Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Habarini wakuu,
Heading isomeke "Matarajio yangu juu ya ujio wa album mpya ya Dizasta Vina (The Verteller)" Cc Wand Paw
Binafsi, tangu nilivyomfahamu huyu mtu wa kuitwa Dazasta Vina miaka michache iliyopita, amekuja kuwa mwana hiphop ambaye namsikiliza zaidi kwa hapa bongo Tz. Yaani kama nikiweka top 3 kulingana na nyimbo za hip hop za bongo ninazosikikiza sana kwa kila siku, chart yangu itakuwa hivi.
1. Dizasta Vina
2. Nikki Mbishi
3. Nash Mc
Kitu kikubwa ambacho kilinifanya niwe shabiki wake mkubwa ni uwezo wake wa kugusa vitu ambavyo wasanii wengi hawapendi/wanaogopa kuvigusa (Rejea; Kanisa, Kikaoni, Hatia II&III). Na pia uwezo wake wa kueleza matukio ya kawaida katika maisha yetu ya kila siku kwa njia ya kipekee kabisa. (Rejea; Hatia I, Nyumba ndogo, fallen Angel, Siku mbaya, Ndoano, kijogoo nk).
Hivi karibuni, Dizasta Vina alitangaza ujio wa album yake iitwayo The Verteller ambayo itatoka 27 December Mwaka huu. Album ambayo itakuwa na nyimbo 20. Hadi sasa, katika albamu hiyo zishasikika track tatu ambazo ni intro ya album (The verteller), Ndoano na No body is safe 3. Nikizisikiliza nyimbo hizi tatu pamoja na kujumlisha jinsi ambavyo namfahamu Dizasta Vina, napata picha kuwa huenda The Verteller ikawa album ya hip hop bora kabisa kuwahi kutengenezwa katika miaka ya hivi karibuni au hata tangu mziki wa hip hop ilipoingia tz,(maana hakuna anayejua).
Tusubiri na tuone.
Nini matarajio yako juu ya ujio wa album mpya ya dizasta vina?
Ila nawe Kendrick Lamar fanya utoke huko mafichoni aisee, Tunahitaji album mpya mbuzi wewe.....