Matarajio yangu juu ya ujio mpya Dizasta Vina (The Verteller)

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Habarini wakuu,

Heading isomeke "Matarajio yangu juu ya ujio wa album mpya ya Dizasta Vina (The Verteller)" Cc Wand Paw

Binafsi, tangu nilivyomfahamu huyu mtu wa kuitwa Dazasta Vina miaka michache iliyopita, amekuja kuwa mwana hiphop ambaye namsikiliza zaidi kwa hapa bongo Tz. Yaani kama nikiweka top 3 kulingana na nyimbo za hip hop za bongo ninazosikikiza sana kwa kila siku, chart yangu itakuwa hivi.
1. Dizasta Vina
2. Nikki Mbishi
3. Nash Mc

Kitu kikubwa ambacho kilinifanya niwe shabiki wake mkubwa ni uwezo wake wa kugusa vitu ambavyo wasanii wengi hawapendi/wanaogopa kuvigusa (Rejea; Kanisa, Kikaoni, Hatia II&III). Na pia uwezo wake wa kueleza matukio ya kawaida katika maisha yetu ya kila siku kwa njia ya kipekee kabisa. (Rejea; Hatia I, Nyumba ndogo, fallen Angel, Siku mbaya, Ndoano, kijogoo nk).

Hivi karibuni, Dizasta Vina alitangaza ujio wa album yake iitwayo The Verteller ambayo itatoka 27 December Mwaka huu. Album ambayo itakuwa na nyimbo 20. Hadi sasa, katika albamu hiyo zishasikika track tatu ambazo ni intro ya album (The verteller), Ndoano na No body is safe 3. Nikizisikiliza nyimbo hizi tatu pamoja na kujumlisha jinsi ambavyo namfahamu Dizasta Vina, napata picha kuwa huenda The Verteller ikawa album ya hip hop bora kabisa kuwahi kutengenezwa katika miaka ya hivi karibuni au hata tangu mziki wa hip hop ilipoingia tz,(maana hakuna anayejua).

Tusubiri na tuone.

Nini matarajio yako juu ya ujio wa album mpya ya dizasta vina?

Ila nawe Kendrick Lamar fanya utoke huko mafichoni aisee, Tunahitaji album mpya mbuzi wewe.....
 
Dogo yupo vizuri, nimememfahamu toka anazaliwa na nimekua nae. Nilipenda sana hiphop zamani na nilikua natungatunga mistari yangu.
Alianza pia kushawishika kutunga yake na hapo mapinduz yakafanyika. Nikawa napenda mistar yake na mpaka sasa nimebaki kua mpenzi msikilizaji
 
Moja kati ya watu ninaowaelewa zaidi kwenye Hip hop ukiniambia nikupe orodha ya wana hip hop huyu jamaa ni namba moja kwangu sio hivi vijamaa vyenu vibana pua vinachana kwa kubenjua benjua vidomo fuc*n
 
Habarini wakuu...

Heading isomeke "Matarajio yangu juu ya ujio wa album mpya ya Dizasta Vina (The Verteller)" Cc Wand Paw

Binafsi, tangu nilivyomfahamu huyu mtu wa kuitwa Dazasta Vina miaka michache iliyopita, amekuja kuwa mwana hiphop ambaye namsikiliza zaidi kwa hapa bongo Tz. Yaani kama nikiweka top 3 kulingana na nyimbo za hip hop za bongo ninazosikikiza sana kwa kila siku, chart yangu itakuwa hivi.
1. Dizasta Vina
2. Nikki Mbishi
3. Nash Mc

Kitu kikubwa ambacho kilinifanya niwe shabiki wake mkubwa ni uwezo wake wa kugusa vitu ambavyo wasanii wengi hawapendi/wanaogopa kuvigusa (Rejea; Kanisa, Kikaoni, Hatia II&III). Na pia uwezo wake wa kueleza matukio ya kawaida katika maisha yetu ya kila siku kwa njia ya kipekee kabisa. (Rejea; Hatia I, Nyumba ndogo, fallen Angel, Siku mbaya, Ndoano, kijogoo nk).

Hivi karibuni, Dizasta Vina alitangaza ujio wa album yake iitwayo The Verteller ambayo itatoka 27 December Mwaka huu. Album ambayo itakuwa na nyimbo 20. Hadi sasa, katika albamu hiyo zishasikika track tatu ambazo ni intro ya album (The verteller), Ndoano na No body is safe 3. Nikizisikiliza nyimbo hizi tatu pamoja na kujumlisha jinsi ambavyo namfahamu Dizasta Vina, napata picha kuwa huenda The Verteller ikawa album ya hip hop bora kabisa kuwahi kutengenezwa katika miaka ya hivi karibuni au hata tangu mziki wa hip hop ilipoingia tz,(maana hakuna anayejua).

Tusubiri na tuone.

Nini matarajio yako juu ya ujio wa album mpya ya dizasta vina?

Ila nawe Kendrick Lamar fanya utoke huko mafichoni aisee, Tunahitaji album mpya mbuzi wewe.....

Mkuu tupia iyo track ya rejea apa kama unayo
 
Album cover
2020-11-22 06.25.12.png

Tracklist
2020-11-22 06.23.07.png
 
Album bora ya HipHop ilikuwa Soga za Mzawa, hii The Verteller pia itaishia kupuuzwa tu.
 
Back
Top Bottom