Nilipoona neno "matani" nikajua ni straight from green city.
Bichwa kubwa,kusikitika huwezi.
na wewe nini: Sura mbaya kama umetaka kupiga chafya ikakataa
Nilipoona neno "matani" nikajua ni straight from green city.
Jamani nilipokuwa mdogo hii ndo ilikuwa hobby yangu maana kwa umbo langu dogo sikuweza kupigana ila ukinikosea kidogo..nitakupa neno utakaa kimya mwenyewe!
Najikumbushia tu...(usinichukie...)
Unataka matani.. Nyani Ngabu, una bichwa kubwa mpaka shuleni ulikuwa unaitwa Headboy! twende twende..
fidel 80, wewe umekonda mpaka ukisimama kwenye ukuta unakaa kama crack...
:Mzee mwanakijiji demu wako amekonda mpaka akivaa t-shirt ya bluu anafanana na sim card ya tiGO.. Asprin unamashavu kama mimba ya panya..
Na wewe TUKUTUKU uso kama shamba la matuta...
Unataka unataka..
Mwangalie kwanza, wewe Bigirita yaani wewe ni mbaya mpaka hutumia lotion inayoitwa 'why bother!'..teh teh..
Zak wewe ni mweusi mpaka ukirushiwa jiwe linarudi kuitisha tochi...
PS: On a light touch...
Utani mwingine unawe ukaumia moyoni...japo usioneshe hasira zako. Hata mie nimeikubali. Huyo jamaa ni munoma.
Tehtehteh mi cmo
Hapa kuna mawili ama ulikulia bandarini...maeneo ya masoko ya mazao, karibu na shughuli za "CREW" za Tanesco...au kule Mwaloni.
Hahahaaa ww ni noumerrr..BIG UP MCHONGOANO (SHUJAAZ)
kwenu watakatifu mpaka ugali mnasongea msalaba
Utani mwingine unawe ukaumia moyoni...japo usioneshe hasira zako. Hata mie nimeikubali. Huyo jamaa ni munoma.
Ndevu mbili ninyi kwenu wachoyo mpaka mkipika kuku mnakula bila kuwasha taa!
Ulikula sabuni ukajinyea mapovu.
Ulimeza kaseti ya Awilo ukajamba ndombolo!
Muone mdomo kama raba ya bubu
diuretic: nyie ni washamba hadi siku moja mlikuwa na kaka yako mnasikiliza redio. mtangazaji akasema, "Na sasa tunawapeleka moja kwa moja hadi uwanja taifa"....mkadandia redio kwa pamoja!
Hahahahahahaa we Mentor una vituko kweli kweli muone kwanza unapiga hodi mpaka kwenye lift.
Masikio yako makubwa mpaka ukienda mgahawa chai inapoa!
brenda18: umekonda hadi unavaa soksi na mkanda....
Heaven on Earth: nasikia wewe ni mjinga hadi ulirudia kunyonya!!!
Kaizer: una shingo ndefu mpaka ina kiwiko
mentor una bichwa kubwaa mpaka watu walikubandika tangazo wakat upo stand wakizani ukuta
Mentor nimechekaje aisee..........na mie namtafuta wa kumtania LOL
Mentor : Twende twende mwangalie umekonda mpaka unachomekea suti.
Mentor kwenu pachafu hadi mende wamechangishana hela kuleta gari la taka
taamu, hahaha!Uliitwa mentor sababu ulinunuliwa chupi mpya ukachomekea koti bila suruali.