Hapana.
Kwa bahati mbaya mwanadamu alipoumbwa kama kiumbe-jamii (social being), hakuumbwa peke yake. Hivyo, maamuzi yote anayoyafanya, yawe mema au mabaya; yanakuwa na athari hadi kwa wengine.
Mtu anapoamua kukata miti, sio kwamba athari hizo zitaishia kwake tu, zitaathiri wote waliounganishwa na wanaoyategemea hayo mazingira kwa namna moja ama nyingine. Adam na Eva walipotenda dhambi, dhambi hiyo haikuwaathiri wao tu, inatuathiri hadi sisi leo hii.
Kama ulivyosema, watoto ambao hawana dhamiri, wala ambao hawaelewi jambo lolote na wasiokuwa na hatia bado wanapatwa na huu ugonjwa, ni kwa sababu ya wale wanaowazunguka. Hawa watoto na watu wengine wasiokuwa na hatia ni waathirika wa wanadamu wenzao wanaoamua kutokufuata utaratibu mzuri aliouweka Mungu.
Mfano mzuri ni uamuzi wa Kaini kumuua Habili. Je, Habili alikuwa na hatia yoyote kustahili kifo? Je, hakufa? Je, Mungu hakuwa fair?
Fairness ya Mungu ipo kwenye matokeo ya maamuzi tunayoyafanya.
Tunapoongelea dhamiri, ni kuwa dhamiri haimlazimishi mtu kufanya uamuzi mzuri, bali inamshawishi na kumpa tahadhari ya matokeo ya uamuzi atakaoamua kuufanya. Dhamiri inasisitiza wema.
Ndio maana kuna watu tunasema dhamiri zao zimekufa, sio kwa sababu wao hawana dhamiri, hapana, bali wameamua kuishi bila kuisikiliza hiyo dhamiri.