Matapeli waoneeni huruma Watanzania

Utapeli wa simu utaendelea kuwepo hadi pale NIDA, TCRA, Wizara ya Mawasiliano watapokubaliana Mtu 1, Line 1 ya Mtandao 1

Kampuni, Biashara zisajili kwa kutumia leseni za biashara husika, pamoja na TIN.

Ikitokea Namba husika imefanya uhalifu wowote NIDA husika ifungiwe kusajili line.

Wasipofanya hivyo wataendelea umiza watu
 
Wazo zuri sana hili. Waongeze angalau iwe dakika 5
 
Nimekuelewa mkuu...

Nilimaanisha kwamba mfano msg imekuja katumiwa 500000 na huyo tapeli anaedai kutuma pesa kimakosa or kivingine alafu akataka arudishiwe labda 400000 kwa kutumiwa kwenye namba ingine au kwa wakala.
Kwanini uyu mtu asiende kutoa iyo pesa aliyotumiwa kwanza alafu ndio akishapata cash aitume? Kuliko kumwambia wakala kuwa atupe pesa kwakuwa pesa anayo kwenye cm.🤔
 
kesi ya laki 1 na nusu unataka kupeleka cyber crimes kweli. yani iyo samehe tu apo mtaliwa pesa na hairudi. wakala hana akili we unakubali vipi kutuma pesA kabla mteja hajakupa cash vipi ikiwa kaja na hela pungufu au akakupa hela feki
 
Huo sasa ni mtindio wa ubongo kuamini msg bila kuhakiki salio!
 
Yaweza kuwa hivyo, lakini hiyo laki na nusu haiangaliwi kwa wingi ama uchache wake, hapo linaangaliwa kosa lililotendwa.

Maana tapeli akipatikana na akabananishwa, hapo hata millioni anatoa ama kwenda kusota jela.
hao matapeli wanatamba kwakua polisi hawana time nao , ni kesi za kitoto
ni kesi zinazokua incited na tamaa ya mlalamikaji
 
Wazee ndo wanaongozwa kwa kupigwa kwa hizi miamala hewa!

BTW:Hicho kitengo cha cyber bora kingefutwa tu huko polisi maana hakina msaada wowote.

Kuna mtu namfahamu ana RB miaka mitatu sasa na namba zilizotumika kutapeli zinapatikana zote tatu na namba ya akaunti iliyopokea pesa wanayo polisi.

Hicho kitengo kingebinafsishwa tu makampuni yakaingia ubia na PT hata kama raia watachangia gharama kuliko ilivyo sasa.
 
polisi hawezi deal na kesi ya kipumbavu kama hizo zinazo zinazozalishwa na tamaa yako, utaulizwa tu, "kwanini umtumie pesa mtu ambaye humjui ?" hapo polisi kamaliza
Mantiki yangu awape kesi polisi wadeal nae wagawane utapeli na huyo mtu.
Ye ni kuwapa no tu na kuwaambia km tumetapeliwa bil 2 na huyu mtu uone km hawajamkamata.
 
Hii mbinu haiwez kutumika hapo..kakamatwa kiboya sana..kama namba iko hewani uyo watu wa cyber wanamnasa vizur tu
 
Wazo zuri sana,ukitumiwa wangefanya kutoa ni baada ya dk 15 kwa mfano ingekua safi sana
 
Wanapigwa wengi sana kwa mbinu hii, na ndio hutumiwa zaidi kwa sasa😬
 
Halafu bado yupo hewani sijui anajiamini vipi sijui anajua Hakuna mtu mwenye kumfatilia au sababu ya ujinga.
kuna jamaa yangu fulani yeye kasomea mambo ya cyber security sijui vidude gani sijui, sasa baada ya dada wetu wa mtaa kutapeliwa tukamuelekeza kwa mshakaji wetu ili amsake huyo tapeli tukamtie adabu, baada ya kuchek tukagundua jamaa yupo mikocheni.... tukiwa tunajiandaa na kuweka mipango sawa na kumshirikisha jamaa yetu ambae ni askari, yule askari akaweka protokali sawa pale kituoni then tukasema sasa tumcheki yupo wapi, ile kucheki tukagundua dakika tatu nyuma jamaa alikuwepo pale pale tulipokua sie kipindi tunamcheki mara ya kwanza halafu akamtumia meseji yule dada "utakufa kifo kibaya saana kwa kunifuatilia" 😀 😀 😀 watu wote tulitawanyika na kesi ikaishia hapo, tukawaachia polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…