Matapeli waoneeni huruma Watanzania

Matapeli waoneeni huruma Watanzania

Utapeli wa simu utaendelea kuwepo hadi pale NIDA, TCRA, Wizara ya Mawasiliano watapokubaliana Mtu 1, Line 1 ya Mtandao 1

Kampuni, Biashara zisajili kwa kutumia leseni za biashara husika, pamoja na TIN.

Ikitokea Namba husika imefanya uhalifu wowote NIDA husika ifungiwe kusajili line.

Wasipofanya hivyo wataendelea umiza watu
 
utapeli wa aina hii umeota mizizi mtaani ni janga kubwa mnoo na ni mara chache sana kuskia matapeli wa aina hii kukamatwa na kuchkuliwa hatua za kisheria.

Miamala ya kutumiwa na kutoa chap chap au kutuma kwa mtu mwingne ndan ya dakika 1 tu ndicho wanachojivunia hawa matapeli

Ingekuwa laini za wateja haziruhusiwi kupokea pesa na kuituma au kuitoa ndan ya dakika 1
Yaani pesa ikishaingia kwa mteja ikae angalau dakika 5 ndipo aweze kufanya muamala wa kuitoa au kuituma.
Nafikiri kwa njia hii tungeweza kuzuia miamala mingi ya kitapeli
Wazo zuri sana hili. Waongeze angalau iwe dakika 5
 
Staili hiyo unatapeliwa kirahisi mno.

Tapeli anaweza tuma pesa na akaiblock muda huo huo.

Utakapouliza salio figures zitaonekana pesa ipo lakini utapotaka kuitoa hauwezi utaambiwa "salio lako halitoshelezi" na baada ya masaa72 tarakimu hizo hupotea na kurudi kawaida.

Kama itakuwa una kiwango cha kutosha kwenye simu waweza kuhadaika baada ya kujiridhisha kuangalia salio na ukatuma kwa tapeli kumbe hela uliyotumiwa haipo.

Sijui kama nimeeleweka vizuri.
Nimekuelewa mkuu...

Nilimaanisha kwamba mfano msg imekuja katumiwa 500000 na huyo tapeli anaedai kutuma pesa kimakosa or kivingine alafu akataka arudishiwe labda 400000 kwa kutumiwa kwenye namba ingine au kwa wakala.
Kwanini uyu mtu asiende kutoa iyo pesa aliyotumiwa kwanza alafu ndio akishapata cash aitume? Kuliko kumwambia wakala kuwa atupe pesa kwakuwa pesa anayo kwenye cm.🤔
 
kesi ya laki 1 na nusu unataka kupeleka cyber crimes kweli. yani iyo samehe tu apo mtaliwa pesa na hairudi. wakala hana akili we unakubali vipi kutuma pesA kabla mteja hajakupa cash vipi ikiwa kaja na hela pungufu au akakupa hela feki
 
Nimekuelewa mkuu...

Nilimaanisha kwamba mfano msg imekuja katumiwa 500000 na huyo tapeli anaedai kutuma pesa kimakosa or kivingine alafu akataka arudishiwe labda 400000 kwa kutumiwa kwenye namba ingine au kwa wakala.
Kwanini uyu mtu asiende kutoa iyo pesa aliyotumiwa kwanza alafu ndio akishapata cash aitume? Kuliko kumwambia wakala kuwa atupe pesa kwakuwa pesa anayo kwenye cm.[emoji848]
Huo sasa ni mtindio wa ubongo kuamini msg bila kuhakiki salio!
 
Yaweza kuwa hivyo, lakini hiyo laki na nusu haiangaliwi kwa wingi ama uchache wake, hapo linaangaliwa kosa lililotendwa.

Maana tapeli akipatikana na akabananishwa, hapo hata millioni anatoa ama kwenda kusota jela.
hao matapeli wanatamba kwakua polisi hawana time nao , ni kesi za kitoto
ni kesi zinazokua incited na tamaa ya mlalamikaji
 
Wazee ndo wanaongozwa kwa kupigwa kwa hizi miamala hewa!

BTW:Hicho kitengo cha cyber bora kingefutwa tu huko polisi maana hakina msaada wowote.

Kuna mtu namfahamu ana RB miaka mitatu sasa na namba zilizotumika kutapeli zinapatikana zote tatu na namba ya akaunti iliyopokea pesa wanayo polisi.

Hicho kitengo kingebinafsishwa tu makampuni yakaingia ubia na PT hata kama raia watachangia gharama kuliko ilivyo sasa.
 
polisi hawezi deal na kesi ya kipumbavu kama hizo zinazo zinazozalishwa na tamaa yako, utaulizwa tu, "kwanini umtumie pesa mtu ambaye humjui ?" hapo polisi kamaliza
Mantiki yangu awape kesi polisi wadeal nae wagawane utapeli na huyo mtu.
Ye ni kuwapa no tu na kuwaambia km tumetapeliwa bil 2 na huyu mtu uone km hawajamkamata.
 
Nilimkamata mmoja 2017 nilimchapa hatari alifurahi na show

Ilikuwa hivi alimtapeli msichana wa rafiki yangu alikuwa akifanya kazi ya uwakala, alimlaghai na akamtapeli kama laki tatu hivi na kidogo, na simu

Alichokosea akachukua namba kwenye simu ya jamaa ambaye ni rafiki yangu akawa anamlaghai yeye ni shemeji yake na amekwama anaomba amtumie pesa jamaa hakujua naye akamtumia pesa jamaa akaona dezo kila baada ya siku mbili akawa anaomba pesa tena jamaa akawa anamtumia bila ya kujua,

Baada kama ya wiki msichana akamtafuta mchumba ake na kumjulisha kuwa nimetapeliwa pesa na simu ndio maana unaona sipo hewani, jamaa ndio kushituka kuwa anatapeliwa akaona hapa njia ya kumpata ni kuendelea kuwasiliana nae na kumtumia pesa ndogo ndogo ili ampate na alimwambie yeye yupo mkoani yaani yupo mbali na mchumba ake kwa hivyo hata mawasilino siku hizi ampati.. aaaa

Jamaa alinifichaga huo mchongo, akajitahidi kumtega jamaa na rafiki zake wengine wakakwama , sasa kuna jamaa akaniibia siri kuwa mwanao katapeliwa yeye na demu wake, yaani na bado anaendelea kutapeliwa, nikakutana naye nikamwambia mwanangu umetapeliwa na unanificha mwanao, akashtuka akanambia sorry mwanangu ndio akanipa picha lote hilo... nikamwambia kumpata mbona kitu rahisi akuamini,

Mimi nikamwambia huyo jamaa lazima atakuwa anakunywa pombe tu wewe mwambie jumaapili moja mkutane mlewe alafu mambo mengine niachie mimi, ilikuwa alhmisi nikamwambia mtumie sms sasa hivi jamaa akamtumia sms yulee tapeli akajibu kuwa pombe zinapanda na akakubali kukutana na shemeji yake aliyemtapelia msichana wake kuwa watakutana waumwagilie moyoo daaah kweli bia tamu jamaa akaingia king banah

Lakini baada ya kuchagua bar kama nne hivi tofauti na kumpeleka jamaa na kumwambia aende bar ingine hatumaye akachagua bar moja baada ya kutusumbua sana tulikuwa na ngoma ngumu kama saba hivi ambazo hazicheki ovyo

Huyo jamaa yangu aliniona nna roho mbaya hatari, kuanzia mchoro mapaka kumtia mkononi na kichapo alichopata jamaa tapeli.. tulibadilisha muonekanao wa sura na miguu yake kwa nondo, tulihakikisha akipumua anatoa damu mdomoni na puani na awezi kutembea ndipo tulipompeleka polisi

Hao ni wetu na sisi ndio dawa yao- mimi nawahitaji sana hao
Hii mbinu haiwez kutumika hapo..kakamatwa kiboya sana..kama namba iko hewani uyo watu wa cyber wanamnasa vizur tu
 
utapeli wa aina hii umeota mizizi mtaani ni janga kubwa mnoo na ni mara chache sana kuskia matapeli wa aina hii kukamatwa na kuchkuliwa hatua za kisheria.

Miamala ya kutumiwa na kutoa chap chap au kutuma kwa mtu mwingne ndan ya dakika 1 tu ndicho wanachojivunia hawa matapeli

Ingekuwa laini za wateja haziruhusiwi kupokea pesa na kuituma au kuitoa ndan ya dakika 1
Yaani pesa ikishaingia kwa mteja ikae angalau dakika 5 ndipo aweze kufanya muamala wa kuitoa au kuituma.
Nafikiri kwa njia hii tungeweza kuzuia miamala mingi ya kitapeli
Wazo zuri sana,ukitumiwa wangefanya kutoa ni baada ya dk 15 kwa mfano ingekua safi sana
 
Wasalamu,

Kipo kisa kilichotokea juzi cha kujifunza. Kinahusisha wahusika wanne. Ambao ni binti, wakala, tapeli na boss wa binti.

Binti wa Kazi kapokea message kwamba katumiwa shilingi 750,000 kupitia namba hii 0672312375 ya tapeli, kisha tapeli kampigia simu binti kwamba amekosea kutuma pesa anaomba arejeshewe pesa hizo, binti kaambiwa asimwambie mtu yeyeto (kuuteka ufahamu) na aende kwa wakala akazitoe pesa hizo KISHA amuwekeek wenye namba hio ya tapeli.

Binti hana uelewa na aina hii ya utapeli kaondoka nyumbani kimya kimya asiwaambie watu kafika kwa wakala. Kafika kwa wakala kamwambia pesa ipo kwenye simu naomba nitumie pesa kwenye simu namba hii akaonyesha namba ya tapeli alikuwa kaiandika kwenye karatasi kisha atatoa hela hio laki saba unusu, wakala akasema hana kiasi hicho yaani lakini saba na nusu bali ana laki moja na nusu, huku tapeli Akiendelea kuongea na binti (kauteka ufahamu wake) akamwambia mwambie anitumie hio laki na nusu.

Wakala akamuuliza binti mara mbili mbili unayo hio hela binti akasisitiza ninayo kwenye simu. Kosa la wakala ni kuamini na kutuma pesa kwa tapeli bila kupokea pesa toka kwa binti. Hili ni kosa kubwa Sana wafanyalo baadhi ya mawakala ajapokea pesa toka kwa mteja anaanza kuruhusu muamala.

Baada ya tapeli kupokea pesa akamwambia binti mpe simu wakala, wakala kupokea simu tapeli akasema "mwambie huyo binti ameshatapeliwa" na wewe wakala ni mpumbavu na mjinga nishawatapeli unatumaje pesa kabla ujapokea pesa" kisha akakata simu.

Wakala akajaribu kuustopisha muamala tayari sekunde ulikuwa ushatolewa. Wakala kambana binti, binti kamuonyesha message aliyotumiwa hela, ni message ya kuforwadiwa yaani message feki. Means binti hana pesa hata mia mbovu.

Wakala kamuweka chini ya ulinzi binti akitaka ampeleke kwenye vyombo husika mabodaboda wakasema huyu binti boss wake tunajua ikashauriwa wamuone boss wake. Kufika kwa boss kuelezwa boss akamwambia wakala hivi inakuaje unatuma pesa KWA mtu na ujapokea pesa mkononi kwanza? Huo ni mzigo wako siwezi toa hata mia"

Wakala akajibu kwamba binti aliniambia pesa anazo kwenye simu atatoa na mimi nikaamini. Maamuzi ya busara yakafanyika kwamba wachangie hasara yaani binti alipe nusu na wakala alipe nusu kwa uzembe wake.

Mme wa boss alitaka alibebe jukumu hilo yaani ailipe hio hasara toka kwa binti wa wakazi sababu anajua ni ajali tu imetokea, mke akatia ngumu maneno yakataka kuzuka mke akatoa maneno mme ikabidi ajitoe na kusitisha mpango wa kuilipa hasara hio Ili dada wa kazi awe na amani, hofu ni mke asijesema anamtaka mdada wa kazi sababu mke ni fyatu achagui maneno.

Muafaka binti atalipa elf 80 badala ya mia 50. Binti kakubali atalipa kwa awamu. Mchana anapigiwa tapeli akapokea akaelezwa akataja ni wakala gani akatajiwa jina la wakala wa tigo aliyemtumia pesa kwenye simu yake 0672312375 (uzoefu anawatapeli wengi alipouliza jina la wakala), tapeli akakumbuka akauliza mpo wapi akaambiwa ni kituoni hapa tumemshikilia binti kwa loud speaker mazungumzo yakiendelea mbele ya wakala, binti na boss tapeli akasema "ni kweli nimechukua pesa huyo wakala ndie mjinga nishawatapeli na pesa sirudishi siwezi rudisha pesa nimepewa na Mungu tairudisha vipi?"

Akaendelea kupiga mkwara "huyo binti hana makosa mwachie mara moja la sivyo nitawafanyieni kitu mbaya," akatishia mikwara ya uchawi (ignorance) kisha akaporomosha Sana matusi mazito ya 5G akasema "nimewaonea huruma hicho kipesa kidogo tu ndo mnapiga kelele je ningechukua nyingi je?' Akaendeleza matusi mazito Sana kwa aibu tukakata simu.

Jana tapeli akapigiwa simu akapokea (sauti ni ya kiume, lafudhi si ya mjini) akaambiwa arudishe hio pesa.Tapeli akaporomosha matusi mazito ya 10 G, eti hawezi rudisha pesa aliyopewa na MUNGU. Tapeli akatumiwa message " tulikuwa na shida na sauti yako tushaikamata tumeihifadhi kwenye chupa inafanyiwa kazi tegemea ugeni "tapeli akapiga simu anabembeleza anaomba msamaha kwamba" msifanye chochote haya ni maisha tu tusimfanye chochote, anarejesha hio pesa."

Akaomba Sana kwa sauti ya huruma na upole atumiwe namba arejeshe hio pesa Ili asidhurike, huku kwa nyuma ikisikika sauti nyingine ya kiume "Hakuna kurejesha pesa hapa."
Tapeli akatumiwa namba Ili arejeshe hela kwa madai yake.

Baada ya kupewa namba akatuma message yenye kuonyesha hela imeingia, hio message ikaja kama zile za kampuni ya simu na sio kama private number (changamoto kwa watu wa IT hawa wanaingiliaje mifumo ya kampuni za simu) message ya hela imekuja kupitia nembo ya kampuni ya airtel na sio kwa private number, ilipoangaliwa salio lina soma sifuri.

Means katuma message hewa. Kumpigia simu akapokea akaelezwa akasema "mbona nimekurudishieni hela yenu si mlituma laki na hamsini na nane? Ndio hio nimerejesha kupitia" KISHA akaendeleza matusi mazito akisema "nawatapeli waganga, wanajeshi, mapolisi, mahakimu, mawaziri sembuse nyie" akaendeleza matusi mazito Sana.

Huku akichimba mkwara "ungekuwa mjanja usingetapeliwa kata simu nipo kazini nawatapeli watu nitoe kiwingu unanipotezea mda kuna Kazi inaingia hapa" then akakata simu. Jioni akapigiwa "eeh unasemaje nipo home nakula ugali na familia" inasikika sauti ya kike kwa nyuma. Nimeweka sauti yake iliyorekodiwa akijigamba, muamala feki aliourejesha, majina ya usajili ya namba hizo mbili ya tigo na airtel.

Changamoto kwa mamlaka husika police, mamlaka ya mawasiliano, kampuni za simu na vyombo vingine ni watz wangapi wanatapeliwa kupitia njia hizi. Kumbuka pana watu awajui haya mfano wadada wa Kazi wapeni elimu. Mtu yeyeto akikuambia jambo KISHA akakuambia usiseme, au message yeyeto ya pesa sijui nimekosea sijui nini wawe na uelewa, matapeli wazee wa ile pesa bado wapo kazini.

Namba yake bado ipo hewani na anapokea tu simu swali anajiamini nini? Je, ni ignorance? Je, pana watu wa kampuni za simu anashirikiana nao? Je, anaingilia mifumo ya mawasiliano ya simu?

Kwa mliotaka kutapeliwa hii sauti si ngeni, hata mimi sio ngeni kwangu. Nimeleta kwenu tuelimishane. Naambatanisha sauti Kati ya tapeli na mtu mwingine.

View attachment 2477989View attachment 2477994View attachment 2477995View attachment 2477991
Wanapigwa wengi sana kwa mbinu hii, na ndio hutumiwa zaidi kwa sasa😬
 
Halafu bado yupo hewani sijui anajiamini vipi sijui anajua Hakuna mtu mwenye kumfatilia au sababu ya ujinga.
kuna jamaa yangu fulani yeye kasomea mambo ya cyber security sijui vidude gani sijui, sasa baada ya dada wetu wa mtaa kutapeliwa tukamuelekeza kwa mshakaji wetu ili amsake huyo tapeli tukamtie adabu, baada ya kuchek tukagundua jamaa yupo mikocheni.... tukiwa tunajiandaa na kuweka mipango sawa na kumshirikisha jamaa yetu ambae ni askari, yule askari akaweka protokali sawa pale kituoni then tukasema sasa tumcheki yupo wapi, ile kucheki tukagundua dakika tatu nyuma jamaa alikuwepo pale pale tulipokua sie kipindi tunamcheki mara ya kwanza halafu akamtumia meseji yule dada "utakufa kifo kibaya saana kwa kunifuatilia" 😀 😀 😀 watu wote tulitawanyika na kesi ikaishia hapo, tukawaachia polisi.
 
Back
Top Bottom