Matatizo: Je, ni uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu?

So kama nimekuelewa vizuri unamaan ya kwamba covid-19 ni kind of adhabu kwa mwanadamu kutokana na kutokwenda na utaratibu uliowekwa sio? Je Mungu hana uwezo wa kuyazuia hayo hata kama kwa wasio na hatia basi?
 
So kama nimekuelewa vizuri unamaan ya kwamba covid-19 ni kind of adhabu kwa mwanadamu kutokana na kutokwenda na utaratibu uliowekwa sio? Je Mungu hana uwezo wa kuyazuia hayo hata kama kwa wasio na hatia basi?
Ukisema adhabu unakuwa unakosea, tumia neno matokeo.

Mwenyezi Mungu ameshakupa maelezo kupitia wanasayansi wake; unawe mikono kwa kutumia maji safi yanayotiririka, uepuke mikusanyiko ya watu wengi, uepuke migusano, n.k. huo ndio utaratibu wake mwema wa kuepuka Covid-19.

Ukiufuata huo utaratibu, hautaipata hiyo Covid-19, na usipoufuata huo utaratibu utapata Covid-19. Wewe kwa kutumia utashi na uhuru wako, ukaamua kutokufuata huo utaratibu, na matokeo yake, ukaipata hiyo Covid-19; je, ni kosa la Mungu au la kwako? Hiyo ni mosi.

Pili; Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa uhuru kamili wa kufanya maamuzi bila kuingiliwa na mtu, hata Mungu mwenyewe haingilii uamuzi unaoufanya, japokuwa ana uwezo huo.

Ameamua kutokuingilia uamuzi wako kwa kuwa ameamua kutojipinga mwenyewe, ameamua kutovunja utaratibu aliojiwekea kwa sababu utaratibu huo ni mzuri.

Ili kuhakikisha unafanya uamuzi ukiwa na uhuru kamili na uamuzi wako ukawa mwema, Mwenyezi Mungu amemuwekea kila mtu dhamiri (conscience) ambayo humuasa na kumshawishi kuamua na kutenda mema.

Kwahiyo Mungu ana uwezo wa kufanya chochote, lakini ameamu kutokuwa dikteta.
 
Achana na sisi tulio na huyo dhamiri mkuu...vp kuhusu vichanga na watoto wanakufa na hizo majanga....huoni hapo hafanyi fair? Na je kama ametuwekea dhamiri ambayo haina wasi wasi means ni perfect kama yeye hiyo damiri ya kufanya vinginevyo inatoka wapi? Au kuna mahali aliloose point?
 
Dah mleta mada ana theory zake bhana [emoji23][emoji23][emoji23]
Existence ya time inakuja kuwa proved na theory yangu ya air kama source ya energy and everything. Hiyo air pia source yake ni Mungu.

Kwa maelezo yako hayo movement ya hizo photons na photons zenyewe zinamtegemea Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwa nini wanadamu tunahangaika sana kuprove uwepo wa sir God

Kwa nini asijitokeze tu malaika wapange maspika hafu simple ani watu waamini

Daaah [emoji23][emoji23][emoji112]

Anyway naamini Mungu yupo

Ila mshua naona anafeli sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana.

Kwa bahati mbaya mwanadamu alipoumbwa kama kiumbe-jamii (social being), hakuumbwa peke yake. Hivyo, maamuzi yote anayoyafanya, yawe mema au mabaya; yanakuwa na athari hadi kwa wengine.

Mtu anapoamua kukata miti, sio kwamba athari hizo zitaishia kwake tu, zitaathiri wote waliounganishwa na wanaoyategemea hayo mazingira kwa namna moja ama nyingine. Adam na Eva walipotenda dhambi, dhambi hiyo haikuwaathiri wao tu, inatuathiri hadi sisi leo hii.

Kama ulivyosema, watoto ambao hawana dhamiri, wala ambao hawaelewi jambo lolote na wasiokuwa na hatia bado wanapatwa na huu ugonjwa, ni kwa sababu ya wale wanaowazunguka. Hawa watoto na watu wengine wasiokuwa na hatia ni waathirika wa wanadamu wenzao wanaoamua kutokufuata utaratibu mzuri aliouweka Mungu.

Mfano mzuri ni uamuzi wa Kaini kumuua Habili. Je, Habili alikuwa na hatia yoyote kustahili kifo? Je, hakufa? Je, Mungu hakuwa fair?

Fairness ya Mungu ipo kwenye matokeo ya maamuzi tunayoyafanya.

Tunapoongelea dhamiri, ni kuwa dhamiri haimlazimishi mtu kufanya uamuzi mzuri, bali inamshawishi na kumpa tahadhari ya matokeo ya uamuzi atakaoamua kuufanya. Dhamiri inasisitiza wema.

Ndio maana kuna watu tunasema dhamiri zao zimekufa, sio kwa sababu wao hawana dhamiri, hapana, bali wameamua kuishi bila kuisikiliza hiyo dhamiri.
 
Dah mleta mada ana theory zake bhana [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha...

Ndio Mkuu, mimi na rafiki yangu mmoja tuna-develop theory zetu zinazohusu Quantum Physiscs.

Tulianza kuzi-develop mwaka 2013, tupo kwenye hatua nzuri na tunajitahidi tuwe tumezimaliza kabla ya 2028 na tuwe tumeshazi-present na kuzi-publish kwenye scientific society kabla ya 2030.
 
Hivi kwa nini wanadamu tunahangaika sana kuprove uwepo wa sir God
Kwa sababu watu wapo busy sana ku-prove absence ya Mwenyezi Mungu.

Kwa nini asijitokeze tu malaika wapange maspika hafu simple ani watu waamini
Kwa sababu Mwenyezi Mungu hajaamua kufanya hivyo.

Anyway naamini Mungu yupo

Ila mshua naona anafeli sana
Hahaha... Na huu ndio ukweli, ambao utakuweka huru kama ukiamua kuupokea kwa imani na dhati.
 
Duh...sa alikuwa na maana gani kuumba dhamiri ya kutega mkuu...why atuwekee mtego wakati alikuwa na uwezo wa kuumba dhamiri kamili ya kutenda yatakayompendeza tu ili kusiwe na nafasi ya kuja kutupanish?
 
Duh...sa alikuwa na maana gani kuumba dhamiri ya kutega mkuu...why atuwekee mtego wakati alikuwa na uwezo wa kuumba dhamiri kamili ya kutenda yatakayompendeza tu ili kusiwe na nafasi ya kuja kutupanish?
Dhamiri haikutegi, inakukumbusha na kukushawishi kutenda mema.

Kama Mwenyezi Mungu angetuwekea option ya kutenda mema tu, tusingekuwa huru.

Yeye anataka tuwe huru.
 
Dhamiri haikutegi, inakukumbusha na kukushawishi kutenda mema.

Kama Mwenyezi Mungu angetuwekea option ya kutenda mema tu, tusingekuwa huru.

Yeye anataka tuwe huru.
Kama dhamira yake tuwe huru..mbona anatuadhibu kwa makosa ambayo angeweza kuyafanya tukayaepuka tu mkuu.
 
Kama dhamira yake tuwe huru..mbona anatuadhibu kwa makosa ambayo angeweza kuyafanya tukayaepuka tu mkuu.
Nimekuambia hakupi adhabu, hayo ni matokeo ya uamuzi tunaoufanya, ambayo yanajulikana kabisa kabla ya kufanya uamuzi.
 
Sawa bwana scientist

Ukikutana na sir God

Mwambie maisha magumu huku

Why atuletee makolona

Ya nini ssa

Mwambie watumishi wake mapadri na masheikh wanakufa kama kuku

Kama anaweza aje fasta tuamshe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivyo basi na Mungu ana chanzo, hakuibuka from nowhere. Tueleze chanzo chake.. ukishindwa ulichoandika hapa hakina maana Wala ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa bwana scientist

Ukikutana na sir God

Mwambie maisha magumu huku

Why atuletee makolona

Ya nini ssa

Mwambie watumishi wake mapadri na masheikh wanakufa kama kuku

Kama anaweza aje fasta tuamshe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha...

Mkuu, Mungu hajaleta Covid-19. Tumeileta sisi wenyewe kwa kutofuata utaratibu wake mwema.

Bahati mbaya haijalishi kama wewe ni Padri au Mpagani, usipofuata utaratibu huo, matokeo huwa yaleyale tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…