyie ni washamba hadi siku moja mlikuwa na kaka yako mnasikiliza redio. mtangazaji akasema, "Na sasa tunawapeleka moja kwa moja hadi uwanja taifa"....mkadandia redio kwa pamoja!

Hahahahahahaa we Mentor una vituko kweli kweli muone kwanza unapiga hodi mpaka kwenye lift.

Masikio yako makubwa mpaka ukienda mgahawa chai inapoa!

brenda18: umekonda hadi unavaa soksi na mkanda....
Heaven on Earth: nasikia wewe ni mjinga hadi ulirudia kunyonya!!!
Kaizer: una shingo ndefu mpaka ina kiwiko

 
Last edited by a moderator:
Mentor : Twende twende mwangalie umekonda mpaka unachomekea suti.
 
Last edited by a moderator:
Mentor kwenu pachafu hadi mende wamechangishana hela kuleta gari la taka
 
mentor una bichwa kubwaa mpaka watu walikubandika tangazo wakat upo stand wakizani ukuta

Hehehe... mkuu wewe tusemeje sasa! Nasikia bibi yako ni mzee hadi alisahaugi pochi yake kwenye safina ya Nuhu.

Mentor nimechekaje aisee..........na mie namtafuta wa kumtania LOL

Heaven on Earth anza na mimi.

Muone kwanza, sura mbaya hadi ukinanii na kipofu bado anafunga macho.


Mentor : Twende twende mwangalie umekonda mpaka unachomekea suti.

Ablessed, unataka? We mshamba hadi huweka redio kwenye friji ndo usikie, 'cool music'


Mentor kwenu pachafu hadi mende wamechangishana hela kuleta gari la taka

diuretic, heri kwetu tu kuchafu yani wewe ni chafu mpaka nzi wakitua mwilini mwako wanakuwa wamevaa buti.

Uliitwa mentor sababu ulinunuliwa chupi mpya ukachomekea koti bila suruali.
taamu, hahaha!

Ndo maana una mikono mikubwa hadi vidole vyako vyote ni gumba!HEHE

Unataka..unataka!??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom